Yaliyowahi kusemwa kuhusu hayati Sokoine

BEATUS JOHN

New Member
Mar 23, 2017
1
0
Kuelekea kuadhimisha kumbukumbu ya Miaka 33 toka Hayati edward Moringe Sokoine afariki dunia na ibada ya kumbukumbu hiyo itafanyika nyumbani kwake Monduli juu.tarehe 12-4-2017.
 
Sokoine, E.M aliwahi kusemwa kama Kiongozi msimamia haki bila unafki na uoga.

Wakati anaanza harakati za kusaka wahujumu na wabadhirifu, alifika kwanza kwa rafiki yake na kumueleza adhima ambayo alipanga kuitekeleza kuanzia kesho yake asubuhi.

Rafiki yake huyo kwa kumjua vema Sokoine, usiku huo huo akawaamsha wanae na kuanza kwenda kutupa bidhaa na vitu vingine porini. Hii ni kuogopa kwamba Kesho yake, yeye angekuwa wa kwanza.

Kama alivyo-bet, asubuhi na mapema sana Sokoine alianzia kwake kupiga search na kutafuta kama alikuwa ni mmoja kati ya wahujumu Uchumi.

Pumzika kwa amani Mkuu Sokoine.
 
Safi sana,
 
Alikuwa na Wake wawili kinyume cha Mafundisho ya Imani yake ya Kikristo lakin cha Kushangaza kwny Mazishi yake Yaliongozwa Kidini na Viongozi wa Kubwa wa dini!

Lakin Makapuku wa huku Uswahilini wakiwa na Wake wawili Kanisa linawatenga!

Kwny Vita vya Uhujumu Uchumi alikurupuka Kama alivyokurupuka John Magufuli kwny Ishu ya Sukari Matokeo yake Taifa likayumba Kiuchumi kwa kuwa ilipelekea Watu wakamwaga Fedha, Vyakula na bidhaa kadhaa Muhimu Baharini kuliko kukutwa na Vikosi vya Utesaji vya Edward Moringe Sokoine!

Katika Muendelezo wa papara zake 1983 Mwalimu Nyerere ilimlazimu kukatiza Mapumziko ya X Mass Butiama kuja ku rescue hali baada ya kuwaweka ndani Wafanyabiashara wakubwa Akina Mzee John Rupia kama walivyowekwa ndani kina Manji kwa Magumashi Magumashi tu!

Kila aliehitajika kuteswa na kufilisiwa alipewa jina 'Mhujumu Uchumi au Kibaraka wa Mabwanyenye' na hapo ndo umekwisha hutapata Mtetezi ukiwa unasulubiwa

Huu ni Upande wa Pili wa Sokoine ambao haujulikani sio lazima sote tuzungumzie Mazuri yake tu!
 
Sokoine, E.M aliwahi kusemwa kama Kiongozi msimamia haki bila unafki na uoga.

Wakati anaanza harakati za kusaka wahujumu na wabadhirifu, alifika kwanza kwa rafiki yake na kumueleza adhima ambayo alipanga kuitekeleza kuanzia kesho yake asubuhi.

Rafiki yake huyo kwa kumjua vema Sokoine, usiku huo huo akawaamsha wanae na kuanza kwenda kutupa bidhaa na vitu vingine porini. Hii ni kuogopa kwamba Kesho yake, yeye angekuwa wa kwanza.

Kama alivyo-bet, asubuhi na mapema sana Sokoine alianzia kwake kupiga search na kutafuta kama alikuwa ni mmoja kati ya wahujumu Uchumi.

Pumzika kwa amani Mkuu Sokoine.
Kwa kuwakamata wahujumu uchumi nchi yetu ilifaidika na nini?
Historia itavifundisha vizazi vijavyo mambo yaliyofanyika na kurudisha nyuma uchumi wa nchi hii.RIP E. Moringe Sokoine
 
Alisemwa kuwa angekuja kuwa rais wa nchi hii, lakini wakamsema kuwa kwa sababu ni wa kanda ile janja hafai, tumtege!
 
Nakumbuka hali ilikuwa mbaya sana ya uchumi kipindi kile matajiri wengi walificha bidhaa majumbani na pesa hawakupeleka Benki na wakati ule Benki maarufu ilikuwa NBC National Bank of Commarce.

Watanzania tulinunua bidhaa kwa njia ya magendo na wenye uwezo tu ndiyo waliweza kupata na masikini waliumia sana.

Kumbuka tulikuwa Tume toka ktk vita ya Kagera,Pia lilikuwa na anguko kubwa la bei ktk soma la dunia kwa mazao toka Africa kama Pamba,mkonge,Chai,korosho,Tumbaku,n.k kwahiyo nchi ilikuwa ktk mtikisiko mkubwa kiuchumi.

Sokoine kama Waziri mkuu alichukua maamuzi magumu kutangaza vita dhidi ya uhujumu uchumi.

Sokoine hakuogopa lolote wala MTU yoyote alisimama ktk kutetea mtanzania mnyonge toka kwa mapapa walikuwa wanalihujumu Taifa.
 
Elimu Bure ni Kweli Imekwama....CCM waliiga Ilani ya CHADEMA na wamekwama (Copy and Paste).

Kila mtu mwenye mwanafunzi shule ya Msingi au Sekondari katika shule za Umma atadhibitisha hili bila shaka

Wakurugenzi wa wilaya wamewaagiza wakuu wa Shule na Kamati za Shule kuitisha michango mbali mbali

Serikali kuu imeshindwa kupeleka pesa kwenye Halmashauri...

Huduma za Jamii kWa ujumla zimekwama Tanzania.

Waalimu wana dai pesa nyingi na Serikali inapiga dana dana kwa kutumia visingizio mbali mbali

Vituo vya Afya na Hospitali za Wilaya hawana dawa kabisa. Bima ya Afya ya Taifa imekwama

Mtu anaenda Hospitali kwa Bima ya Afya, anaandikiwa kila kitu halafu anaambiwa Kanunue Dawa

Wito: watanzania tulipe Kodi kwa Moyo Zaidi....Tumsaidie Rais JPM ili tufichue wakwepa kodi...
.
 
Kwa kuwakamata wahujumu uchumi nchi yetu ilifaidika na nini?
Historia itavifundisha vizazi vijavyo mambo yaliyofanyika na kurudisha nyuma uchumi wa nchi hii.RIP E. Moringe Sokoine
Kwan uchumi wetu ulienda mbele au ukikua juu kipindi gan?
 
Back
Top Bottom