Bunge la 11, mkutano wa 3, kikao cha 16
Maswali na majibu
Maswali na majibu
Swali: Serikali iliahidi milioni 50 kwa kila kijiji, ni lini fedha hizo zitatolewa?
Majibu: Serikali imetenga shilingi bilioni 59.5 kwa ajili ya wananchi wa vijijini na zitagawanywa milioni 50 kwa kila kijiji punde tuu baada ya kuidhinishwa na bunge.
Swali: Nini kauli ya serikali kuhusu kulipa fedha za uhamisho na kujikimu watumishi waliohamishiwa wa Halmashauri ya Mbogwe?
Majibu: Baadhi yao wameshalipwa, Ofisi ya rais TAMISEMI inafuatilia suala hili ili kuhakikisha watumishi 65 waliosalia wananalipwa.
Serikali inajipanga kuhakikisha madai ya watumishi inayoanzishwa yanalipwa.
Swali: Serikali ina mpango gani wa kuipandisha hadhi zahanati ya Tabata A kuwa kituo cha Afya katika jimbo la Segerea?
Majibu: Zahanati haina eneo la kutosha kupandishwa hadhi, H/shauri ya Ilala imetenga milioni 75 kwa ajili ya kuongeza majengo ikiwa ni maandalizi ya kuipandisha hadhi.
Swali: Serikali imejipangaje kutatua tatizo la maji katika jimbo la Kibiti?
Majibu: Serikali ilitenga shilingi milioni 403 ambapo tayari shilingi milioni 271 tayari zimepokelewa. Katika bajeti ya mwaka 2016/17 halmashauri imetenga shilingi milioni 83.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji kwenye vijiji vya jimbo hilo
Swali: Ni lini barabara ya Mkomazi hadi Same mjini itajengwa kwa kiwango cha lami?
Majibu: Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kutekeleza ujenzi, aidha tayari serikali imeshajenga km 19. Serikali imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwenye sehemu iliyobaki ya km 96.
Swali: Ni lini barabara ya Hulue hadi Iwonjo itapandishwa hadhi na kuanza kumilikiwa na TANROADS?
Majibu: Mchakato huo upitie ofisi ya mkoa wa Dodoma kabla ya kufika wizarani.
Serikali pia inapanga kujenga barabara ya Mbande hadi Kibakwe kwa kiwango cha lami.
Swali: Serikali ina mpango gani wa kutatua tatzo la makazi ya Polisi nchini?
Majibu: Serikali imechukua mkopo wa riba nafuu na tayari imejenga nyumba 360 Dar, Unguja na Pemba. Serikali ina mpango wa kujenga nyumba 4136 kwa ajili ya makazi ya Polisi.
Swali: Je serikali ina mpango gani wa kuondoa unyanyasaji wa wavuvi unaofanywa na JWTZ?
Majibu: Serikali haijawahi kupokea tuhuma zozote juu ya swala hilo. Aidha askari wa JWTZ wanatakiwa kuheshimu sheria za jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Swali: Je serikali itatenga lini maeno ya kilimo katika vijiji vinavyopakana na mbuga ya Serengeti?
Majibu: Serikali imeshachukua hatua ya kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Serikali pia inachukua hatua za haraka punde wanyama wanapoingia katika makazi ya watu, Na wakati mwingine ikibidi serikali inatoa kifuta machozi.
Serikali inashughullikia migogoro yote kati ya wakulima na wafugaji.
Swali: ZFA kujiunga na shirikisho la FIFA, nini hoja ya serikali?
Majibu: FIFA iliwaandikia barua ZFA kuwafaamisha kuwa haiwezekani kuitambua ZFA kama shirikisho kamili.