Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,743
- 2,600
Katika ripoti iliyokabidhiwa kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Seelemani Jafo Machi 18, 2025 jijini Dar es Salaam, mambo 10 yalibainika, yakiwamo ya kampuni za wawekezaji kutosjiliwa Kituo cha Uwekezaji (TIC), kamapuni za wageni kutosajiliwa wala kuea na leseni za biashara, wageni kuuza bidhaa bei za chini, wageni kumiliki mnyororo wa biashara yote na wazawa kutumia vitambulisho vyao kusajilia kampuni za wageni.
Akizungumza kabla ya kukabidhi ripoti hiyo, Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa kuchunguza suala hilo, Profesa Edda Tandi Luoga alisema baada ya kutembelea maduka 75 walibaini kuwepo kwa wageni 152 wanaofanya biashara na kati yao wageni 28 walikuwa wanafanya kazi kinyume na masharti ya vibali vyao vya ukaazi.
Katika upelelezi uliofanyika katika maghala 11 mkoani Dar es Salaam walibaini kuwepo kwa wageni watatu wanafanya kazi kinyume na vibali vyao hivyo kuleta jumla ya wageni 31 wanaonya kazi kinyume na vibali vyao.
“Kamati iliwakabidhi kwa idara ya Uhamiaji na kati yao 24 waliondolewa nchini wakati kamati ikiendelea na kazi.”
Pia kamati ilipotembelea viwanda, ilibaini kuwepo kwa wafanyakazi wa kigeni wanaofanya kazi zisizokuwa na utaalamu na ambazo zingeweza kufanywa na wazawa.
“Katika ukaguzi na uchunguzi kwa viwanda 11 kulikuwa na wageni 106 na wazawa 778 kamati ilibaini kuwa wageni wote 106 walioajiriwa walikuwa wanafanya kazi za kawaida ambazo zingepaswa kufanywa na wazawa,” alisema.
Kuhusu usajili wa kampuni, alisema walibaini kuwepo kwa kampuni 9,380 zilizosajiliwa na Wakala wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), ambapo miongoni mwake ni asilimia 9.2 ndio zilikuwa zimesajiliwa katika Kituo cha Uwekezaji (TIC).
“Hali hii inaashiria uwepo wa mianya inayoruhusu wageni kusajiliwa kampuni na kufanya biashara zinazodhaniwa kupaswa kufanywa na wazawa bila ufuatiliaji wa kutosha,” alisema.
Katika usajili pia walibaini wazawa kutumia vitambulisho vyao vya utaifa (Nida) kusajilia kampuni za wageni na hivyo kuonekana kama wamiliki wakati ni wafanyakazi tu.
Walibaini pia kuwepo kwa maduka 29 yanayofanya biashara mitandaoni yasiyo na leseni na maduka 27 yaani asilimia 93.7 hawakuwa na usajili. Pia walibaini majukwa 14 ya nbiashara ambapo 12 kati yake hawakuw ana leseni wala usajili.
Jambo lingine walilobaini ni wageni kuwaondoa wazawa katika maeneo ya biashara waliyopangisha kwa kulipa kodi kubwa, na kwa kutumia malipo ya ziada yanayojulikana kama kilemba na pia wageni kuuza bidhaa kwa bei ya chini ya soko hivyo kupunguza uwezo wa wazawa kuhimili ushindani
Walibaini pia wageni kumiliki mnyororo wote wa thamani toka mzigo unapoagizwa mpaka kufika kwa mlaji: “Wanaagiza mizigo, na kuitoa bandarini kupitia kampuni za kigeni na kusafirisha kupitia kampuni za kigeni.”
Kamati pia ilibaini kuwa wafanyabiashara wengi wa kigeni Kariakoo hawatumii benki, wanafanya malipo kwa kubadilishana bidhaa kati yao.
Kamati iliponunua bidhaa katika maduka 10 ambapo wafanyabiashara wanane hawakutoa risiti na hata hao waliotoa risiti, mmoja alitoa risiti ya kughushi.
Soma>>>>Kufurika kwa Wachina Tanzania ni fursa au janga?
Njia zilizotumika
Akieleza njia walizotumia kupata taarifa, Profesa Luoga alisema walitumia njia nane kupata taarifa na kuzichakata, ambazo ni kupitia utafiti, sheria zinazohusu na biashara na uwekezaji Tanzania na mikataba biashara huru na makubaliano ya kibiashara katika Jumuiya za Maendeleo Kusini mwa Afrika.
Alisema walikusanya taarifa kutoka kwa taasisi zinazotoa leseni, vibali vya biashara, uwekezaji na ukaazi, wafanyabiashara na kufanya uchunguzi na ukaguzi katika maeneo 110 ya biashara, soko la madini, viwanda na maghala katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Alisema pia walipata uzoefu kutoka kwa nchi nyingine za Uganda, Msumbiji, Botswana, Afrika Kusini, Burundi, Malawi, Kenya na Malaysia na kupitia sheria za biashara na uwekezaji za Zimbambwe na Lesotho.