Yanga, Manji asije akawa Kisingizio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga, Manji asije akawa Kisingizio

Discussion in 'Sports' started by Elli, Mar 5, 2011.

 1. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,116
  Trophy Points: 280
  Wapendwa, Mimi ni mshabiki sana wa michezo kwa ujumla hasa football ila kuna jambo moja huwa linanekera sana sana. Tumeshajenga tabia mbaya sana kwenye michezo yetu ya kuweka visingizio mbele.

  Kuna mifano lukuki ambayo timu zetu iwe za ngumi, riadha, football au netball wanapopoteza mchezo basi huwa kunatokea visingizio kibao. leo Simba na Yanga watacheza, mchezo huu ni mzuri lakini kuna tatizo la kiutawala au labda la kimaslahi kwa upande wa Viongozi na Mfadhili wao Manji....

  Kila mtu alishuhudia wiki hii habari kuwa Manji mara kaondoka mara karudi mara sijui hivi au vile, ili mradi tu.

  Naomba sana sana, isije kuwa kisingizo mkapoteza mchezo eti kwa sababu kuna matatizo ya kiutawala kwenye timu yenu, nasema hivi kwa sababu kuna kipindi Simba walipoteza michezo kibao, kuulizwa rit ni kwa sababu ya akina Dalali na uongozi wake kuna matatizo.

  Mtaingia uwanjani mkiyajua hayo, tuelezeni mapema kabisa, tafuteni alternative na sio kuja na visingizio. nawatakia kila la heri wote Simba na Yanga. Mcheze kwa amani na washabiki wenu wafurahi.
   
Loading...