Yaliyojiri: Mkutano wa Wanahabari na Spika wa Bunge, Job Ndugai

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,281
Waandishi wa habari tuko uwanja wa ndege wa Julius Nyerere terminal 1 wakimsubiri Spika wa Bunge.

Camera zetu pia zipo tayari...

View attachment 487054
Waandishi tunaendelea kusubiri baada ya saa nzima kupita tokea mkutano wa Spika Mh Job Ndugai kutakiwa kuanza uwanja wa ndege

tmp_15386-IMG_20170326_100301-924140143.jpg


==========

UPDATES
Mpaka huu 10.14 bado Spika Job Ndugai hajafika.
Mkuu wa kitengo cha habari - Bunge Owen Mwamdumbya ametaarifu wanahabari kuwa Spika amefika tayari kwa mahojiano

View attachment 487060

Waandishi tumeshatoka Uwanja wa Ndege tunenda kwenye ziara maalum kwa ajili ya kufanya mahojiano na Spika wa Bunge Mhe Ndugai

tmp_25460-IMG_20170326_105418638228224.jpg

Waandishi wa habri tumefikishwa bandarini ofisi za Mamlaka ya Bandari muda huu kwa ajili ya mahojiano na Spika wa Bunge Mh Job Ndugai

tmp_25460-IMG_20170326_110018610656140.jpg

Spika Ndugai akiwa na wabunge 10,amefuatana na waandishi hadi Bandari ya Dar,
Waandishi tunamsubiri Spika wa Bunge Mh Ndugai ambaye kwa muda huu ana mazungumzo ya ndani na viongozi wa Mamlaka ya Bandari

tmp_25460-IMG_20170326_111054-975790073.jpg

Waandishi wa habari tumeshangaa sana tuliambiwa mahojiano yanafanyika airport, tunapelekwa bandarini.

Spika Job Ndugai yuko bandarini kupata maelezo zaidi kuhusu kontena zilizokamatwa zenye mchanga kutoka migodini
Spika Job Ndugai na wabunge wa kamati ya nishati wanafanya ziara Bandari kuu kukagua kontena zilizokamatwa zenye mchanga .
tmp_25460-IMG_20170326_113202-212324108.jpg

Spika Job Ndugai akipokea maelezo kutoka kwa watendaji wa bandari kwenye kontena zilizozuiliwa.
View attachment 487088
tmp_25460-IMG_20170326_114959-1562983560.jpg

Spika Ndugai anapokea maelezo kutoka uongozi wa bandari kuhusu kontena zilizozuiliwa na sasa anatembelea kontena hizo



==>>Spika Ndugai: Ndugu waandishi mnavyoona hadi Spika nimekuja hapa, jua kuna sintofahamu nyingi.
==>>Spika Ndugai: Baada ya kuona suala hili la makontena nikaona nije ili kujua ukweli. Hili si jambo dogo.Tutaona jinsi gani kuishauri Serikali
==>>Spika Ndugai: Namshukuru Rais Magufuli kuja huku bandarini na ya kuyang'amua makontena 20 ya mchanga.
==>>Spika Ndugai: Tutapenda kujua biashara ya madini kama taifa tunafaidikaje?
==>>Spika Ndugai: Kama Bunge, tutaunda timu ya kuja kutathimini biashara hii ya mchanga na madini kwa ujumla.
==>>Spika Ndugai: Timu hii pia itaangazia hatua za awali toka uchimbaji wa madini hapa nchini hadi huko nje tunapoenda kuyauza.
tmp_25065-IMG_20170326_125233104927810.jpg

Baada ya kutembelea bandarini, Spika Ndugai kapanda gari na kuelekea Hoteli ya Serena.
View attachment 487114
Katika siku ambazo waandishi wa habari tumechezewa akili tukio la leo. Tulichoambiwa na ambacho tumeenda kufanya vitu viwili tofauti kabisa. ......

IMG_20170326_184835.jpg
IMG_20170326_184839.jpg
 
Kumbe huu mkutano ni wa kweli. I was wondering kwann jamaa anafanyia airport, je anafanya baada ya kutua nchini au anafanya mkutano then anasepa?? Time will tell. Eeh Mungu wa Wote, Mungu wa Kina Bashite na cc raia wa kawaida saidia spika huyu acfanyiwe Kinanalization na mkutano uendelee, spika huyu actumwe India kutibiwa kwa cku 12.
 
Heshima kwenu Wakuu,

Kwa taarifa zilizotolewa jana, ni kwamba Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Job Ndugai, ataongea na Wanahabari katika viunga vya Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.

Ntajitahidi Kuwaletea kile atakachozungumza.

Karibuni.

=======

UPDATES;

1005hrs: Bado anasubiriwa Mheshimiwa kufika, bado hajafika. Waandishi wanaendelea kusubiri baada ya saa nzima kupita tokea mkutano wa Spika Mh Job Ndugai kutakiwa kuanza uwanja wa ndege.
C703lBSXwAIYvaz (1).jpg

Waandishi wa habari wako uwanja wa ndege wa Julius Nyerere terminal One wakimsubiri Spika wa Bunge.

1030hrs: Mkuu wa kitengo cha habari - Bunge Owen Mwamdumbya ametaarifu wanahabari kuwa Spika amefika tayari kwa mahojiano
 
Back
Top Bottom