Nimejipiga mwenyewe nikanunua azam unga,maziwa,samli,mayai.Nikachemsha samli iyeyuke nikachanganya unga,yai moja,chumvi kidogo,na sukari kiduchu kwa ladha maji yakawa maziwa nikakanda weee mpaka unga ukawa unalia pichuuuuuu pichuuuuu ukawa tayari niaketengeneza madonge haaaa zilizonifanya sina hamu nazo tamuje sasa tamu balaa ila sasa ni kau kau hapa nshazikatakata namuwekea dogo kwa mfuko aende nazo kaukau na mie nimeziweka juu ya friji ziwe nangatai zangu.
Poor me sijui kupika chapati kila nkipika ni kaukau tu.Asa leo nikaweka yai sababu yai zinalainisha nazo zikantenga picha ya hizo kaukau ntawawekea kesho.
Pia kama umeweka mafuta kidogo sana inaweza fanya chapati kua ngumu
ishuu sio recipe ni kuhusu kulaini tu ndo ishu zenyewe..
Huko kulainika ntamwambia tu kwa mdomo chapati lainika? Lazima recipe ili vipimo viende sawa na step kwa ajili ya super soft chapati
Chapati ili iwe kaukau inategemea haujaulanisha vya kutosha au umepika kwenye moto mdogo. Jipime hapo tu. Mayai, samli ni vikolezeo tu kama karoti kwenye wali ambao unaweza kuiva vizuri kuwa bokoboko au kuwa mbichi.
Nimejipiga mwenyewe nikanunua azam unga,maziwa,samli,mayai. Nikachemsha samli iyeyuke nikachanganya unga,yai moja,chumvi kidogo,na sukari kiduchu kwa ladha maji yakawa maziwa nikakanda weee mpaka unga ukawa unalia pichuuuuuu pichuuuuu.
Ukawa tayari nikatengeneza madonge haaaa zilivonifanya sina hamu nazo tamuje sasa tamu balaa ila sasa ni kau kau hapa nshazikatakata namuwekea dogo kwa mfuko aende nazo kaukau na mie nimeziweka juu ya friji ziwe nangatai zangu.
Poor me sijui kupika chapati kila nkipika ni kaukau tu. Asa leo nikaweka yai sababu yai zinalainisha nazo zikantenga picha ya hizo kaukau ntawawekea kesho.
Hahhahha lol umenifurahisha amu
Hio chapat kwanza km utajipatia kamashine kako kakukandia kasecond hand itakua vizuri!!
Mm hapo siku zote ni bahati nasibu!! Ila pia unga angalia wanasemaaga unga wa ppf sijui ndo mzuri kwa chapat
Hivi ya kukandia chapati si ndo ile ya keki ya kukandia???
sijawahi kuulizia sh ngapi??
he he jamani sijakata tamaa jumapili nataka kupika tena chapati so farkhina nakutegemea tena ntapika live kila stage mutaipata