Ikiwa Afrika ina historia ya utawala wa mabavu na kutojali haki kwa raia, mfumo wa vyama vingi na chaguzi kama njia za kubadilisha utawala zinagonga mwamba.
Afrika imeshuhudia vita, mifarakano na manyanyaso ya watawala kutokubali kuachia maamuzi ya wengi katika chaguzi na vivyo hivyo kutokubali kuachia madaraka.
Nchi nyingi zimefeli Ivory coast, Guenea, Rwanda, Burundi, Kenya ni mifano ya karibuni ya nchi za Afrika kutojali demokrasia na haki za maamuzi.
Ikiwa kwa miaka ya nyuma tuna uzoefu wa watawala kutokubali kuachia madaraka kwa kuteka zoezi zima la chaguzi, kuweka sheria mbovu za chaguzi ili kujipendelea, kupinduwa matokeo, kutumia vyombo vya dola kujilinda na mengine mengi mabaya kule Zanzibar ndio wao wameleta hitimisho kabisa.
Kwamba sasa wameleta zama mpya. " Ukishindwa uchaguzi futa' hili ndio hitimisho la demokrasia kwa afrika.
Zanzibar tayari imetowa somo(lesson) kwa viongozi wa Afrika kwamba sasa wanaweza kufuata mkondo huu, na wala hawapaswi kuwa na wasiwasi.
Suali ni jee ndio ulimwengu umeruhusu hili liendelee Afrika au ndio Zanzibar imeachwa kufanya haya kwa upendeleo maalumu?
Sioni tena maana ya Demokrasia na utawala wa sheria Afrika na Zanzibar ndio mfano hai kwa sasa.
Kwangu mimi ikiwa hili litapita na dunia inyamazie(dalili za kunyamazia tayari) basi hili ndilo hitimisho la Demokrasia Afrika.