Yanga mpira ni sayansi mpira ni pesa

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Nadhani kama ni sindano itakuwa dawa imewakolea. Uongozi wa Yanga unatakiwa utambue kuwa duniani kote mpira umebadilika, mpira umekuwa ni sayansi maana yake lazima ufundishwe na walimu/kocha waliosoma haswa. Pia mpira ni Pesa na Pesa sio za kuchangisha Mashabiki na wanachama, Pesa ni za Uwekezaji.Hivyo uongozi wa Yanga najua kauli mbiu ya Klabu ya Simba ya kuwa, "IGE UFE" haikwepeki mnatakiwa muingie kwenye Mchakato wa Uwekezaji kwa maana ya kuwa Kampuni. Acheni mpira wa kizamani hii ni Karne ya Sayansi na Uwekezaji.Achaneni na Mawazo ya kina mzee Akilimali yamepitwa na wakati.
 
Kuiga mambo mazuri sio mbaya,
Kwa miaka mingi simba imekua ikianzisha mambo meengi mazuri baadae yanga inaiga,

wafate nyayo za simba kwa kila jambo ila hawatowacha kuliwa,wafanye wafanyavyo tabu ipo palepale
 
Back
Top Bottom