Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Taarifa za ndani za CCM ni kwamba mpaka sasa kumetokea mgawanyiko; wapo wanachama na baadhi ya viongozi wa CCM ambao wameunga mkono madai ya wananchi kuzitaka mamlaka zihakiki tuhuma dhidi ya Kada wa CCM na mkuu wa mkoa wa DSM bwana Paul Makonda almaarufu Daudi Bashite, juu ya vyeti vya kitaaluma. Na kundi lingine ambalo linaamini kwamba hata kama mkuu huyo alifeli darasa la saba au hata awe hakufika darasa la saba Kwa maslahi ya c...hama, akingiwe kifua.
Uongozi wa juu wa chama hicho umewaagiza wanachama kutokukuza madai hayo, na badala yake wajiandae Kwa mkutano mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwezi huu wa machi, kama maandalizi ya kubadili katiba ya chama hicho, iendane na matakwa ya mwenyekiti wao Mhe. Magufuli. Wasomi mbalimbali na wachambuzi wa masuala ya kiiasa wamedai kuwa CCM inakoelekea, inarudi zama za 'Kudumisha fikra za mwenyekiti'.
Takribani wiki mbili sasa, mkuu wa mkoa wa DSM amekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na mijadala mbalimbali, juu ya tuhuma dhidi yake, kwamba anatumia vyeti ambavyo sio vyake, mbali na kufeli kabisa mtihani wa kidato cha NNE Kwa kupata alama Sifuri, pia anasemekana alighushi vyeti.
Ndani ya CCM kinachoendelea ni kulazimishana na kuonyana kwamba wamuache Bashite aendelee na ukuu wa mkoa wasihoji taaluma yake na historia yake ya elimu.