Yanayojiri bungeni Dodoma leo tarehe 07/06/16

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Maswali na Majibu
Swali: Ni lini serikali itatekeleza ahadi yake ya kutekeleza miradi ya maji Iringa vijijini?

Majibu: Serikali inatekeleza miradi katika vijiji kumi na saba kwa sasa katika jimbo hilo.
Serikali inashughulikia kuwalipa makandarasi wote ambao wanakamilisha miradi ya maji.

Swali: Je serikali ina mpango gani wa kupitia mpango wa ugatuaji wa madaraka "d by d" ili kuondoa mgogoro kati ya wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wananchi?

Majibu: Kuwepo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ni kushusha madaraka kwa wananchi, ofisi ya rais TAMISEMI imeendelea kufanya majadiliano yanayowezesha ugatuaji huu wa madaraka. Aidha mfumo huu hauna mwingiliano wowote.

Swali la nyongeza: Je serikali haioni mfumo huu unawafanya wakuu wa wilaya wanakuwa ombaomba kwa wakurugenzi wa halmashauri?

Majibu: Suala hili halikubali, na serikali itafanya utafiti ili kufahamu kama lipo.

Swali: Je mradi wa barabara wa wilaya ya Mbinga vijijini utakamilika lini?

Majibu: Ulitarajia kukamilika tarehe 30/06/16 lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza, mradi huu unatarajia kukamilika 30/09/2016.

Awamu ya pili ya mradi huu itakamilika tarehe 30/01/2017

Swali: Ni lini ujenzi wa barabara ya Mlowa hadi Mvumi mision utaanza?

Majibu: Serikali inatambua umuhimu wa barabara hii. Azma ya serikali ya kujengwa iko pale pale. Kwa sasa itajengwa na ofisi ya rais TAMISEMI kupitia mfuko wa barabara ili iweze kupitika wakati wote.

Swali: Ni lini serikali itazipatia kata za Korogwe vijijini huduma ya mawasiliano?

Majibu: Serikali imeshaipatia fedha kampuni ya Tigo na mradi wa kuweka mawasiliano katika kijiji cha Kazara na mradi unatarajia kukamilika 30/06/16.

Aidha vijiji vya kata nyingine vilivyobakia zitawekwa katika miradi ya awamu ya pili na ya tatu itakayotekelezwa na kampuni ya Halotel.

Swali: Nini kauli ya serikali kwa kutokamilika kwa mradi wa Gwati katika jimbo la Nkasi Kaskazini?

Majibu: Serikali inatarajia kupeleka fedha 30 Juni 2016 ili kukamilisha mradi huo. Serikali itapeleka kiasi cha milioni 550 kwa ajili ya kumalizia mradi huo, fedha hizo ni ufadhili kutoka serikali ya Japan.

Swali: Je serikali itaanza lini kutekeleza mradi wa maji wa Bariadi, Maswa na Itilima?

Majibu: Tayari mkandarasi ameshaajiriwa kuandaa makabrasha ya zabuni. Mradi utagharimu kiasi cha £uro 313.

Awamu ya kwanza itagharimu kiasi cha £uro 105. Aidha serikali ya Ujerumani itachangia kiasi cha £uro 25, Pia mfuko wa green climate fund utachangia kiasi cha £85, mradi utachukua miaka miwili kukamilika. Aidha mkandarasi atakamilisha kuandaa makabrasha ya zabuni tarehe 30/06/2016.

Awamu ya pili ya mradi huu utagharimu kiasi cha £uro 208

Swali: Serikali ina mpango gani wa kutatua mgogoro wa eneo la Misukumilo mpanda mjini linalodaiwa kuwa jeshi la wananchi JWTZ?

Majibu: Kutokana na sababu za kiinteligensia serikali ilikabidhi eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 3500 kwa jeshi la kujenga taifa na kulipa fidia kwa wananchi. Aidha serikali inatarajia kulipima tena eneo hilo na litapungua toka ekari 3500 hadi 2800.

Swali: Je kwa nini serikali isibadilishwe sheria ya leseni za magari amabyo inamlazimisha mwananchi kulipia kodi gari iliyokaa muda mrefu bila kutumika? Je serikali haioni inawaibia wananchi wake?

Majibu: Kodi hiyo ipo kwa mujibu wa sheria. Hakuna msamaha wa kodi kutokana na kwa gari iliyokaa bila kutumika kwa muda mrefu. Kupitia sheria hii, serikali haiwaibii wananchi.

Aidha serikali inapitia upya sheria hii na kuona namna kuiboresha.

Swali la nyongeza: Je serikali ina mpango gani wa kuboresha stika za magari ili kudhibiti stika bandia?

Majibu: Serikali inaleta mswada utakaoshughulikia mambo mbalimbali kuhusu kodi. Na kwa sasa unatumika mfumo wa kielektroniki wa kutoa stika hizo.

Swali: Je serikali ina mkakati gani wa kuongeza bajeti ya wizara ya maliasili na utalii?

Majibu: Wizara kupitia bodi ya utalii, imetenga kiasi cha shilingi bilioni 2.7 kwa ajili ya kutangaza vivutio vya kitalii vilivyo Tanzania, hili ni ongezeko la 16.7 ukilinganisha na mwaka 2015/16.

Serikali ina mpango wa kuboresha vyuo vitatu vya utalii. Aidha serikali italegeza masharti yaliyopo wakati wa kuanzisha kampuni za kitalii.

Swali: Je kisiwa cha shungimbili kimeuzwa shilingi ngapi?

Majibu: Kisiwa cha Shungimbili hakijauzwa, aidha kimeingizwa katika mpango wa kampuni inayojenga loji katika kisiwa hicho. Mradi ukikamilika, tozo zitaendelea kama kawaida.
 
Back
Top Bottom