Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,535
Kufuatia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukataa kuwa si kweli rais Magufuli amepanga kuufuta upinzani nchini ifikapo mwaka 2020.
Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Aikaeli Mbowe alimuuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kama atakuwa tayari kuwajibika endapo kambi hiyo italeta uthibitisho ndani ya Bunge kuwa Rais na Serikali ya awamu ya 5 imepanga kuufuta Upinzani nchini ifakapo mwaka 2020.
Aidha Naibu Spika Dkt Tulia Akson Mwansasu alilikataa swali hilo kwakuwa sio swali la kisera hali iliyosababisha kambi rasmi ya upinzani kupiga mayowe kuonyesha kutokuunga mkono maelezo hayo ya Naibu Spika.
=======
Swali:
Kwa kuwa mwaka jana kulikuwa na upungufu wa sukari, napenda kuipongeza serikali kwa kushughulikia suala hili.
Serikali imejipanga vipi kuzuia hali ile isijirudie mwaka huu?
Waziri Mkuu:
Naahidi hakutatokea upungufu wa sukari. Tuna viwanda vitano na vinatosheleza mahitaji nchini. 86% ya kiasi cha malengo ya uzalishaji kimeshazalishwa hadi kufikia mwezi Januari.
Serikali imekaa mara nyingi na wazalishaji wa sukari kujadili njia ya kuboresha uzalishaji wao.
Swali:
Serikali ina mpango gani wa haraka wa kuleta chakula ili kudhibiti mfumuko wa bei uliopo sasa.
Waziri Mkuu:
Serikali inaendelea kuhamasisha wazalishaji wa ndani kwenye maeneo yenye chakula cha ziada ili waweze kwenda kusambaza chakula kwenye maeneo yenye upungufu.
Swali la nyongeza:
Kuna kaya kama 3000 ambazo hazina uwezo wa kununua chakula, je serikali ina mpango gani na hawa?
Waziri Mkuu:
Suala la uwezo ni jambo pana. Kila kaya inatakiwa ijiongezee kipato na si kusubiri serikali ipeleke pesa. Nawasihi wafanyabiashara wasipandishe bei ili wale wa kipato cha chini waweze kumudu.
Swali:
Katika bajeti ya 2016/17 mfuko wa walemavu haukutengewa fedha zozote na kupelekea baraza la watu wenye ulemavu kutofanya kazi yake ipasavyo, je serikali inasema nini kuhusu jambo hili?
Naibu Waziri:
Katika bajeti ya 2017/18 tunatarajia kutenga fedha kwa ajili ya mfuko huu na tumeshaanza kuandaa mapendekezo ya hili.
Swali:
Serikali ina mpango gani katika kukabili athari za matetemeko ya ardhi nchini?
Naibu Waziri Anthnony Mavunde:
Serikali imejipanga kutoa elimu kupitia kwa baraza la jiolojia kwa wananchi ili kuwasaidia kupunguza athari za majanga haya.
Serikali imetunga sheria mpya ya menejimenti ya maafa ambayo inaelekeza kuundwa kwa kamati za maafa katika wilaya.
Tathmini ya maeneo yenye viashiria vya kupatwa na maafa imeshafanywa nchi nzima.
Swali la nyongeza:
Utayari wa serikali uko vipi ili kukabiliana na majanga kama tetemeko?
Serikali ina vifaa vya kuweza kupima athari au hata kutabiri maafa?
Jibu:
Sheria imeundwa mahsusi kwa ajili ya suala hili na kamati za maafa zinazoundwa kutokana na sheria hii zitasaidia watu kuwa tayari muda wote.
Masuala ya matetemeko yanasimamiwa na Wakala wa Jiolojia. Hadi sasa tuna vituo kadhaa vyenye vifaa vya kutosha kupima.
Swali kutoka kwa Mbunge wa Bukoba Mjini:
Je Miongozo hiyo ya sheria inawasaidia vipi wananchi wa Kagera town walio katika hali mbaya hadi sana kwa sababu ya tetemeko?
Jibu kutoka kwa A. Mavunde:
Kwa case ya Bukoba, michango iliyotolewa na taasisi mbalimbali ikiwemo Bunge, haikusemwa itafanya nini bali ilisemwa tu kuwa ni kwa ajili ya wahanga. Serikali imeamua kujenga taasisi za serikali ili kuwafikia walengwa katika huduma za hospitali na shule.
Swali:
Kumekuwa kukitolewa taarifa ya kuanza uchimbaji katika migodi ya Liganga na Mchuchuma, lini kazi hii itaanza?
Jibu: N/W viwanda.
Upembuzi yakinifu umeonesha Liganga inaweza kutoa tani mil2.9 za chuma kwa mwaka na mchuchuma inaweza kutoa tani mil 3 za makaa ya mawe kwa mwaka.
Kwa sasa taratibu za kulipa fidia zinaendelea kwa wananchi wa maeneo jirani na migodi hiyo kabla uchimbaji haujaanza.
Swali la nyongeza:
Serikali ina mkakati gani kuwasaidia wananchi wa njombe ambao ni wakulima waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora wa kuuzwa mgodini?
Jibu:
Serikali imeitaka kampuni kutoa elimu na mikopo kwa wananchi ili waweze kunufaika na kushiriki katika shughuli za kibiashara katika maeneo hayo. Vijiji kadhaa vimepewa elimu ya ulimaji mbogamboga na ufugaji.
Swali:
Serikali ilisema mwezi aprili fidia italipwa juni 2016 na uchimbaji kuanza machi 2017, kwanini hivi sasa serikali inatoa majibu yasiyo na matumaini?
Jibu:
Fidia ni kubwa sana hivyo serikali bado inajipanga kukamilisha. Kuhusu kuanza kwa uchimbaji, mwezi machi bado haujafika hivyo taratibu zikikamilika unaweza kuanza muda huo.
Swali:
Upo ushahidi wa kukosewa kwa lugha ya Kiswahili kwa Wabunge na Viongozi wa Serikali. Je Wizara inalichukuliaje hili, kabla ya kuanzisha Sera ya lugha?
Pia Sera ya lugha itakuja lini?
Jibu:
Serikali iko tayari kupitia BAKITA kutoa semina bungeni kwa viongozi wote ili watumie lugha kwa ufasaha.
Wizara bado inakusanya maoni ya wadau kuhusu Sera ya Lugha.
Swali la nyongeza:
Baadhi ya nyimbo huwa zinadhalilisha wanawake kwenye luninga. Je Serikali inalichukulia vipi suala hili?
Jibu:
Tuna vyombo vinavyopitia maudhui ya filamu au nyimbo.
======
Dodoma, Alhamisi, 2 Februari, 2017: Serikali imetoa ufafanzi kuhusu masuala mbalimbali kuhusu utawala wa Sheria na kuainisha mikakati yake katika kuzuia au kupunguza athari za matetemeko ya ardhi nchini. Ufafanuzi huo umetolewa mjini hapa leo.
Serikali Kutoingilia Mihimili ya Dola
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesisitiza kuwa Serikali inaheshimu mgawanyo wa mihimili mitatu ya dola nchini. Waziri Mkuu alikuwa akifafanua kuhusu malalamiko kuwa baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa kesi zao zinachukua muda mrefu.
Aidha, Waziri Mkuu amekanusha vikali madai kuwa Serikali inakusudia au imetangaza kufuta vyama vya siasa hasa vya upinzani nchini madai yaliyotolewa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe.
Mkakati Kuzuia Majanga Ya Asili
Akijibu hoja kuhusu mikakati ya kupambana na athari za majanga ya asili, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Anthony Mavunde, amesema Serikali tayari inao mkakati wa kitaifa wa kupambana na majanga ya asili yakiwemo matetemeko.
Aidha, Serikali imeandaa Sera ya Taifa ya Menejimenti ya Maafa ambayo imeainisha aina mbalimbali za maafa ikiwemo tetemeko la ardhi pamoja na majukumu ya kila mdau katika kushughulikia maafa. Aliongeza kuwa, Serikali pia imeandaa Mwongozo wa Taifa wa Kukabiliana na Maafa ambao unaelekeza Taasisi kiongozi na wajibu wao wakati wa kukabiliana na majanga.
Liganga, Mchuchuma Kuzalisha Megawati 350
Serikali imesema kuwa, miradi unganishi ya Mchuchuma na Liganga itakayotekelezwa kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Group (SHG) Limited ya China kupitia ubia wa pamoja wa Tanzania China International Mineral Resources Limited (TCIMRL) itazalisha zaidi ya ajira 33,000 na kuipatia nchi umeme wa megawati 350.
Akitoa ufafanuzi huo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa kampuni hiyo imeshapewa leseni na vibali vingine muhimu na sasa inakamilisha ulipaji wa fidia ili kuanza kazi. “Miradi hiyo unganishi itawezesha kuchimbwa makaa ya mawe kiasi cha tani milioni (3) na chuma ghafi tani milioni 2.9 kwa mwaka,” alisema.
Usalama wa Raia Mipakani
Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo ya mipaka inachukua hatua za pamoja na vyombo vya nchi jirani kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao katika maeneo hayo.
Akijibu hoja kuhusu suala la usalama wa raia wanaoishi pembezoni mwa mipaka ya Tanzania, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amefafanua kuwa operesheni za pamoja zinafanyika katika mipaka ya nchi na vikao vya ujirani mwema ili kuhakikisha usalama. Wananchi wameombwa kutoa taarifa wanapowaona wageni wasioeleweka katika maeneo yao ili kuimarisha usalama.
Wanahabari Waendeleze Kiswahili
Serikali imewapa changamoto wanahabari nchini kuwa chachu ya kuendeleza lugha ya Kiswahili. Wakijibu maswali mbalimbali ya wabunge kuhusu matumizi ya Kiswahili fasaha katika vyombo vya habari, Waziri na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, wameliambia Bunge kuwa, ni vyema sasa hata wamiliki wa vyombo vya habari wakaanza kuzingatia ufaulu kwa somo la Kiswahili kabla ya kuwaajiri waandishi.
Kwa upande wake Waziri Nape akitoa majibu ya nyongeza, alisema kuenziwa kwa Kiswahili nchini kumeipa Tanzania hadhi ya kuwa makao makuu ya taasisi mbalimbali za Afrika zinazojihusisha na maendeleo ya lugha ya Kiswahili.
Imetolewa na:
Idara ya Habari-MAELEZO.