jamani ndugu zangu wa jf, huyu jirani yangu ni kaka ana mkubwa tu na ana miaka 26 sasa na ni mhitimu wa diploma ya procurement mwaka juzi 2014 katika chuo cha uhasibu mbeya (TIA) na kwa sasa anakaa kwa dada yake mkubwa wa kwanza huku maeneo ya soweto mbeya. sasa shemeji yake (mume wa dada yake) huwa anapenda kumfanyia vituko vya mara kwa mara ila huyu jamaa anabaki kimya sana na kukosa la kufanya, ila yakimshinda huwa ananipigiaga simu na kuniomba ushauri lakini na mimi ninakosaga la kumwambia kusema kweli.
huyo mumwe wa dada yake kuna wakati huwa anamwambia jamaa amuwekee maji ya kuoga, kumuandalia chakula au hata kuwa anampigia nguo pasi kama dada yake hayupo, ilhali anajua kuna watoto wadogo na wanaweza kufanya shughuli kama hizo, na mshikaji anakuwa hana jinsi anaamua tu kumtumikia kafiri ili apate yake ridhiki.
kwa sasa ameomba aje akae na mimi kwa muda ili aondokane na hii karaha ya huyu bwana mkubwa, na mimi ndio nipo ninafikiria mombi yake kwa sasa.
anatia sana huruma............
kwa hiyo ndio umeamua kummaliza kabisa........Angekuwa Dar ningemtesa X2 coz akishika kisimu chake kaz kukandia wanaume wa Dar jf kumbe anaishi kwa dada.Akalime viazi umalila.
yeye ni mwenyeji wa morogoro mkuuRafiki yako ni wa Dar?
kweli kabisa kabisa kaka. ila siwezi kumtosa best yangu huyu lazima nitakaa naye kidogo na kujaribu kumpa mwanga wa haya mema yaliyoshauriwa humu...........Mwambie ajisogeze...
Asibweteke asubiri kuajiriwa na kidiploma.
Aangalie mtaani kuna fursa gani....
Hata akifungua kigenge cha kisasa
Au akaangishe dagaa mchele feri aje kuuza
Kidogo kidogo asepe.
Au kwao mbeya kama wanalima ajihusishe na biashara ya mchele
Au afungue kibanda cha chips
Maana hapo anafukuzwa bila kuambiwa toka
MkwereHuyo Shemeji yake Ni Kabila gani kwanza?
Sio MKWERE mkuu!Anijibu kwanza kabila hiyo njemba ( shemeji yake na Msela) isije kuwa katoka makabila yenye Laana .
kwa hiyo ndio umeamua kummaliza kabisa........
Aangalie ustaarabu kusubiri ajira na hicho kidiploma anasubiri meli airport..... Ajiandae kutumwa na shemeji ake, atatumwa zaidi ya hapo