YAJUWE MAHITAJI 18 MUHIMU YA MWANAMKE.

YAJUWE MAHITAJI 18 MUHIMU YA MWANAMKE.

Joined
Aug 8, 2018
Posts
13
Reaction score
9
Na Joachim Mkwawa
[emoji2398]Rejesha Mahusiano Yaliyovunjika.

Habari yako ndugu na Mwanajamii mwenzangu.

Leo nataka uyajuwe,ujifunze na utimize wajibu wako kwa Mpenzi wako ama mwandani(mwanandoa)wako.Na kama nilivyotiririka hapo juu ni kwamba nitaangazia MAHITAJI 18 MUHIMU YA MWANAMKE KATIKA MAHUSIANO AMA NDOA.

Kuna ukweli kwamba Mahali popote palipo na changamoto katika Mahusiano ama Ndoa ni dhahiri kwamba Mwanaume hakutimiza wajibu wake.
Ukweli huu wengi huupinga hasa sisi wanaume na hii ni kwa sababu kwamba Muwamba ngoma huvutia kwake na ile hali ya kutokujuwa yatupasayo kuwajibika nayo kwa wanawake wetu tuwapo kwenye mahusiano.

Tafsiri fupi tu ya ndoa ni kwamba Ndoa ni kujidhiki wewe,kujitoa wewe,kwa ajili ya mwenzio.Na 75%ya maisha ya mwanamke hutegemea sana uwepo wa mwanaume;hata kama Mwanamke huyo atakuwa na mali kiasi gani.Hii ni hutokana na ukweli kwamba kuna mahitaji hayo 18 muhimu hawezi kuyapata na kutlridhika nayo kutoka popote zaidi ya mwanaume.

Pia 75%ya maisha ya mwanaume katika mahusiano ni Kuwajibika(Man management power)kwa mkewe.Sasa wajibu wako kama mwanaume kwa mkeo ni kutimiza mahitaji yake.
Kutokuyajuwa hayo mahitaji na kuyatimiza ipasavyo ndiko huwa kunaleta mitafaruku,migogoro na migongano ya kifikira na hata kumfanya mwanamke ajaribu kutafuta uhitaji kutoka nje.

Leo ondokana na tatizo hilo kwa kuyajuwa na kuyatimiza yafuatayo:-.
(1)AMANI YA NAFSI.
~Ndugu yangu;Mwanamke huhitaji sana Amani.Tena Amani hii ni ile impayo mtu utulivu ndani ya moyo.Haijalishi kuna mapishano fulani huwa mnapitia na hata kupigana.Mwanamke anahitaji mahala salama kwake,anahitaji mahala pa utulivu.
Na kipimo cha hili hitaji ni kwamba unapokuwa naye je,anakufurahia??.Anao uhuru wa kukusemesha ama kukuhoji chochote hasa pale anapokuwa amekukwaza ama umemkwaza??.Je,inapotokea haupo anakuwaje??,Ama inapotokea umekasirika anapatwa na hali gani??.Na je,ukimkwaza na ukajirudi kutaka muyamalize anachukuliaje??.

Sasa mahala pasipo na Amani hata kuwajibika huwa hakupo.Mume ukiingia tu nyumbani mke hukosa raha,Huogopa kukusemesha nk.Hali hii wewe mwanaume usitaraji kupata ushirikiano mzuri ktk mambo mbalimbali ikiwemo ushauri na hata jambo la ushirishwaji hukosekana.Hapa ujuwe hakunaga maendeleo.

Ushauri:-
Simama kama mwanaume,timiza wajibu wako kwa kuichochea Amani na mapatano ndani yenu badala ya mabishano na mapishano.

(2)UPENDO:-
~Mwanamke huhitaji upendo wa dhati na wa kweli.Kumbuka Upendo wa kweli huvumilia,Huheshimu,hufariji,Hujali,hutunza na kulinda wengine.Wenzetu hawa wakikosa upendo hujihisi upweke,hukosa Amani na Raha mioyoni mwao.Ukimpenda na kuhakikishia upendo mwanamke naye anakupenda...,na atakuwa tayari kukutumikia na hata kukutetea kwa kila hali popote awapo.
Pasipo upendo pana machafuko,dharau,maudhi na kila aina ya changamoto na hata kufanya uhusiano usiweze kudumu.

(3)TUMAINI(HAKIKISHO).
~Mwanamke huhitaji Tumaini.Na siku zote Tumaini ndiyo sababu kubwa ambayo humbakiza mwanamke kwa mme.Tumaini humpa kuvumilia na kustahimiri mikiki mikiki ya mahusiano au ndoa.Tumaini humpa dhanio(tarajio) la uhakika juu ya kile alichokitarajia pindi anaingia nawe katika uhusiano huo mliyo nao.Tumaini humsahaulisha na kumstahimilisha nyakati na hali hasi(mbaya) mnazopitia hasa za kiuchumi na migogoro mbalimbali katika mahusiano yenu.
Je,unamtumainishaje mkeo??.Unamtia moyo anapokosea au hata katika hali ngumu zile mnazopitia kiuchumi??.

Kumbuka tu kwamba Mwanamke huwa haitaji uongo japo huamini katika kudanganywa.Namaanisha kwamba unapomtumainisha(muahidi) hakikisha kweli unafanya kwa vitendo au unaonyesha harakati kwamba unapambana ili kuishinda hali mbaya mliyonay😵nyesha juhudi za kweli katika kile umemuahidi/kumtumainisha.
Hii itakubeba moyoni mwake,itampa ujasiri wa kukuvumilia na kusema hapana mbele ya majangili ama matapeli(wapita njia)wa mapenzi.Je,umeshawahi kuona kwamba mtu fulani mwenye uwezo anamtaka binti mzuri na pengine naye kwao wako vizuri kiuchumi lakini unashangaa binti anajibu kwamba Aliyenaye anamtosha!;na huku anayezungumzwa kuwa anatosha ni hohe hahe??.Hiyo ndiyo nguvu ya Tumaini.
TUMAINI maana yake ni kwamba Tulia ukiwa na mimi kuna ushindi(mafanikio).Tumaini maana yake upo peke yako kwangu nami ni wako hivyo usijali kwani wewe ni wangu na ushindi wako ni wajibu wangu.Leo hatuna kitu lakini hatutaishi hivi milele kwani kesho yetu ni bora kuliko leo.

(4)MAWASILIANO
~Mwanamke hupenda mtu wa mawasiliano.Haijarishi mnapigiana simu ama kutumiana jumbe fupifupi za maandishi(Sms) nzuri nk.Lkn pia mke huhitaji mtu anayejali uwepo wake.Pendelea kumjulia hali uwapo mbali naye,fuatilia yuko wapi anafanyaje,amekula ama la!.Pili Unapokuwa naye faragha(kitandani) usiwe bize na simu,laptop ama vitu vingine visivyo na tija kwake.Usisubiri hadi yeye akusemeshe(aanzishe maongezi),Usisubiri hadi yeye akupapase ndipo ujuwe kwamba anataka haki yake.Mawasiliano mazuri ya faragha hujenga upendo na kumfanya mwanamke ahisi na kuamini kukubalika kwako.


Leo naishia hapa tukutane tena Kesho katika mada hii muhimu kwa mustakabali mzima wa kujenga na kuyaenzi mahusiano na ndoa zetu.

Wako;
Joachim Mkwawa
[emoji2398]REJESHA MAHUSIANO YALIYOVUNJIKA.
joachimmkwawa8@gmail.com
 
Mi ninakaswali et........
Mwanamke anayezungumziwa ni huyuhuyu wa KIENYEJI au ni yale machotara ya KIMAREKANI?????

Kama ni hawa wakina " MWAJUMA NDALA NDEFU" aiseeeeeeeeeeeeee
We west our tymeee
 
Mi ninakaswali et........
Mwanamke anayezungumziwa ni huyuhuyu wa KIENYEJI au ni yale machotara ya KIMAREKANI?????

Kama ni hawa wakina " MWAJUMA NDALA NDEFU" aiseeeeeeeeeeeeee
We west our tymeee
Namzungumzia mwanamke aliye katika mahusiano/ndoa.Hao chotara naamini hata wewe unawajuwa kwamba hawanaga time na mambo ya mahusiano/ndoa.Pesa iko mbele.
Hvy hapa namtaja mwanamke anayeweza kuoleka ama aliyeoleka.
 
Akimaliza..naombeni msaada wa short notes
Ningeweza andika kifupi tu kwa kuyaorodhesha ukanielewa japo naamini usingenielewa kiundani namaanisha nini.Ndiyo maana kwa kila hitaji ama hatua nikalazimika kuitetea hoja kwa kuielezea.
Nakushukuru kushiriki usisite kuendelea utajifunza kitu.
 
Ni vizuri mkuu ukatuwekea na mahitaji ya wanaume
Yah nalijuwa hilo kwa sababu kimsingi mahitaji ya mwenzi wako ndiyo majukumu ama wajibu wako kwake.Hivyo hata mwanamke anapaswa kuyajuwa mahitaji ya mwanaume ili aingiapo katika mahusiano ya kimapenzi ama ndoa ajuwe fika kwamba kuna wajibu anaopaswa kuutimiza kwa mwanaume wake.Hivyo nitaweka
 
Pesa ipo au haipo ?
Kama haipo mahitaji hayo ni batili
Lazima iwepo lkn si kama wengi tunavyodhani bali pesa ipo kupitia hitaji la Matunzo,Kujali na kumhudimia.
Ikiwa unaendesha mahusiano yako hada kwa kumlipa mwanamke pesa kila mara baada ya kukutana Kimwili ama hukutani naye hadi ulipie kwanza basi wazi kwamba huyo si mtu uliye na mipango naye kimaisha.Mpo kwenye biashara.Hivyo hata ukimfumania na mtu hutakuwa na cha kusema ama kumfanya coz huna haki kwake.Mke hawi hivyo brother fanya utafiti utaona.

Kipimo cha mwanamke mwenye nia na wewe iwapo unataka kumjuwa ni kidogo sana.Kimojawapo ni kwamba ikiwa wewe ni mnywaji wa pombe na yeye ni mnywaji basi siku ukiwa vizuri nenda naye baa.Agiza kwa fujo walau round 2 hivi zenye bia tatu tatu kila mmoja.Ukiona haongei usijali.Mkimaliza agiza tena angalau round 1 ya bia mbili mbili kila mtu.Ukweli mwenye nia lazima akukatishe na anaweza mwambia mhudumu no no usilete inatosha ama atakwambia tukanywee nyumbani,au anaweza kuanza kukushauri kuwa utumiaji mbaya wa pesa kiasi hicho kwa ulevi wa masaa tu haufai nk.

Lkn mpita njia(mzugaji/mpitaji) anapoona meza inazidi kupendeza lazima utaona anaagiza maji kuzima nguvu ya pombe,trip za chooni haziishi kwenda kujitapisha.Agizo la jikoni kwamba iletwe nyama choma lazima liwepo.Lkn pia simu za kuwapigia shoga zake na kuwatambia uwepo wake hazitakata.Na wakati mwingine lazima akushauri mhamishe kijiwe.Kifupi haoni uchungu wa pesa yako hata kama hamkuitafuta wote.

Mke ni tabia
 
Back
Top Bottom