Yanayoendelea Sudani yanakatisha tamaa

Yanayoendelea Sudani yanakatisha tamaa

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Posts
11,660
Reaction score
11,664
Kwasisi wanamabadiliko yanayoendelea Sudan yanatukatisha tamaa sana.

Baada ya dikteta Bashiri kufurushwa tukaamini umma wa Sudan umeshinda.

Lakini ghafla jeshi ambalo lilikuwa beneti na wananchi wamewasaliti na jana tu jeshi limeua watu zaidi 30.

Limesema nchi itaendeshwa kijeshi hadi uchaguzi utakapoandaliwa

Kwa hali tusishangae Bashiri akarudi tena madarakani

Sisi miafirika ni taabu tupu
 
Nchi zote za Kidikteta Mafisadi wakubwaara zote wanakua ni majenerali na maafisa wa jeshi.

Hapo ukombozi utakuaja pale wanajeshi wenye vyeo vya kati watakapoamua kuwa upande wa wananchi mana wengi wanakuaga na maisha ya kawaida.
Wale majeneral wengi ni sehemu ya ufisadi wa Serikali ya kijeshi iliyotoka.
Hao wanazuga tu lakini wanalinda maslahi yao waliyojichotea wakati wa utawala dhalimu.

Hata hivyo Watashindwa Jeshi kuzima nguvu ya umma ni tabu sana hasa raisi anapotolewa madarakani .
Panakua na migawanyiko mingi sana.
Ya kikabila ,kirafiki na kimitizamo miongoni mwao. Wengine wanaamua kuungana na wananchi ambao ni ndugu zao maskini kuwalinda wasiuawa na watu walioshiba kwa ufisadi na madaraka na rasilimali za umma kwa muda mrefu.

Sudani soon itatulia tu na nguvu ya umma itashinda.
 
Wacha jeshi lishike jeshi lililainika likakubali kuunda serikali ya mpito ambayo raia ndio wangekuwa wengi.Waandamaji bado wakaendelea na vurugu na maandamano nchi inakuwa haitawaliki.Naunga mkono jeshi kushika nchi.Raia wa Sudan wamezengua.
 
Acha upotoshaji ww dogo, kwenye serikali ya mpito wanajeshi ndio walitaka kuwa wengi. Kibaya zaidi wanajeshi waliokuwa wanataka kuwa kwenye hiyo serikali ni wale waliokuwa na mafungamano na El Bashir. Ww lazima uunge mkono jeshi kulazimisha kuongoza, kwani hata hapa nyumbani vyombo vya dola ndio pumzi ya ccm. Ushahidi ni siku Magufuli alipopokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha.
 
Ndugu Yejodaya, ongezea, jeshi walikubaliana nao kuwa nusu kwa nusu uwaziri, ila hao viongozi wa waandamanaji wametaka majeshi yahukumiwe na waandamanaji, tena wamezidi kuwa wanapinga kila kitu.

Akili ya kusema ondokeni keenye power, na tutamifunga, tutalifumua jeshi nk.. hao wanajeshi mdio waliomuondoa Bashir na mkuu wa majeshi kipenzi cha bashir.
 
Acha upotoshaji ww dogo, kwenye serikali ya mpito wanajeshi ndio walitaka kuwa wengi. Kibaya zaidi wanajeshi waliokuwa wanataka kuwa kwenye hiyo serikali ni wale waliokuwa na mafungamano na El Bashir. Ww lazima uunge mkono jeshi kulazimisha kuongoza, kwani hata hapa nyumbani vyombo vya dola ndio pumzi ya ccm. Ushahidi ni siku Magufuli alipopokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha.
Waliompindua All bashir ni wanajeshi sio raia.Wanajeshi ndio wamemsweka ndani.Serikali ya mpito si ya kudumu raia wangekubali tu Ku share madaraka na wanajeshi . Sababu na jeshi lime changia kuondoka Al bashir.Swala la kusema ohh Walikuwa na mafungamano na Albbashir hayana uzito sababu Kila askari hula kiapo cha utii kwa Raisi aliyepo madarakani kama Hayupo kiapo yalipo tena na utii kwake haupo tena automatically
 
Wapenda mabadiliko ila bila nyie wenyewe kubadilika na ndio maana hakuna mabadiliko.
 
Wananchi wa Sudani walitanuka vichwa wakajisahau kwamba wao walikua na mchango mdogo sana kwenye mapinduzi

Kila wanachoshauriwa wanagoma, acha yawakute.
 
Waliompindua All bashir ni wanajeshi sio raia.Wanajeshi ndio wamemsweka ndani.Serikali ya mpito si ya kudumu raia wangekubali tu Ku share madaraka na wanajeshi . Sababu na jeshi lime changia kuondoka Al bashir.Swala la kusema ohh Walikuwa na mafungamano na Albbashir hayana uzito sababu Kila askari hula kiapo cha utii kwa Raisi aliyepo madarakani kama Hayupo kiapo yalipo tena na utii kwake haupo tena automatically

Wanajeshi ndio waliompindua Albashir? Wananchi waliandamana na wanajeshi wakaamua kuwa upande wa wananchi. Raia wamekubali kushare madaraka na wanajeshi, ila idadi ndio inayogomba.
 
Waandamanaji wamegeuka wanafki, vibaraka (wamejawa tamaa)

Jeshi ndo kila kitu kwenye nchi japo ni makosa kujihusisha katika siasa kwa baadhi ya nchi

Waandamanaji Wao wanataka kila kitu wahodhi tena kwa muda mfupi kwa kulazimisha na kutumia nguvu

Wamesahau Misri Mursi aliondolewa na jeshi japokuwa alikuwa rais halali aliyechaguliwa kidemokrasia

Watulize nyodo hata kama wakipewa selikali ya kiraia, jeshi likitaka kupindua linapindua tu bila kujali nani yupo madarakani
 
Back
Top Bottom