Bunge la 11, Mkutano wa 3, Kikao cha 30
Maswali na Majibu
Swali : Je serikali imejipanga vipi kuwezesha wananchi kuanzisha viwanda?Maswali na Majibu
Majibu : Serikali inafuatilia viwanda vilivyobinafsishwa, Serikali inahimiza halmashauri kutenga maeneo ya uwekezaji, wawekezaji wazawa wanahimizwa kushirikiana na wawekezaji wa nje ili kuwekeza katika viwanda.
Pia serikali kupitia taasisi zake za kibenki inawawezesha wananchi kuwekeza.
Swali : Ni lini serikali itakiona kiwanda cha Manonga ili kiweze kufanya kazi?
Majibu : Waziri wa viwanda yupo tayari kwenda Manonga, serikali imedhamiria kufufua kiwanda cha Mononga Tabora. Aidha kiwanda hicho kilisitisha kuendelea kuzalisha kutokana kuzalisha juu ya kiwango.
Swali : Je serikali imeshalipa stahiki za wastaafu wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki iliyovunjika?
Majibu : Serikali imeshalipa stahiki za wastaafu 31,519 kati ya 31,831 kiasi cha shilingi bilioni 115.3, aidha wastaafu waliolipwa ni wale waliojitokeza.
Aidha mwaka 2013 serikali iliwalipa wastaafu wengine 219 kiasi cha shilingi bilioni 1.8 na kufanya kiasi chote kilicholipwa kuwa ni shilingi bilioni 116.88.
Swali : Je serikali ina mpango gani wa kusambaza umeme katika wilaya ya Rorya? Na ni lini mpango wa REA awamu ya pili utakamilika. Na REA awamu ya tatu itaanza lini?
Majibu : Mpango wa REA awamu ya pili umekamilika kwa 15%, aidha serikali imemtaka mkandarasi kuharakisha mpango huu, Awamu ya pili ya REA itakamilika Juni 2016. Mpango wa REA awamu ya tatu utaanza Julai 2017.
Swali : Ni kiasi gani cha fedha mgodi wa Bulyankulu ulitumia kwa ajili ya ujirani mwema?
Majibu : Mgodi huo ulitumia Dola za marekani milioni 1.98 sawa na shilingi bilioni 4.4 za kitanzania. Aidha mgodi pia unaajiri wafanyakazi wazawa kwa kushirikiana na Halmashauri.
Swali la Nyongeza : Ni kiasi gani halmashauri inapata kutoka kwenye mgodi wa Kiwira?
Majibu : Mgodi wa Kiwira haujaanza kazi na upo katika hatua za mwisho, Ikiwa mgodi huu utaanza kazi, halmashauri italipwa kodi ya 0.3% pia serikali itapata mrahaba na wafanyakazi zaidi ya 1000 wataajiriwa.
Swali : Ni lini barabara ya chuo kikuu cha Ardhi hadi Makongo hadi Goba na Tegeta hadi Madale itajengwa?
Majibu : Barabara hizo zipo katika mpango wa serikali wa barabara kwa kiwango cha lami. Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa kina wa barabara Tegeta hadi Madale umekamilika.
Aidha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya chuo kikuu cha Ardhi hadi Makongo hadi Goba utafanyika sambamba na ujenzi wa barabara hiyo. Aidha serikali imeshatenga fedha katika bajeti yake ya mwaka 2016/17.
Swali : Ni lini serikali itawezesha chuo cha DMI kuweza kutoa kozi ya usalama wa gesi na mafuta ili wananchi waweze ajiri kupata sekta ya mafuta na gesi?
Majibu : Serikali kwa kushirikiana na Norway na wadau wengine, ipo katika hatua ya mwisho kukamilisha hatua za mwisho kuanza kutoa kozi hii. Serikali inatarajia mpaka ifikapo mwaka 2019 kitakuwa kimeanza kutoa mafunzo hayo.
Aidha vyuo vya Dodoma na chuo cha madini vinatoa kozi za mafuta na gesi na kitakachoongezeka ni kozi ya usalama wa mafuta na gesi.
Swali : Ni lini ujenzi wa barabara ya Tanga, Pangani, Saadani hadi Bagamoyo utaanza?
Majibu : Barabara hii ipo chini ya sekretarieti ya Afrika ya Mashariki. Aidha Upembuzi yakinifu na Usanifu wa kina umeshakamilika.
Pia Benki ya maendeleo ya Afrika imeonesha nia ya kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii. Punde fedha hizo zikipatikana, ujenzi utaanza.
Serikali pia itatenga fedha kwa ajili ya fidia na kujazia ujenzi wa barabara hiyo.