Yafahamu yafuatayo kuhusu meno ya mwanadamu

hydroxo

JF-Expert Member
Oct 19, 2015
3,293
6,878
1.Mwanadamu uanza kuota meno,kabla hajazaliwa,na meno huchomoza juu na kuonekana baada ya miezi 6 mpaka mwaka baada ya kuzaliwa.

2.Wastani wa urefu wa jino la mwanadamu ni sentimita 2

3.1/3 ya jino la mwanadamu huwa chini ya fizi na 2/3 ya jino huchomoza juu ya fizi,hii ni sawa na kusema kipande cha chini cha jino ni kirefu zaidi kuliko cha juu.

4.kibadara mnemba(enamel) ambayo ni sehemu ya juu ya jino ndio sehemu ngumu kuliko zote katika mwili wa mwanadamu.

5.Kwa kawaida mwanadamu hutumia sekunde 45 mpaka 70 kusafisha meno wakati muda unaoshauriwa kiafya ni dakika 2-3 kila siku.

6.seti za meno ni kitu cha pekee ukitoa alama za vidole ambazo hazilingani kati ya mtu mmoja na mwingine.

7.Mtu mzima ana jumla ya meno 32.

8.Jino lililowahi kuuzwa kwa bei ya gharama kuliko yote duniani ni la mwanafizikia Isaack Newton.liliuzwa kwa $3633 mnamo mwaka 1816 nchini uingereza.

9.mwanadamu hutumia wastani wa siku 39 katika kipindi cha maisha yake yote kusafisha meno.

10.mwanadamu ana aina kuu 4 za meno.
 
9. Hizo siku 39 katika maisha, mbona ni za mwezi 1 na wiki 1 inamaana binadamu huishi siku 39 hapo nadhani umechemka lekebisha hiyo.
 
Duu JF ni zaidi ya hivi vyuo kata, kuna kila aina ya elimu
 
Je kwa kawaida mtoto mdogo anatakiwa aanze kuota meno ya juu au chini? Na kama inatakiwa juu ikaanza chini au inatakiwa chini ikaanza juu wa does it imply?
 
9. Hizo siku 39 katika maisha, mbona ni za mwezi 1 na wiki 1 inamaana binadamu huishi siku 39 hapo nadhani umechemka lekebisha hiyo.
nadhani hujamwelewa vizuri,ina maana ukichukua muda unaopiga mswaki kila siku mf:leo dakika moja,kesho sekunde 50 nk kwa maisha yako yote ukaujumlisha utapata siku hizo 39 kuwa ulizitumia kupiga mswaki.
 
Amavubi,zifuatazo ni aina kuu nne za meno ya mwanadamu;

1.meno ya mbele au ya kukatia(incisors); meno haya hupatikana mbele ya mdomo na kwa idadi ni 8, manne kwa kila taya(taya ya juu manne na taya ya chini manne) sifa yake kubwa ni kuwa marefu na yaliyochongoka.

-kazi yake kubwa ni kukatia vitu.

2.machonge(canine); haya hupatikana baada ya meno ya mbele na kwa idadi ni manne,mawili juu na mawili chini,yamechongoka kiasi na ni makali pia kazi yake kubwa ni kuchanachana na kulalua chakula.

3.magego madogo(pre-molars); haya ni meno baada ya machonge na ni manene kiasi,pia yana kigongo huku na huku na msawazo katikati,kwa idadi ni 8 manne kwa kila upande.

-kazi yake kubwa ni kusaga chakula.

4.magego(molars);haya hupatikana mwishoni mwa mdomo na ni 12 kwa idadi sita kwa kila upande,ni manene mapana na yenye nguvu pia yana msawazo mkubwa.

kazi yake kubwa ni kusaga chakula.
 
Mi sidhani watoto wanatoka kwa Mungu kama ndio uchuro nayo ni baraka Mungu aliyonipa jinsi mwanangu alivyomzuri na anavyonipenda siwezi kumdhuru kiss meno yalivyoota. Cause I have heard a story zamani mtoto akiota meno hivyo watu walikuwa wanaenda kumuacha porini na kuondoka sijajua tatizo ni nn kwa watoto wanaoota meno vice versa.
 
Mi sidhani watoto wanatoka kwa Mungu kama ndio uchuro nayo ni baraka Mungu aliyonipa jinsi mwanangu alivyomzuri na anavyonipenda siwezi kumdhuru kiss meno yalivyoota. Cause I have heard a story zamani mtoto akiota meno hivyo watu walikuwa wanaenda kumuacha porini na kuondoka sijajua tatizo ni nn kwa watoto wanaoota meno vice versa.T
Those were primitive beasts.
 
Back
Top Bottom