Yajue magonjwa hatari yaendezwayo na mbu13

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,831
1. Malaria
Malaria, jina Lina asili ya Italian ikiwa na Maana "upepo mbaya" au “bad air”, ni homa inayosababishwa na vimelea viitwavyo Plasmodium, ambao wanaeneza baada ya kuumwa na mbu jike aitwaye Anopheles.

Kwenye mwili wa mwanadamu, vimelea hawa huzaliana kwenye INI. Na kisha huanza kushambulia seli nyekundu za damu. Mwaka 2013 inakadiriwa kuripotiwa wagonjwa wanaokadiriwa 198 million waliougua malaria duniani kote na kuua watu zaidi ya 500,000 wengi wao wakiwa ni watoto barani Afrika.

Dalili za malaria ni homa, kuumwa na kichwa, na pia kutapika. Dalili hizi huanza kujidhihirisha kati ya siku ya kumi hadi ya kumi na tano baada ya maambukizi. Isipotibiwa haraka malaria ni hatari kwa maisha, kwani huathiri mfumo mzima wa ysambazaji wa damu.
Sehemu mbalimbali vimelea vya malaria vimekuwa sugu kwa dawa mbalimbali

2. Lymphatic filariasis (elephantiasis) Homa ya Matende
Ugonjwa wa matende ni aina ya ugonjwa unaosababisha ngozi na tishu zilizo chini ya ngozi ya mwanadamu kuwa nene (thickening of skin and underlying tissue).Ugonjwa huu huathiri miguu, mikono, figo, korodani na kusababisha korodani kuvimba na kuwa kubwa sana.

Inakisiwa watu milioni 120 duniani wana maambukizi ya ugonjwa huu ambapo kati yao milioni 40 wamepata madhara makubwa kutokana na ugonjwa huu. Kati ya hawa walioathirika theluthi moja huapatikana katika bara la Afrika, theluthi moja nyingine hupatikana India, na kiwango kilichobakia hupatikana katika visiwa vya Pacific, Marekani na Asia ya kusini.

Ugonjwa wa matende husababishwa na vimelea aina ya minyoo (parasitic worm) vinajulikana kama Wuchereria bancrofti, Brugia malayi, B. timori ambavyo huenezwa na mbu jike aina ya culex quinquefasciatus mosquitoes na jamii fulani ya mbu dume (Anopheles species) wakati minyoo aina ya Brugia roundworms huenezwa mbu wanaojulikana kama Mansonia mosquitoes. Mbu hawa hueneza ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwengine.

Aina nyingine ya ugonjwa wa matende inayojulikana kama nonparasitic elephantiasis au podoconiosis ambayo haisababishwi na vimelea vyovyote hupatikana katika nchi za Afrika Mashariki (Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi) Sudan, Egypt na Ethiopia. Asilimia 6 ya maambukizi ya aina hii ya podoconiosis hupatikana nchini Ethiopia.

Nini hutokea baada ya maambukizi?
Kwa kawaida mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu huwa na mabuu (larvae) kwenye mfumo wa damu mwilini mwake wanaojulikana kama microfilariae. Mabuu haya husafiri kutoka kwenye mfumo wa damu hadi kwenye mfumo mwingine unaojulikana kama mfumo wa limfu (lymphatic system) na kukua kuwa minyoo kamili (adult worms) ambayo huziba mfumo huu wa limfu ambao unategemewa sana katika kuweka uwiano sawa wa maji (fluid balance) kati ya mfumo wa damu na tishu ndani ya mwili na husaidia kuupa mwili kinga dhidhi ya magonjwa mbalimbali.

Minyoo hii huishi kwa miaka minne hadi sita na katika uhai wake huzaa mamilioni ya mabuu (microfilariae) mengine wakati ikiwa kwenye mfumo wa damu.

Mbu huenezaje ugonjwa huu?
Mtu ambaye ameambukizwa ugonjwa huu huwa na mabuu kwenye mfumo wake wa damu na anapongatwa na mbu ambawo wanauwezo wa kuchukua mabuu haya ambayo huendelea kukua na kufikia hatua ya kuambukiza mtu mwingine ndani ya mwili wa mbu.Kwa kawaida, ukuaji huu wa mabuu ndani ya mwili wa mbu huchukua wiki moja hadi tatu na baada ya kukua na kufikia hatua ya kuambukiza mtu mwingine, mabuu haya husogea mpaka kwenye sehemu ya mdomo wa mbu ambayo ndio huwa humng'ata mtu wakati mbu anapofyonza damu kutoka kwa mtu. Mbu mweye mabuu kwenye mdomo wake anapomngata mtu ili kufyonza damu, ndipo mabuu haya yanapoingia kwenye mwili wa mtu na hivyo kusababisha maambukizi ya ugonjwa huu.

Dalili za ugonjwa huu ni zipi?
• Dalili kubwa ya ugonjwa huu ni kuvimba sehemu ya chini ya mwili yaani kwenye miguu na vidole.Pia mtu anaweza kuvimba sehemu ya mikono au mkono wote pamoja na vidole vya mkononi. Wengine huvimba kwenye korodani (wanaume).
• Kuhisi uzito na kukamaa kwa mikono au miguu kutokana na uvimbe uliopo.
• Kutoweza kutumia kiungo husika kilichovimba.
• Maumivu au kutohisi vizuri kwenye mikono au miguu.
• Kupata maambukizi ya mara kwa mara kwenye sehemu iliyovimba.
• Ngozi kuwa nene na ngumu kwenye mikono au miguu.
Dalili nyingine ni pamoja na

Homa
Maumivu ya kichwa
Maumivu kwenye jointi na mifupa
Kutapika
Vidonda kwenye mikono au miguu
Mistari ya rangi nyekundu inayoonekana kwenye mikono au miguu (red streaks)

Vipimo vya uchunguzi

• Blood examination under microscope - Kipimo cha kuangalia damu kwenye hadubini ili kuangalia kama kuna mabuu ya ugonjwa huu wa matende.Kwa wale ambao wana ugonjwa huu kwa muda mrefu, mabuu hayaonekani kwenye damu kwani tayari yatakuwa yameshaingia kwenye mfumo wa limfu. Hivyo, kutoonekana kwa mabuu kwenye damu kwa kutumia hadubini si kigezo cha kusema kwamba mgonjwa hana ugonjwa huu wa matende.

• Vipimo vyengine vinavyoweza kutumika ni pamoja na CT Scan, MRI, Doppler Ultrasound, Radionuclide Imaging ili kuweza kutofautisha ugonjwa huu na magonjwa mengine yanayosababisha kuvimba kwa miguu au mikono kama saratani za aina mbalimbali, kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu (blood clot) na kadhalika.

• Kwa wale wenye kuvimba korodani, ni muhimu kwa daktari kuchukua kipimo kwa kukwangua sehemu husika kisha kuchanganya na potassium hydroxide na kutazama kwenye hadubini kama kuna dalili (Meddler bodies, sclerotic bodies) za ugonjwa wa fangasi unaojulikana kama chromobalstomycosis (unaosababishwa na fangasi aina ya Fonsecaea pedrosoi, Phialophora verrucosa, Cladosporium carrionii, au Fonsecaea compacta). Pia ukungu huu huweza kuoteshwa maabara ili kuangalia kama kuna fangasi aina yoyote ile niliyotaja hapo juu watakaota.

Tiba ya ugonjwa wa matende ni nini?
Tiba ya ugonjwa wa matende hutegemea na sehemu husika. Kwa wagonjwa walio katika jangwa la sahara, tiba ni dawa aina ya albendazole pamoja na ivermectin. Kwa wagonjwa waliopo sehemu nyingine duniani tiba huusisha matumizi ya albendazole pamoja na diethylcarbamazine.

Kusafisha sehemu iliyoathiriwa na ugonjwa wa matende mara kwa mara husaidia kupunguza dalili na viashiria vya ugonjwa huu.

Kwa wale waliovimba korodani kutokana na ugonjwa wa matende, tiba yake ni upasuaji.Wakati mwingine, kama mgonjwa atakuwa amevimba sana korodani, basi baada ya kufanyiwa upasuaji wa kawaida, atahitaji kufanyiwa upasuaji kurekebishwa ngozi yake (plastic surgery).

Katika utafiti uliofanywa na chuo cha Liverpool school of tropical medicine mwaka 2005, umeonyesha dawa ya antibiotiki hususan doxycyline inaweza kutumika kutibu ugonjwa huu wa matende kutokana na minyoo (adult worms) kuwa na bakteria aina ya wolbachia wanaoishi ndani ya minyoo hii, hivyo dawa hii hutibu kwa kuua bakteria hawa na kusababisha minyoo hii kufa, na kuondosha kabisa microfilariae kwenye damu ya mgonjwa na hivyo mgonjwa kupona. Dawa hii hutumika kwa muda wa wiki 8. Hata hivyo, kama mgonjwa atakuwa na mabuu ndani ya mfumo wake wa limfu, basi itakuwa vigumu kwake kupona. Utafiti zaidi unahitajika ili kuwa na uhakika zaidi juu ya dawa hii kutibu ugonjwa huu.

Kinga ya ugonjwa wa matende ni nini?

• Shirika la afya duniani (WHO) limeanzisha jitihada za kutokomeza ugonjwa huu wa matende ifikapo mwaka 2020.
• Matumizi ya dawa aina ya albendazole kwa wale walio katika hatari kupata ugonjwa wa matende unaosababishwa na vimelea.
• Kuvaa viatu wakati wa kutembea nje ili kujikinga kupata maambukizi ya aina ya podoconiosis.
• Kuosha miguu na mikono kwa kutumia maji na sabuni
• Kuosha miguu kila siku kwa kutumia antiseptic (bleach).


3. Yellow fever/ Homa ya Manjano
Homa ya manjano (pia: Homanyongo, inayojulikana kwa Kiingereza kama yellow jack au yellow plague,) ni ugonjwa mkali unaosababishwa na virusi.
Katika hali nyingi, dalili hujumuisha homa, homa ya baridi, kukosa hamu ya chakula, kichefuchefu, maumivu ya misuli hasa mgongoni, na maumivu ya kichwa.

Kwa kawaida dalili hupona kwa siku tano. Kwa watu wengine baada ya kupata nafuu, homa hurudi, maumivu ya fumbatio hutokea, na uharibifu wa ini huanza na kusababisha ngozi ya njano. Ikiwa hii itatokea, hatari ya kuvuja damu na matatizo ya figo unaongezeka.


4. West Nile fever/ Homa ya Maghabiribi mwa Nile
Homa hiyo inatapakazwa na virusi vinavobebwa na mbu, ambavyo mwanzo viligunduliwa Uganda. Dalili zake ni homa, maumivu makali ya kichwa, kuchoka sana, maumivu ya mwili, kuwashwa mwili, kutapika, mwili kutoka vipele na kutoka mitoki.

5. Dengue fever/ Homa ya Dengue
HOMA YA DENGUE : MAMBO MUHIMU KUFAHAMU
Homa ya dengue huitwa pia homa inayovunja mifupa ( breakbone fever), ni moja ya maradhi ambayo hutokea zaidi msimu wa mvua. Dengue husababishwa na virusi ambao hukupata baada ya kung’atwa na mbu.

Kuna aina 4 za virusi vinavyosababisha Dengue ; DENV-1, DENV-2, DENV-3 na DENV-4.
Ikitokea umeugua Dengue kutokana na aina moja ya kirusi mwili hutengeneza kinga dhidi ya kirusi hicho lakini kinga hiyo haiwezi kuzuia maambukizi ya aina nyingine ya virusi vya Dengue. Kwa sababu kuna aina 4 za virusi vya Dengue katika maisha yako unaweza kuugua Dengue hadi mara 4. Lakini hofu kubwa ni kwamba baada ya kuugua Dengue mara moja maambukizi yanayofuata huja na dalili mbaya zaidi kuliko maambukizi ya mara ya kwanza.

Virusi wa dengue husambaa kupitia mbu jike aina ya Aedes Aegyptus.
Kirusi anayesababisha ugonjwa wa Dengue
Mbu anayesambaza Dengue ana tabia za kipekee……Mbu anaesambaza dengue huitwa Aedes aegypti;

Mbu huyu ni mdogo mwenye rangi nyeusi na madoa meupe. Kitabia mbu hawa hutaga mayai kwenye maji yaliyotuama hasa kwenye makopo ya maua, hupendelea makopo yenye rangi nzito yaliyo kwenye eneo lenye kiza au matenki yaliyo wazi.

Mbu wa dengue hung’ata vipindi viwili kwa siku, hung’ata asubuhi kabla jua kuchomoza mfano wakati unafungua mlango asubuhi au unatoka kwenda nje ya nyumba, pia hung’ata wakati wa jioni masaa machache kabla ya jua kuzama. Mda mwingine mbu wa dengue hung’ata usiku maeneo yenye mwanga. mfano kwenye baa watu wakiwa wanakunywa.

Tofauti ya mbu wa malaria na Mbu wa dengue, ni kwamba mbu wa dengue hung’ata watu bila kushtukiwa kwa sababu huwa hana kelele na hupendelea kuuma sana kwenye magoti na viwiko.
Mbu aina ya Aedes aegypt ambaye husambaza Dengue

Msimu wa mvua na ugonjwa wa Dengue

Dengue ni moja ya magonjwa ambayo huja na mvua ambayo yana jina lisilo rasmi ; Monsoon diseases (Kundi hili la magonjwa hujumuisha na malaria , magonjwa ya kuhara pia). Wakati wa mvua mbu wanaosambaza ugonjwa wa Dengue huzaliwa kwa wingi pia mbu hawa hukimbilia ndani ya makazi wakati wa mvua hivyo kuwa rahisi kung’ata watu

Ugonjwa wa Dengue huja katika muonekano wa aina mbili
Muonekano aina ya kwanza : Dengue ya kawaida

Aina hii ya Dengue ndio hupata watu wengi na huwa haina madhara makubwa. Dengue ya kawada huanza siku 4 hadi 10 baada ya kung’atwa na mbu mwenye virusi vya dengue.

Huanza na dalili kama mafua yanayoambatana na homa kali
Homa huambatana na dalili kama:

Kichwa kuuma sana na kuwa na maumivu nyuma ya macho
Maumivu ya misuli na viungo
Mwili kuchoka sana
Kuvimba mitoki (lymph nodes).

Muhimu kufahamu mtoto akipata dengue dalili za mwanzo huwa tofauti na mtu mzima anaweza kuwa na homa tu.

Muonekano aina ya pili: Dengue Kali

Hii ni Dengue ambayo huwa na madhara makubwa huweza kupelekea kifo

Dalili zake huja baada ya dalili za Dengue ya kawaida, hujumuisha :

Tumbo kuuma sana
Tumbo kuanza kujaa
Kutapika zaidi ya mara tatu kwa siku
Kutapika damu hata mara moja
Kupoteza fahamu kwa ghafla
Kutoka damu kwa ngozi, puani au masikioni

NB : Katika watu 100 wanaopata dalili mbaya za ugonjwa wa dengue, wagonjwa 90 huwa Watoto wenye umri chini ya miaka 15. Hivyo mtoto anapoumwa dengue inapaswa kuchukulia ugonjwa wake kwa uzito mkubwa na umakini.

Mgonjwa wa dengue hupitia hatua 3 za ugonjwa…..

Ugonjwa wa Dengue huwa na hatua 3 za kuumwa ; Hatua ya homa, Hatua ya hatari na hatua ya kupona

01. Hatua ya homa
Hatua hii huanza na homa ya ghafla inayoambatana na maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, maumivu ya maungio kama magoti, na mwili kupoteza maji

02. Hatua ya hatari
Hatua hii huja siku ya 3 hadi 7 baada ya kuanza kuugua. Hutokana na mishipa ya damu kuanza kufuja plasma na virusi vya Dengue kushambulia seli zinazogandisha damu.
Utaanza kupata damu kwenye ngozi, kutoka damu puani au masikioni, mishipa ya damu kuvuja plasma na kusababisha shock. Hudumu kwa zaidi ya masaa 48.

kuna hatari kubwa ya watu kupoteza maisha katika kipindi hiki endapo kusipopatikana matibabu sahihi.

03. Hatua ya Uponaji
Katika hatua hii mwili huwa na uchovu sana ambao utadumu kwa zaidi ya wiki

Ukali wa ugonjwa wa Dengue hutegemea vitu kadhaa

Umri wako (watoto hupata Dengue kali)
Iwapo una mimba au la (Dengue huwa kali kwa mjamzito)
Iwapo una maradhi mengine kama kisukari, UKIMWI nk
Lishe yako
Iwapo ushawahi ugua dengue kabla (Dengue ya pili huwa kali)
Ubora wa huduma za afya ulizopewa

Uponaji wa Dengue

Ugojwa wa dengue mara nyingi huisha wenyewe, idadi ya vifo huwa ni ndogo katika watu 100 wanaougua dengue ni mtu 1 tu anayeweza kufariki. Tatizo huja iwapo mtu kapata aina ya ugonjwa mkali wa dengue vifo kwa wagonjwa 100 hufikia 5 lakini iwapo hutapata tiba yoyote uwezekano wa kufariki hufikia asilimia 50

USIJITIBU NYUMBANI, NENDA HOSPITALI

Kama una dalili za dengue kama homa kali na kichwa kuuma jitahihidi kuwahi hospitali
Hospitali daktari atachukua maelezo yako na kukupima mwili.
Kipimo cha dengue huchukuliwa kwenye damu , pia kupitia damu daktari atapima wingi wa chembechembe zinazogandisha damu na wingi wa damu.

Ukiwa na dengue utaanzishiwa matibabu ya kuupa sapoti mwili, kupunguza maumivu pia unaweza kuhitaji kuongezewa chembechembe sahani za damu (platelet transfusion)

KANUNI ZITAKAZOSAIDIA MWILI WAKO UWAHI KUPONA

01. Pumzisha mwili kwa kulala

02. Kunywa maji ya kutosha na vimininika vingi kama juisi

03. Tumia dawa za kupunguza homa

04. Usitumie aspirin au ibuprofen
6. Chikungunya
Chikungunya is a mosquito borne virus that has been identified in over 60 countries in Asia, Africa, Europe and the Americas. In late 2013, chikungunya virus was found for the first time in the Americas on islands in the Caribbean, since then, well more than 1 million local transmission cases have been reported.
Chikungunya is a viral disease transmitted by the bite of infected mosquitoes such as Aedes aegypti and Aedes albopictus. It can cause high fever, join and muscle pain, and headache.
Chikungunya does not often result in death, but the joint pain may last for months or years and may become a cause of chronic pain and disability.
There is no specific treatment for chikungunya infection, nor any vaccine to prevent it. Pending the development of a new vaccine, the only effective means of prevention is to protect individuals against mosquito bites.
7. Zika fever
The Zika virus is also transmitted through the bite of an infected Aedes species mosquito, the same mosquitoes that spread dengue and chikungunya viruses.
If symptomatic, symptoms are generally mild–fever, rash, joint pain, or red eyes. Severe disease requiring hospitalization is uncommon and deaths have not been reported.
Outbreaks of Zika virus disease (or Zika) previously have been reported in tropical Africa, Southeast Asia, and the Pacific Islands. Zika virus likely will continue to spread to new areas. In May 2015, the Pan American Health Organization (PAHO) issued an alert regarding the first confirmed Zika virus infections in Brazil.
8. Ross River fever
Ross River virus disease (RRVD) is a mosquito borne virus. About 55%–75% of people who are infected do not feel sick, according to the US Centers for Disease Control and Prevention (CDC).
For those who do feel sick, symptoms of RRVD include joint pain and swelling, muscle pain, fever, tiredness, and rash. Most patients recover within a few weeks, but some people experience joint pain, joint stiffness or tiredness for many months.
RRVD infection cannot be spread from person to person. It is found throughout Australia, Papua New Guinea, parts of Indonesia and the western Pacific Islands.
9. Eastern Equine Encephalitis
Eastern Equine Encephalitis (EEE) is spread to horses and humans by infected mosquitoes, including several Culex species and Culiseta melanura.
Symptoms of EEE disease often appear 4 to 10 days after someone is bitten by an infected mosquito.
EEE is a more serious disease than West Nile Virus (WNV) and carries a high mortality rate for those who contract the serious encephalitis form of the illness. Symptoms may include high fever, severe headache, stiff neck, and sore throat. There is no specific treatment for the disease, which can lead to seizures and coma.
10. Japanese Encephalitis
Japanese encephalitis (JE) is the most important cause of viral encephalitis in Asia. About 68,000 clinical cases are reported annually. It usually occurs in rural or agricultural areas, often associated with rice farming.
Japanese encephalitis geography/CDC
Japanese encephalitis geography/CDC
JE virus is transmitted to humans through the bite of infected Culex species mosquitoes, particularly Culex tritaeniorhynchus.
Most JE virus infections are mild (fever and headache) or without apparent symptoms, but approximately 1 in 250 infections results in severe disease characterized by rapid onset of high fever, headache, neck stiffness, disorientation, coma, seizures, spastic paralysis and death. The case-fatality rate can be as high as 30% among those with disease symptoms.
There is a protective vaccine against Japanese encephalitis virus.
11. La Crosse Encephalitis
La Crosse encephalitis virus (LACV) is transmitted to humans by the bite of an infected mosquito. Most cases of LACV disease occur in the upper Midwestern and mid-Atlantic and southeastern states.
It was reported first in 1963 in LaCrosse, Wisconsin and the vector is thought to be a specific type of woodland mosquito (Aedes triseriatus) called the tree-hole mosquito.
Among people who become ill, initial symptoms include fever, headache, nausea, vomiting, and tiredness. Some of those who become ill develop severe neuroinvasive disease (disease that affects the nervous system).
In rare cases, long-term disability or death can result from La Crosse encephalitis.
12. St. Louis Encephalitis
St. Louis Encephalitis (SLE) is transmitted from birds to man and other mammals by infected mosquitoes (mainly some Culex species). SLE is found throughout the United States, but most often along the Gulf of Mexico, especially Florida.
Most persons infected with SLEV have no apparent illness. Initial symptoms of those who become ill include fever, headache, nausea, vomiting, and tiredness. Severe neuroinvasive disease (often involving encephalitis, an inflammation of the brain) occurs more commonly in older adults. In rare cases, long-term disability or death can result.
13. Western Equine Encephalitis
Western Equine Encephalitis (WEE) is found west of the Mississippi including parts of Canada and Mexico. The primary vector is Culex tarsalis.
As with EEE a vaccine is available for horses against WEE but not for humans
 
Ukienda nyamisati kuna mmbu balaaaa tena ni mmbu wanaambukiza ugonjwa wa matende

Ova
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom