Yajue mataifa matano(5) yanayoongoza kwa nguvu za kijeshi duniani!

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,262
1,220
Kawaida taifa linaloongoza kwa teknolojia ya angani yaani mifumo ya kisasa ya RADA na ndege vita huongoza kwa nguvu za kijeshi. pia idadi ya askari ambao wana silaha nzito nzito huongeza kigezo. meli za kisasa zenye nguvu na nyambizi(submarine), makombora ya masafa marefu na ysle ya kudungua ndege au makombora ya kudungua makombora mengine, vifaru vingi vya kisasa na magari yenye vifaa maalum ya kivita huongeza 'credit'. mbinu na uzoefu wa kupigana vita nyingi na hasa ngumu pia ni kigezo. Mataifa yafuatayo yanafunika ktk hayo:
1. MAREKANI. hawa wanaongoza kwa kutengeneza na kuuza ndege nyingi za kisasa na hatari sana duniani mfano B-2 SPIRIT isiyoonekana kirahisi kwenye rada, F-16 n.k. ndege zao zimeuzwa hadi Italy, Israel na Saudi Arabia. Pia uwezo wao wa kupambana na adui yeyote huwapa maksi kubwa. Aircraft carrier walizonazo, zimewapa maksi kubwa. pia wanasifika kuwa na vikosi hatari vya makomandoo vijulikanavyo kama SEAL-SEA, AIR and LAND
2. URUSI: wako vizuri ila kusambaratika kwa USSR kuliwafanya washuke kiuchumi na hivyo uwezo wao wa kijeshi kidogo ukaathiriwa. hili ndo taifa lenye ndege nzuri nyingi za kisasa baada ya Marekani. mataifa mengi yasiyoshibana na nchi za magharibi hupenda kununua ndegevita na vifaa vingine hatari kwa Warusi. mfano IRAN, SYRIA na LIBYA
3. CHINA: wako vizuri pia hasa ardhini na majini. ndegevita zao havina nguvu sana ukilinganisha na zile za Wamarekani na Warusi. wanatengeneza makombora mazuri na hatari sana. wana vifaa vingi vikali vya jeshi la ardhi hasa vifaru imara na vya kisasa. wanaongoza kuwa na idadi kubwa ya askari duniani tena wakiwa na silaha nzitonzito.
4. UINGEREZA: wapo vizuri pia hasa angani na pekee sana majini. ndege zao maarufu za kivita ziitwazo PHANTOM zinawabeba sana. wanasifika kuwa na mimeli na minyambizi ya hatari.
5. JAPAN: wazuri na wasiri sana ktk teknolojia zao za kivita. ktk mataifa makubwa duniani Japan hawapendi kuuza sana silaha zao za kivita. ndiyo sababu ktk vita ya dunia kambi za kijeshi za Marekani zilipigwa na ndegevita hatari za Kijapan ambazo Wamarekani hawakuwahi kuzijua. waliwajibu kwa NYUKLIA huko HIROSHIMA na NAGASAKI. cha pekee kwa Wajapani ni mimeli ya kisasa. najua mnafahamu viwanda vikubwa duniani vya meli viko huko. pia jeshi lao la ardhi liko vzr sn.
Bila shaka ISRAEL, UFARANSA na UJERUMANI wangefuata baada ya hapa.
 
us propaganda nyingi tu ndo maana vita nyingi anakimbiaga hajawahi kushinda mrusi ni noma ayse
 
Yani kwa macho unajua nani hatari zaid.sasa ivi unasikia tena habari ya islamic state zaid ya kusikia kuw wamepotez maeneo
 
So far what I know, Russia ndo nchi ya kwanza. Sababu kadhaa
1. Kuanguka kwa USSR kulichangiwa kwa kiad kikubwa na over investment in military. Bado wana silaha nyingi na bora tangu cold war

2. Wako vizuri kwa technology ya vita ambayo nchi nyingi hats USA wameshindwa kuzi-counter. Mfano Ballistic missile zao no bora zaidi duniani zinacover long distance most destructive na margin of error in ndogo
Battery defence system yao ni bora zaidi. Mf. S-300 battery system haijapata mfano wake duniani na tayari wameshaupgrade kwenda S-400

3. Uchumi wao unategemea zaidi kuuza silaha nje. Hii imewafanya wawe more competitive na innovators
Etc etc etc
 
1.lie....ussr waliangushwa na marekani sababu kuwashinda katika inteligence techniques,yaani C.I.A. ndio maana baadae K.G.B ikawa decommissioned sabab waliona ina matatizo...na kuanguka kwa bei ya mafuta pia kulichangia nchi kushindwa kujiendesha(also C.I.A walihusika katika hili)
2.Hakuna vita yyte izo defence system silitestiwa zikaonekana hatari zaidi ya exaggeration za kwenye youtube basi...Huwezisema kitu flani n i bora kuliko kingine bila kuona challenge ilizo zi counter.
3.uchumi wa russia unategeme oil for 60%+
 
1. Over investment in military in moja ya sababu sio sole reason kufeli kwa USSR
2. Hakuna millitary technology inayookuwa operational bila testing. S-300 defence system ni best in tje world tafuta source yoyote unayoamini. Iko juu zaidi ya USA's patriotic missile system kwa vigezo vingi tu. Na mbaya zaidi wakati USA na NATO hawajapata namna ya ku i-evade jamaa wameupgrade kwenda S-400

Jaribu kukumbuka speech ya obama alipokuwa anajaribu kuucalm down ulimwengu kuhusu tishio la Russia
 
Pia wenzetu wana economy diversification. Baada ya mafuta arms sales ni source yao kubwa ya mapato. Jaribu kufuatilia kwa mfano mauzo ya hiyo S-300 kwa Iran yatagharimu kiasi gani ndo utapata picha
 
#mmarekani kule #iraq ,vietnam, afaganistan,#libya ....#mrusi kawai kupigana vita gani karne ya sasa??
Inabidi ujue nchi haipimwi nguvu kwa kuingia vitani moja kwa moja tu. Kuna vigezo vingi mf. Kupitia nchi zingine zilizo vitani inaziuzia silaha kuangalia ufanisi wake. Vita kuu ya pili ya dunia ilitanguliwa na Spanish Civil War ambapo Hitlet na washirika wake walishiriki kumdsidis General Franco ili kujaribu military capability yao.

Turudi keenye mada. Urusi iko vitani pande nyingi. Migogoro mingi unayoona imekua migumu kutatuliwa na USA ina urusi nyuma yake mf. Syria na Ukraine mashariki. Silaha za urusi zinatumika huko

Pia ikumbukwe Urusi ni nchi yenye satellite nyingi zaidi na makombora mengi zaidi duniani (ICBM) na pia imekusanya silaha nyingi zaid za nyuklia kuliko nchi yoyote

Nitaizungumzia USA baadaye kidogo
 
mfano #urusi ingepgana vyote ivyo uchumi wake ungekuaje leo??ukraine mrusi hajapgana kaenda kulinda #warusi wenzake ile ya #syria siezi vita coz kuna mkono wa mataifa mengi pale kwa maoni yangu naisi mpaka kusema nchi inaongoza kivita wameangalia vigezo vingi sana
 
Uzi hauzungumzii nguvu za kiuchumi Bali kijeshi. Uchumi wa Russia sio mzuri kama USA. Labda sababu hiyo ndo inakufanya use unageneralize.
 
Back
Top Bottom