Yaliyojiri leo Bungeni kipindi cha maswali na majibu, 20.03.2016

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
BUNGE LINAENDELEA LEO 20.03.2016, MASWALI NA MAJIBU

Swali: Mbunge Jackson Rweikiza swali kuhusu ujenzi wa chuo cha VETA Bukoba

Majibu
: Serikali inaendelea kuandaa michoro ya majengo, barabara, maji na umeme na mitaala ya kufundishia, pia serikali inaendelea kuongea na wafadhiri ili wachangie juhudi za serikali

Swali la nyongeza: Ni lini chuo kitaanza kujengwa na swali la pili je kiasi gani kimetengwa kwenye bajeti kwaajili ya ujenzi wa chuo cha VETA Bukoba.

Majibu: Ujenzi wa chuo unaanza baaba ya kupitia hatua mbalimbali na baada ya kumaliza hatua hizo ndipo serikali itasema lini itaanza kujenga. Naibu anaomba mbunge awaamini.

Swali: Serikali imepangaje kiwango cha gharama kwa kila mwanafunzi kwa shule za bweni na za kutwa ni kiasi gani, na kiwango hicho hakitasababisha kuporomoka kwa ubora wa elimu.

Jibu: Serikali imeanza zoezi la kupanga shule Binafsi za sekondari na msingi kwa makundi ili kuweka viwango vya ada kwa kuzingatia ubora wa huduma na hivyo kutoathiri kiwango cha elimu inayotolewa.

Wizara inatarajia kuwa utaratibu wa ada elekeze hautaathiri ubora wa elimu katika shule binafsi kwa sababu ada hiyo itapangwa kulingana ba ubora wa huduma na miundombinu iliyopo shuleni.

Aidha amesema Serikali imefanya utafiti kuhusu gharama za kusomesha mwanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari ambapo kupitia utafiti huo imebaini kuwa ada zinazotozwa katika shule binafisi zinatofautiana kwa kiasi kikubwa kulingana na huduma zinazotolewa,aina ya shule na miundombinu iliyopo.

Swali:
Serikali imejipangaje kuwasaidia wavuvi wadogo?

Majibu:
Kuna mradi ulioko bara na visiwani na serikali imeanzisha benki ya kilimo ili kuwawezesha wavuvi. Wawakilishi wa wavuvi 99 wamepatiwa mafunzo ili wafundishe wenzao.

Swali la nyongeza: Ni lini mafunzo yatafika jimbo la Kojani?
Majibu: Katika bajeti inayokuja ndipo serikali itasema lini mradi utafika

Swali: Ni lini serikali itakuja na bei elekezi ya maziwa kwa lita?
Majibu: Ni kweli bei iko juu, lakini bei elekezi inaamuliwa na kanuni za soko hivyo ni vigumu kuweka bei elekezi lakini serikali itajitahidi kujenga viwanda

WIZARA YA MAMBO YA NDANI:

Swali: Je serikali inamkakati gani kuzuia mauji ya vikongwe?
Majibu: Serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusaka waganga wa jadi wanaopiga lamri chonganishi.

Swali: Je tutawasaidiaje vikongwe kwa kuwapelekea gesi ili wasipikie kuni ili macho yao yasiwe na rangi nyekundu. Serikali inawachukulia hatua gani wauaji?
Majibu: Kuna mikakati mbalimbali inachukuliwa ili kupunguza matumizi ya kuni na kinyesi cha ng'ombe kupitia nishati mbadala. Pia serikali imechukua hatua kwa takwimu za Julai mwaka jana mpaka Machi kuna kesi zinaendelea mahakamani.

WIZARA YA VIWANDA:


Swali: Je sera ya viwanda imesimamiwa vipi
Majibu: Ili kuchochea maendeleo ya viwanda serikali imeandaa mkakakati wa kuimarisha utekelezaji wa sera hiyo ili kukuza uchumi na kuongeza ajira.

Swali: Je waziri anaahidi nini kwa mkoa wa Lindi kwa mpango huu wa viwanda?
Majibu: Bajeti inakuja na mambo mazuri ikiwa ni pamoja na kukuza zao la Mhogo.

WIZARA YA MAJI:

Swali: Lini serikali itakuza mradi wa maji Masasi?
Majibu: Mradi wa maji safi Masasi na Nachingwea unakusudiwa kuendelea kufanyiwa upanuzi ili kufikisha huduma kwa vijiji vingi zaidi. Kwasasa mkandarasi anaendelea na ujenzi wa miundombinu

Swali: Serkali katika bajeti billion 1 iliyopita pesa zilitengwa na hazijafika je zitafika lini halmashauri ya Masasi?
Majibu: Makusanyo hayakuwa mazuri hivyo pesa haikupelekwa na sasa kwasababu makusanyo ni mazuri pesa itapelekwa kwa uhakika. Pia amependekeza mamlaka ya MWANAWASA itapanga bei nzuri ya kuunganisha maji

Swali: Richard Ndassa Serikali ni lini mradi wa maji Sumve utaanza?
Majibu: Ni kweli serikali iliahidi kupeleka maji Sumve na kupitia bajeti serikali itasema ni lini.

========================
Ratiba inayofuata ni matangazo kutoka ofisi ya Spika kisha Waziri wa Fedha atawasilisha mpango wa maendeleo wa miaka 5.
 
SWALI LA NYONGEZA:
Ni ipi kauli ya serikali kuhusiana na sakata la LUGUMI?
Sidhani kama hilo swali litakosekana
 
Si hawataki tujue kinachoendelea huko bungeni,haya maswali majibu ambayo ni akama michezo tu ya watoto nani ana mpango nayo!Wakwende zao huko.Walishatuona sisi ni mazombi,tunapangiwa ni nini cha kusikia na nini cha kutazama.
 
haya ni yale mambo ya baby cow,"if a father cow have 4 legs how many legs do baby cow have" wakae wenyewe na mihezo yao ya kombolela hiyo.
 
Back
Top Bottom