Yaliyojiri: Uchaguzi wa Marudio visiwani Zanzibar - Machi 20, 2016

Zikiwa zimesalia dakika chache kuanza kwa zoezi la kupiga kura,muitikio wa wapiga kura bado unaonekana kusuakusua ingawaje sababu bado hazijafahamika kwa mfano katika kituo cha Madungu Chakechake Pemba BBC wameripoti kuwa hadi sasa hivi hakuna mpiga kura aliyefika na kituoni wapo Maafisa wa tume na Maafisa usalama tu.
ImageUploadedByJamiiForums1458446388.369005.jpg
 

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,227
5,270
Fuatilia yanayojiri katika Uchaguzi wa Marudio visiwani Zanzibar hapa.

=> Rais anayetetea nafasi yake, Dkt. Mohamed Shein amepiga kura katika kituo cha Bungi kisiwani Unguja

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed alizungumza na wanahabari baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera kisiwani Unguja ambapo alisema anaamini atashinda kwa kishindo na kuhusu kushindwa alisema tusubiri matokeo ya uchaguzi ndiyo yataamua.

"Nimepata nafasi ya kupiga kura kama haki yangu ya kimsingi na kumekuwa na utulivu mkubwa kwenye zoezi hili,hali ya ulinzi imeimarishwa.

"Matumaini yangu ni kushinda kwa kishindo, kuhusu kushindwa ndugu muandishi tusubiri matokeo ndiyo yataamua".Alisema Dkt. Ali Mohammed Shein

IMG-20160320-WA0015.jpg

IMG-20160320-WA0021.jpg

IMG-20160320-WA0029.jpg


=> Wazanzibari kadhaa wamejitokeza kupiga kura:
Cd9xGoPW8AAvyjK.jpg

Cd9stX-UkAUaSJY.jpg


* Uzi huu ni wa Moja kwa Moja(LIVE) hivyo unaweza kuona post zikitokea moja kwa moja ukiwa kwenye uzi huu.

Matukio mengine ya kukumbukwa leo katika Tanzania:

March 20, 1980: Rais Julius Nyerere awasili Serengeti akiwa njiani kwenda kwenye mapumziko mafupi Butiama

March 20, 1990: Halmashauri Kuu ya CCM yampongeza Rais Ali Hassan Mwinyi kwa kuvunja Baraza lote la mawaziri na kuliunda upya

March 20, 1992: Halmashauri Kuu ya CCM yaazimia kwamba askari wote (armed forces) wasiendelee kwa wanachama wa CCM

March 20, 2006: Ali Muhsin, mmoja wa mawaziri wa kwanza wa Zanzibar huru anafariki

March 20, 2015: Rais Jakaya Kikwete kwa mamlaka aliyopewa na katiba anawateua wabunge wawili (Dr. Grace Khwaya Puja and Innocent Sebba
 
Leo tutashuhudia vibweka vingi vinginevyoni hivi wapiga kura Zanzibar yote wanaweza hata elf 2 wasifike ila Jecha atasema waliojitokeza laki 3

Ukiona had saa 6 vituo havina watu alafu kuanzia saa 8 vijana wanaanza kujitokeza ujue wamenunuliwa ili kuondoa aibu

HII SINEMA YA LEO NI KALI KULIKO ZOTE ZILIZOTOKEAGA NGOJA NIKAE HAPAHAPA NISIPITWE NA KITU hyo ndio CCM leo ndio inaonesha ile rangi yake halisi ya NYOKA WA KIJANI
 
Naangalia uchaguzi huu kwa jicho la tatu. Utaonyesha kiasi halisi cha kura ambazo ccm huwa wanapata. Hii itasaidia kujua kura za cuf.
Ha ha ha mkuu unamanisha ata Lowassa angesusa uchaguzi mkuu na Magu akapata zile Milion 8 basi ungesema kuwa watanzania waliokajiandikisha walikuwa milion 22 bas zilizobaki milion 10+ zingekuwa za Lowassa au…??
 
Back
Top Bottom