Yanayojiri Mashariki ya Kati

Yanayojiri Mashariki ya Kati

Didododi

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2023
Posts
351
Reaction score
475
Bei ya mafuta ilipanda baada ya Iran kurusha makombora ya balistiki dhidi ya Israel na kuzua hofu ya mzozo mkubwa katika eneo la Mashariki ya Kati ambao unaweza kuvuruga usambazaji wa mafuta.

Brent crude - kigezo muhimu cha bei ya mafuta kimataifa - kilipanda kwa zaidi ya 1% hadi $74.40 kwa pipa.

Wakati wa biashara Jumanne, kigezo hicho kilipanda kwa zaidi ya 5%. Iran ni nchi ya saba kwa uzalishaji wa mafuta duniani, kulingana na Utawala wa Taarifa za Nishati wa Marekani, na mwanachama wa tatu kwa ukubwa wa shirika la wazalishaji wa mafuta la Opec.

Wafanyabiashara pia wanahofia kuongezeka kwa mzozo wa kijeshi katika eneo hilo kunaweza kuathiri usafiri wa meli kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz.

Njia hiyo ya meli - ambayo iko kati ya Oman na Iran - ni muhimu kwa biashara ya kimataifa ya mafuta na 20% ya bidhaa za ulimwengu zinapitia humo.

Wanachama wengine wa OPEC Saudi Arabia, UAE, Kuwait na Iraq pia hutuma mafuta mengi wanayouza nje kupitia Mlango huo wa Bahari.

BBC
 
Taarifa nakupa za ndani kabisa .

Israel amepanga kushambulia siku ya ijumaa Iran , targets zikiwa ni visima vya mafuta na kambi za jeshi ....Kuna 76% ya kushambulia siku ya ijumaa. Kumbuka siku ya Ijumaa AYATOLLAH ataongoza sala ya wazi na ndio israel itapiga huo msikiti.
 
Taarifa nakupa za ndani kabisa .

Israel amepanga kushambulia siku ya ijumaa Iran , targets zikiwa ni visima vya mafuta na kambi za jeshi ....Kuna 76% ya kushambulia siku ya ijumaa. Kumbuka siku ya Ijumaa AYATOLLAH ataongoza sala ya wazi na ndio israel itapiga huo msikiti.
Itakua ni uzembe wa Hali ya juu sana, maana Qur an 4:102 imeshamueleza wakati wa Hali ya vita wanatakiwa waswali namna Gani.
 
Back
Top Bottom