Yaliyojiri Zanzibar ndani ya wilaya ya Micheweni usiku wa jana 26 Juni, 2016

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
YALIYOJIRI NDANI YA WILAYA YA MICHEWENI USIKU WA JANA TRH 20/06/2016.

IMG-20160621-WA0003.jpg


Majira ya saa nne usiku wa jana ktk eneo la Kinazinu jimbo la Wingwi gari mbili za polisi ambazo ndani yake walikuwemo mazombi walishuka ghafla ktk eneo hilo ambalo kwa kawaida wana Kinazini wanakuwa wanaangalia Tv na kuanza kuwafurasha watu kwa kuwapiga kwa magongo,bakora na mikia ya taa.

Katika kurukushani hiyo na kwa kuwa waliwavamia watu ghafla bila ya kujipanga walifanikiwa kuwapiga wafuasi wetu wanne ambao.

1.ALI SULEIMAN SAID MIAKA 27Huyu kiasi fulani hadi nakutana nae hajaumia sana na yuko vizuri afya yake na hana sehemu alioathirika.

2.FATMA JUMA HAMAD MIAKA 25,Wakati nafanya mahojiano nae alinielezea kuwa amepigwa na ameumia sehemu ya uso kama ambavyo picha yake inavyoonekana.

Aidha amesema pia alipata kipigo kilichomuathiri ktk maeneo ya maziwa.

3.ALI OMAR HASSAN MIAKA 52,Huyu Ustadh alipata kipigo katika eneo la mkono na kifuani,Alipatwa na mkasa huo akiwa safarini kurejea Kiungoni kuja kwake Kinazini ambapo njiani alikutana na wahuni hawa wakamshambulia kwa magongo na mikia ya taa.

4.HAMAD ABDALLA ALI,MIAKA 48 Huyu ni katibu wa Tawi la Kinazini naye alipata kipigo cha mikia ya taa ktk maeneo ya mikono lakini yuko vizuri ule uvimbe umeondoka,ENEO LA MIANZINI Katika eneo hili pia walipita ktk duka la BARAKA ALI majira ya saa nne na dakika arobaini.

Mizingani Hapa kwa kawaida ya wana Mianzini pia ni eneo lao la kawaida ambalo nao wanaangalia TV, waliwavamia watu na wakakimbia mbio wakabakia watu wawili ambao mmoja ni mmiliki wa duka lenyewe na OTHMAN HEMED ABDALLA MIAKA 30.

Kiujumla watu wote walikimbia akabaki mwenye duka na mwenzake OTHMAN.Mwenye duka hajaguswa hata upele huyu ni askari mstaafu na hasira zao zote wakazielekeza kwa bwana OTHMAN wakampiga marungu matano,manne mgongoni na moja la kichwani.

Kwa mujibu wa maelezo yake marungu manne yote aliyopigwa ya mgongo bado alikuwa anafahamu zake lakini hili moja la tano walimpiga kichwani na kupelekea kupoteza fahamu kabisa.

IMG-20160621-WA0002.jpg


IMG-20160621-WA0001.jpg

Huyu ni mgonjwa wa sukari na pressure hali yake ni dhaifu sana ndio mana alishindwa kukimbia.Picha nimeiambatanisha.

Baada ya kumaliza kipogo hapo ndio walielekea ktk kijiji cha Kiungoni kama ambavyo mabomu yalivyosikika.

Hilo la Kiungoni litaelezwa na wadau wa wilaya husika.

Baada ya kumaliza mahojiano nao nimetoa maelekezo kuwa wale wote ambao hali zao sio nzuri waende hospitali na waanzie polisi kuchukua Pf3.

Wakati naandika taarifa hii nikiwa ktk mahakama ya konde nimepokea taarifa kuwa tayari wameshafikishwa kituoni wote kwa pamoja kwa gari ya wagonjwa ya jimbo na tayari wameshapata PF 3 na nimewaelekeza wazitoe kopi kwani wanaweza kuwapokonya
 
Daa poleni but nini kimepelekea kichapo hicho kutokea na kuumizwa wana hao wa Tanzania ?
 
Hawa watu kwenye picha wanaonekana hawana izo sehemu za kupiga. Poleni sana Tuipendeni nchi yetu tuwe makini na amani iliyopo.
 
Me sishangai mabo kama haya kutokea maana siasa ndio zimetufikisha hapa... Wanasiasa wana imani zao msiseme ni Mipango ya Mungu
 
Back
Top Bottom