Yanayoendelea Uganda kwa Bobi Wine family na wapinzani hata shetani anashangaa

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
5,159
5,399
Ktk biblia imeandikwa kuwa zitiini mamlaka zilizowekwa ikiwa ni msisitizo kuwatii viongozi wote wa umma na jeshi kwa ujumla kwa maamzi yote yanayoamriwa.

Mambo yalianza kuwa tofauti kwa mfalme Nebkadneza alipoonja shubiri kutoka kwa vijana mahiri Daniel,Shadrake misheck na Abdnego walipokataa kutii amri ya dikteta mfalme Nebkadneza.

Wakasema hatuwezi kuitii hiyo sanamu na kuisujudia wakati yupo Mungu wa kweli apaswaye kuabudiwa ktk roho na kweli na siyo hii sanamu yako.

Mfalme alitoa amri akitumia katiba katili ya nchi na kuamru moto mkali ili vijana wachomwe moto na hakufanikiwa kabisa huku akiwaambia enyi vijana hivi hamjui kuwa imeandikwa kuzitii mamlaka hamjui ya kuwa mimi mfalme Nebkadneza nimewekwa na Mungu bado vijana hawamkuelewa.

Ingawa yametokea kwingi duniani afrika lakini yanayoendelea Uganda ni funika bovu.Askari wa Uganda na serikali yake wameua wapinzani na raia mno lakini waliosalia wameendelea kupambana mpaka mwisho.

Juzi serikali imeamru walinzi binafsi nyumbani kwa Bob wine kuondolewa haieleweki wakiwaondoa ili wafanyaje?.Bob Wine anapitia maumivu kama wanaharakati wengine afrika walivyoteseka Kensaro Wiwa nigeria,Tundu Lissu Tz,Kiza Besigye,Mandela Nelson na wengineo.

Funga kazi ni video inayosambaa mtandaoni ikiwaonesha askari wa Uganda wakimtesa mke wa Bob wine na mtoto anayeonekana kuwa ni mwanaye wakimvua nguo na kumwacha uchi hadharani mbele ya mwanaye huku wakimkimbiza mtoto asione mateso anauofanyiwa mama huyo.

Nasimama ktk mstari wa haki za binadamu kuwa sioni sababu ya serikali ya Uganda kufanya haya kwa raia mwenzao.Udhalilishaji huu unawadhalilisha wanawake wote duniani popote walipo.Ni nani anayependa mama yake afanyiwe hayo hadharani na abakie huru.Wanaume pia hudhalilishwa ila udhalilishaji kwa mwanamke huyu mke wa Bob wine umevuka mipaka yote.

Nina imani hata SHETANI amezidiwa mbinu na askari wa serikali ya Uganda kwa ubunifu wao.Ni heri watu wafe,wadhalilike,wabaki walemavu,wabakwe na kupata kila aina ya teso ili viongozi wa vyama tawala waendelee kutawala.HAIKUBALIKI.

JUMUIYA ZA KIMATAIFA, ASASI ZA HAKI ZA BINADAMU ZIINGILIE KATI JUU YA UDHALILISHAJI HUU ULIOFANYIKA KWA MKE WA BOB WINE.JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI HAINA UBAVU WA KUKEMEA UOVU HUU KWANI WANACHAMA WAKE WENGI WANAUNGA MKONO TUKIO HILI.

####STOPTOUCHERMENTOVEROPPOSITIONWOMANIN AFRICA####.
 
Madaraka ya kulevya, huyu m7 alikuwa mwanamapinduzi kwelikweli lakini ndo hivyo kalewa madaraka, inategemea na makuzi ya mtu toka utotoni, hata hutu wine nae hatujui akipata madaraka atakuaje.

Wawe wanajitahidi kuwapa madaraka watu waluolelewa ndani ya ustaarabu.
 
Nimeamini madaraka yanalevya, tuseme m7 anataka kuongoza mpk mwisho wa uhai wake?

Mara abadilishe umri, mara katiba yaan viongozi wetu wa Afrika kama wana uraibu vile.
 
Hapa kwetu nako wanafanyiwa kama haya, watu kupotezwa, kupigwa, kudhalilishwa, kutumikia vifungo virefu bila yaushahidi, kupokonywa mali zao nk
Kambi moja viongozi afrika mashariki hakuna wa kumunyooshea Mseven kidole hakuna kabisa.
 
Back
Top Bottom