Yanga kunani paleeeeee....!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga kunani paleeeeee....!!!!!!

Discussion in 'Sports' started by sinafungu, May 7, 2012.

 1. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Duuh roho inaniuma sana, naomba wanayanga wenzangu tujuzeni wengine tusofahamu kinachoendelea pale jangwani, hivi tatizo pale ni ,
  1. kocha...........
  2. uongozi.......
  3. wachezaji........
  na nini kifanyike hiii ni aibu sana.
   
 2. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kaka nitatia team pale Mjengoni baadaye kupata hali halisi ya leo(siku 1 baada ya kuvuliwa nguo jana) lakini kwa jinsi ninavyofahamu mimi tatizo pale ni uongozi,viongozi wameshindwa kuendesha team kiufanisi,wachezaji na makocha hawalipwi mishahara kwa wakati,hakuna umoja kabisa makundi mengi yamezaliwa,viongozi waliokuwa na msaada mkubwa kuliko hata huyo Mwenyekiti wamejiengua kama kumsusia team hivi na hata kama umeangalia ile mechi utaona wachezaji wa Yanga walikuwa wanacheza ilimradi wameugusa mpira hakukuwa na morali ile tuliyoizoea wanayokuwaga nayo siku wanayocheza na Simba,na ni kama vile kuna wachezaji waliokuwa wameandaliwa(pengine labda na kundi fulani) kutengeneza matokeo ya namna ile na ndo maana ilifika kipindi hata kipa Said Mohamed alitaka kugomea penalt moja.
  Sasa kwa maoni yangu,kinachotakiwa kufanyika ni:-
  1.Uongozi kuondoka,wa'resign tuchague watu wenye uwezo wa kuiendesha Yanga kiufanisi.
  2.Kupunguza wachezaji wote wasio na manufaa kwa team ambao wanaweza kufikia hata 20,na kusajili wengine watakaoweza kuiletea Yanga matokeo chanya.
  3.Kubadili benchi zima la ufundi,Papic aachwe aende zake na Minziro hana jipya amesha'prove failure mara zote alizoachiwa team,watafute kocha mpya kutoka nje.
  4.Kurudisha umoja kati ya Viongozi na Wapenzi wa Yanga wenye uwezo wa hata kuisaidia team kwa fedha zao binafsi pale inapolazimika.

  Mwanachama wa Yanga.
   
 3. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Na muwaambie viongozi wenu waache kusajili wachezaji kwa majina tu.. Ati mchezaji kisa jina Asamoah basi ndio mnamsajili bila ya kujua kiwango chake.. Au yule mwingine Nape.. Mwili ule kama mnyanyua chuma.. Halafu punguzeni kuongea sana.. Na mwisho mkubali mmefungwa na timu ambayo iko juu kimpira na yenye wachezaji wenye viwango.. Tunawahitaji msimu ujao muwe challengers wetu vinginevyo Azam watachukua nafaci yenu permanently..
   
Loading...