Yaliyojiri Bungeni Dodoma leo Januari 31 2017, Kilango, Bulembo, Palamagamba waapa

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Yanayojiri Bungeni Dodoma Leo mkutano wa sita Januari 31,2017


Mkutano wa Sita wa Bunge unaanza Jumanne Januari 31, 2017 na kumalizika Februari 10, 2017 Mjini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo utaanza na kauli ya serikali kuhusu hali ya chakula pamoja na deni la taifa na hali ya uchumi nchini.


View attachment 465601
Ukumbi wa BungeMkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea Taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge ambapo Kamati 14 za kisekta na mtambuka zitawasilisha taarifa zake Bungeni katika kipindi hiki.


Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:- KIAPO CHA UAMINIFUKufuatia uteuzi wa wabunge watatu walioteuliwa na Mhe. Rais Dk. John PombeMagufuli hivi karibuni na Uchaguzi Mdogo uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Zanzibar Tarehe 22 Januari 2017, kutakuwana Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wapya wanne ambao ni:- Mhe. Alhaji Abdallah Majula BulemboMhe. Prof. Palamagamba John KabudiMhe. Anne Kilango MalecelaMhe. Ali Juma Ali - (Jimbo la Dimani)MASWALIKatika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwapapo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi.


KAULI ZA MAWAZIRI

Aidha, katika Mkutano huu wa Bunge Kauli mbili za Mawaziri zitawasilishwa kama ifuatavyo:-Kauli ya Serikali Kuhusu Hali ya Chakula Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.

Kauli ya Serikali kuhusu Deni la Taifa na Hali ya Uchumi Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.MISWADA YA SHERIAKatika mkutano huu, miswada ifuatayo itajadiliwa...Muswada wa Sheria ya Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa mwaka, 2016 (The Medical, Dential and Allied Health Professionals Bill2016).


Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na.4) wa mwaka 2016. {The Written Laws (Miscellaneous Amendments)}, Bill, 2016)

========

Bunge linaanza leo tukitegemea wabunge wapya kuapishwa.

Naona wabunge wameanza kuitwa kwa ajili ya shughuli ya kuapishwa.

Mbunge mteule wa Dimani ameapa kutumikia wananchi

Ameapa Anne Kilango Malecela

Abdallah Bulembo amefuatia kuapa

Professa Palamagamba Kabudi ameapa pia


Maswali na Majibu

Swali:
Serikali ina mpango gani wa kuboresha maslahi ya walimu hasa vijijini?

Majibu: Serikali inaendelea kujenga nyumba za walimu, katika mwaka 2017/18 serikali inatarajia kujenga nyumba 1818, serikali imelipa madeni yenye thamani ya shilingi bilioni 20.1. Bado walimu wanadai madeni ya shilingi bilioni 26.04 ambayo tayari yamehakikiwa. Serikali inajipanga kulipa deni hilo.

Swali: Ni lini serikali itavipa hadhi vituo vya afya Mirerani na Oleklesh na ni lini serikali italeta gari ya wagonjwa.
Jibu: Maombi ya kupandisha hadhi kituo cha Oleklesh tayari yamefika wizara ya afya. Halmashauri imetenga gari moja la wagonjwa kwa ajili ya kuhudumia zahanati mbalimbali za halmashauri hiyo.

Swali: Ni mkakati gani ambao serikali inaweka kuzia tatizo la ulawiti na ubakaji.

Jibu: Sheria inaelekeza kwa mtu anayepatikana na kosa la ubakaji au ulawiti kuhukumiwa miaka 14 jela ila iwe fundisho kwa wengine.

Serikali imeanzisha dawati la jinsia kila wilaya ili kushughulikia matatizo hayo. Mahakama zimekuwa zinashughulikia kesi hizi kwa haraka punde ushahidi wa kuridhisha unapopatikana.

Swali: Ni lini serikali itaingilia kutatua mgogoro katika vijiji vya mpanda vijijini?

Majibu: Wizara itaharakisha kutoa ushauri wa kitaalam na kwa kushirikiana na halmashauri ya Mpanda itaanzisha WMA

Swali: Serikali ina mpango gani wa kushusha bei ya maji ktk halmashauri ya Shinyanga?

Majibu: Bei zimepandishwa baada ya kupata kibali kutoka mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA). Serikali ina mapango wa kupunguza gharama ya maji hasa itakapoanza kutumia nishati ya umeme na jua.

Swali la Nyongeza: Ni lini serikali itaondoa 'service charge' kwenye bili za maji?
Majibu: Tayari imeanza kwa kufunga mita za luku, punde zoezi hilo likikamilika, swala hilo la service charge litakwisha.

Swali: Ni kwanini nguzo za umeme zisilipiwe na serikali ili kurahisisha wananchi kupata umeme?

Majibu: Wananchi hugharamia nguzo za umeme kwa hiyari yao ili kuharakisha uunganishwaji wa umeme sehemu ambazo TANESCO hawajasogeza miundombinu hiyo.

Swali: Ni lini serikali itajenga kiwanda cha tumbaku na kusindika asali Tabora?

Majibu: Serikali imefanya na wawekezaji nchini Vietnam na China ili kuwekeza katika viwanda vya Tumbaku. Kituo cha uwekezaji TIC kinatakiwa kunadi fursa zilizopo katika uwekezaji ktk mkoa huu.

Chama cha ushirika mkoa wa Tabora wapo kwenye mchakato wa kuanzisha kiwanda cha kuongeza thamani ya tumbaku.
Wananchi wanahimizwa kuanzisha viwanda vidogo kwa ajili ya kusindika asali.

Serikali Imeahidi kuimarisha kazi ya upelelezi na uendeshaji wa mashtaka kwa lengo la kujenga kesi na kuwa na ushahidi wa kutosha na usiotia shaka ili kuiwezesha Mahakama kufikia maamuzi ya kuwatia hatiani watuhumiwa wa vitendo vya ubakaji.

Habari zaidi...

Akijibu swali la mbunge wa Viti maalum Rita Kabati, aliyeuliza nini mkakati wa serikali wa serikali kunusuru watoto wasiendelee kufanyiwa matendo ubakaji na ualawiti, na utaratibu gani unatumika kushughulikia watuhumiwa wa kesi hizo.

Waziri wa Katiba na Sheria mhe. DKT HARRISON MWAKYEMBE amesema serikali serikali imeanzisha madawati ya Jinsia katika vituo mbalimbali vya polisi yanayopokea taarifa mbalimbali toka kwa wananchi ili kuwezesha jeshi la polisi kuendelea na hatua mbalimbali za upelelezi kwa ufanisi.

Amesema katika kufanya uchunguzi wa matukio ya ubakaji serikali inakabiliwa na changamoto ushahidi kufichwa pale unapohitajika na wahusika wa pande zote mbili kutokana na kuyamaliza matatizo hayo kifamilia.
 
Yanayojiri Bungeni Dodoma Leo mkutano wa sita Januari 31,2017


Mkutano wa Sita wa Bunge unaanza Jumanne Januari 31, 2017 na kumalizika Februari 10, 2017 Mjini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo utaanza na kauli ya serikali kuhusu hali ya chakula pamoja na deni la taifa na hali ya uchumi nchini.


View attachment 465601
Ukumbi wa BungeMkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea Taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge ambapo Kamati 14 za kisekta na mtambuka zitawasilisha taarifa zake Bungeni katika kipindi hiki.


Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:- KIAPO CHA UAMINIFUKufuatia uteuzi wa wabunge watatu walioteuliwa na Mhe. Rais Dk. John PombeMagufuli hivi karibuni na Uchaguzi Mdogo uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Zanzibar Tarehe 22 Januari 2017, kutakuwana Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wapya wanne ambao ni:- Mhe. Alhaji Abdallah Majula BulemboMhe. Prof. Palamagamba John KabudiMhe. Anne Kilango MalecelaMhe. Ali Juma Ali - (Jimbo la Dimani)MASWALIKatika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwapapo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi.


KAULI ZA MAWAZIRIAidha, katika Mkutano huu wa Bunge Kauli mbili za Mawaziri zitawasilishwa kama ifuatavyo:-Kauli ya Serikali Kuhusu Hali ya Chakula Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.

Kauli ya Serikali kuhusu Deni la Taifa na Hali ya Uchumi Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.MISWADA YA SHERIAKatika mkutano huu, miswada ifuatayo itajadiliwa...Muswada wa Sheria ya Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa mwaka, 2016 (The Medical, Dential and Allied Health Professionals Bill2016).


Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na.4) wa mwaka 2016. {The Written Laws (Miscellaneous Amendments)}, Bill, 2016)
 
Hili ndio swali tunalotakiwa kupata majibu yake na kama hayupo basi this is something serious na tunapaswa kuanza kuwaza nje ya box.
 
Ataibukia Bungeni........Alhamisi na kuomba kuuliza swali kwa PM....ikiwemo usalama wake kama Mbunge na heshima ya wabunge ndani na nje ya Bunge
 
Waulize pia na zile ajira mpya na uhamisho wa watumishi utakuwa lini, sijui kwann wapinzani hawatumii hii kete, wataungwa mkono sana coz vijana wengi wapo mtaan jobless na walishaahidiwa ajira zipo ila hakuna dalili.
 
maswal n yale yale na majb n yale yale ya cku izote. selkar ina mpango.,,,,)
 
Hivi huwa hakuna maswali mapya? naona maswali ya toka mwaka 2005-2010-2010-2015 ni yale yale tu, hakuna mapya...

Hivi Bunge ni kijiwe cha kukutana na kupigiana story za Uongo na kweli?
 
Back
Top Bottom