Ya Zuma na ANC kama Jakaya na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Zuma na ANC kama Jakaya na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JOYCE PAUL, Jul 17, 2011.

 1. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot]TAARIFA KWA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA ZIARA YA KISERIKALI NCHINI AFRIKA KUSINI,[/FONT]
  [FONT=&quot]TAREHE 18-21 JULAI 2011[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]1.0 UTANGULIZI[/FONT] [FONT=&quot]Kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mheshimiwa Jacob [/FONT][FONT=&quot]Gedleyihlekisa Zuma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atafanya ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini tarehe 18-21 Julai 2011. Hii itakuwa ni ziara ya kwanza ya kiserikali kufanywa na Rais wa Tanzania nchini Afrika Kusini. [/FONT] [FONT=&quot]Madhumuni [/FONT][FONT=&quot]ya ziara hii ni kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini katika nyanja zote na kutafuta maeneo mengine ya ushirikiano.[/FONT] [FONT=&quot]Katika ziara hii inatarajiwa kuwa, pamoja na mambo mengine, yatafanyika mazungumzo rasmi baina ya serikali mbili (bilateral talks), kutasainiwa mikataba mbali mbali ya ushirikiano na kutakuwepo na dhifa ya kitaifa kwa heshima ya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake.[/FONT] [FONT=&quot]Taarifa hii ina lengo la kuelezea masuala makubwa sita kama ifuatavyo:[/FONT] [FONT=&quot](i) [/FONT][FONT=&quot]Ratiba ya Ziara[/FONT] [FONT=&quot](ii) [/FONT][FONT=&quot] Hali ya Kisiasa, Kiusalama na Kiuchumi nchini Afrika Kusini[/FONT] [FONT=&quot](iii) [/FONT][FONT=&quot]Uhusiano wa Tanzania na Afrika Kusini (Bilateral Relations)[/FONT] [FONT=&quot](iv) [/FONT][FONT=&quot]Uanzishaji wa Tanzania-South Africa Bi-National Commission (BNC) na kutiwa saini kwa mikataba mingine ya kisekta[/FONT] [FONT=&quot](v) [/FONT][FONT=&quot] Masuala yanayohusu jumuiya ya Watanzania (Tanzanian Diaspora Community)[/FONT] [FONT=&quot](vi) [/FONT][FONT=&quot]Mkutano wa Wafanyabiashara (Tanzania-SA Business Forum)[/FONT] [FONT=&quot]RATIBA[/FONT] [FONT=&quot]Mheshimiwa Rais Kikwete anatarajiwa kuwasili alasiri ya tarehe 18 July 2011 na kufikia kwenye nyumba ya wageni wa Serikali iliyopo Waterkloof. Tarehe 19 Julai 2011 Mheshimiwa atapokelewa na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake na kufuatiwa na mazungumzo rasmi baina ya ujumbe wa nchi mbili hizi. Mazungumzo hayo yatafuatiwa na kutiwa saini kwa mikataba ya ushirikiano na mawaziri wanaohusika mbele ya waandishi wa habari. Waandishi wa habari wataruhusiwa kuwauliza MaRaisi maswali mawili kila mmoja.[/FONT] [FONT=&quot]Mheshimiwa Rais atakwenda kuweka shada la maua kwenye uwanja wa Uhuru na baada ya hapo atahudhuria kongamano la wafanyabiashara kwa chakula cha mchana.[/FONT] [FONT=&quot]Alasiri Makamu wa Rais wa Afrika ya Kusini, Mheshimiwa Kgalema Montlante atamtembelea Mheshimiwa Rais Kikwete kwenye makazi ya Serikali alikofikia na jioni hiyo ndipo kutakuwa na dhifa ya kiserikali kwa heshima ya Rais Kikwete.[/FONT] [FONT=&quot]Siku ya pili Mheshimiwa Rais atatembelea mji wa Cape Town ambapo atatembelea kisiwa cha Robben na mashamba ya zabibu na hatimaye jioni kurejea nyumbani Tanzania.[/FONT] [FONT=&quot]HALI YA KISIASA, KIUSALAMA NA KIUCHUMI AFRIKA KUSINI[/FONT] [FONT=&quot]2.1 [/FONT][FONT=&quot]HALI YA KISIASA[/FONT] [FONT=&quot]Kwa ujumla hali ya kisiasa nchini Afrika Kusini ni ya utulivu na utengamano. Hata hivyo, kuna masuala manne ambayo kwa sasa ndiyo yanatawala, ambayo niuchaguzi wa Serikali za Mitaa, misuguano ndani ya Chama Tawala na washirika wake yaani Shirika la Vyama vya Wafanyakazi (COSATU) na Chama cha Kikomunisti (SACP), maandamano na migomo dhidi ya huduma zisizoridhisha na taarifa juu ya njama za kumuondoa Rais Zuma kutoka katika nafasi yake ya Rais wa ANC.[/FONT] [FONT=&quot]3.1.1 Uchaguzi wa Serikali za Mitaa[/FONT] [FONT=&quot]Afrika Kusini ilifanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mnamo tarehe 18 Mei 2011. Uchaguzi huu ulikuwa na ushindani mkubwa kuliko chaguzi zote zilizopita. Ushindani mkubwa ulikuwa hasa kati ya vyama vya African [/FONT][FONT=&quot]National Congress ([/FONT][FONT=&quot]ANC) na Democtaric Alliance (DA).[/FONT] [FONT=&quot] Matokeo ya jumla ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi yaliipa ANC ushindi wa viti vingi zaidi, lakini Chama hicho cha upinzani katika manispaa zote kwa kupata asilimia 62 ya kura zilizopigwa ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2006 ambapo ilipata asilimia 67. [/FONT] [FONT=&quot]Kwa upande mwingine, chama kikuu cha upinzani cha DA kilipata asilimia 23.9 kutoka asilimia 14 ya mwaka 2006, huku kikiongoza katika jimbo la Western Cape na hivyo kufanikiwa kutawala Halmashauri ya jiji la Cape Town kwa kutoa Meya wakati huo kikiendelea kushikilia nafasi ya Waziri Mkuu wa jimbo hilo.[/FONT] [FONT=&quot]ANC ilipata jumla ya viti 5,633 vya udiwani na halmashauri 198 wakati DA ilipata viti 1,555 na halmashauri 18. ANC na DA vilifuatiwa na vyama vya Inkatha Freedom (IFP) na cha Congress of the People (COPE).[/FONT] [FONT=&quot]Uchaguzi huu ulishuhudia ongezeko la wapiga kura na kuweka rekodi tangu mwaka 1994. Asilimia 57.6 ya waliojiandikisha kupiga kura walijitokeza ikilinganishwa na asilimia 48 ya mwaka 2000 na 48.4 ya mwaka 2006.[/FONT] [FONT=&quot]Pamoja na kushinda kwa ujumla na kupata viti vingi tena, kushuka kwa ANC ikilinganishwa na matokeo ya uchaguzi uliopita wa mwaka 2006 kumeonekana dhahiri karibu katika miji yote mikubwa kama hivi (kwenye mabano ni asilimia ya kura ilizopata mwaka 2006): Johannesburg 58%(62%), Nelson Mandela Bay 51%(66%), Cape Town 32% (37%) na Tshwane 55% (56%).[/FONT] [FONT=&quot]Hali imekuwa tofauti kwa chama cha upinzani cha DA (Democratic Alliance) ambacho katika majimbo yote hayo, pamoja na kuwa nyuma ya ANC, kiliongeza idadi ya kura kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na mwaka 2006: Johannesburg 34%(mwaka 2006: 27%), Nelson Mandela Bay 40%(24%), Cape Town 60% (41%) na Tshwane 38% (30%). [/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]3.1.2 Misuguano ndani ya Chama Tawala na washirika wake[/FONT] [FONT=&quot]Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na misuguano na hali ya wasiwasi baina ya Chama Tawala (ANC) na washirika wake (tripartite alliance) ambao ni South African Communist Party (SACP) na Confederation of South African Trade Unions (COSATU). Aidha, misuguano hiii pia imeihusisha Jumuiya ya Vijana ya ANC (ANCYL) na hususan Rais wa Jumuiya hiyo Bw. Julius Malema.[/FONT] [FONT=&quot]Chanzo cha misuguano hii ni kutoridhika kwa vyama shiriki na ANC yaani SACP na COSATU kwa upande mmoja na ANCYL kwa upande mwingine juu ya hali ya kijamii na kiuchumi nchini Afrika Kusini. Washirika hawa wa ANC wamekuwa wakielezea wazi wazi juu ya kutoridhishwa na jinsi Serikali inavyoshughulikia matatizo makubwa ya nchi kama vile ukosefu wa ajira na umasikini uliokithiri hususan miongoni mwa wa Afrika Kusini weusi. [/FONT] [FONT=&quot]Itakumbukwa kuwa vyama vya SACP, COSATU na ANCYL vilikuwa mstari wa mbele katika kampeni iliyomuwezesha Rais Zuma kushinda kinyang’anyiro cha Rais wa ANC mwaka 2007 dhidi ya Rais wa wakati huu Bw. Thabo Mbeki. Washirika hawa walikuwa na matumaini makubwa kuwa uongozi wa Rais Zuma ungeleta mabadiliko makubwa na ya haraka katika maisha ya wananchi wa kawaida na kuwa Rais Zuma angefuata zaidi sera za mrango wa kushoto tofauti na mtangulizi wake alivyofanya kwani walikuwa wakimlaumu kwa kukumbatia sera za nguvu ya soko na kusahau hali ya wananchi masikini. Licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya sasa katika kuboresha hali ya maisha bado washirika hawa wanaona kuwa kasi ya mabadiliko haitoshi na hivyo kuzua malumbano na manung’uniko miongoni mwao. Ushirika huu umekuwa ukiilaumu Serikali kwa kufumbia macho tuhuma za rushwa dhidi ya baadhi ya viongozi.[/FONT] [FONT=&quot]3.1.3 Maandamano na Migomo[/FONT] [FONT=&quot]Katika siku za karibuni kumekuwepo na maandamano na migomo ya mara kwa mara vikiendeshwa na raia wa kawaida na vyama vya wafanyakazi nchi nzima kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kutoridhishwa na huduma za jamii. Maadamano na migomo hii mara kadhaa imekuwa ya shari kiasi cha kutokea mapambano baina ya waandamanaji na jeshi la Polisi na kusababisha majeruhi na hata vifo. [/FONT] [FONT=&quot]Mfano wa hivi karibuni kabisa ni wa mauaji ya muandamanaji mmoja (Bw. Andries Tatane) katika mji wa Ficksburg jimbo la Free State tarehe 13 Aprili 2011. Mauaji haya yamelaaniwa vikali na hata Rais Jacob Zuma mwenyewe. Polisi 6 waliohusika katika mauaji hayo wamekamatwa na kufunguliwa mashitaka. [/FONT] [FONT=&quot]3.1.4 Taarifa za njama za kumuengua Rais Jacob Zuma kutoka kwenye u-Rais wa ANC[/FONT] [FONT=&quot]Siku za karibuni vyombo vya habari viliripoti kuwepo kwa mpango wa kumuondoa Rais Zuma kutoka kwenye nafasi yake ya U-Rais wa ANC katika uchaguzi mkuu wa chama utakaofanyika mwishoni mwa mwaka kesho (2012). Taarifa hizo zilidai kuwa viongozi wa ngazi za juu wa ANC na Serikali wakiongozwa na Waziri wa Makazi, Bw. [/FONT][FONT=&quot]Tokyo Sexwale[/FONT][FONT=&quot] ndio wanaoandaa mpango huo. Wengine waliotajwa ni pamoja na Mwenyekiti wa ANC wa Jimbo la KwaZulu Natal, Bw. [/FONT][FONT=&quot]Zweli Mkhize[/FONT][FONT=&quot], [/FONT][FONT=&quot]Rais wa ANCYL, Bw. [/FONT][FONT=&quot]Julius Malema[/FONT][FONT=&quot],[/FONT][FONT=&quot] Mweka Hazina wa ANC, Bw. [/FONT][FONT=&quot]Mathews Phosa[/FONT][FONT=&quot] [/FONT][FONT=&quot]na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya ANC, ambao wengine pia ni Mawaziri kama vile Mabwana [/FONT][FONT=&quot]Jeff Radebe[/FONT][FONT=&quot],[/FONT][FONT=&quot]Fikile Mbalula[/FONT][FONT=&quot],[/FONT][FONT=&quot]Paul Mashatile[/FONT][FONT=&quot],[/FONT][FONT=&quot]David Mabuza[/FONT][FONT=&quot],[/FONT][FONT=&quot]Cassel Mathale[/FONT][FONT=&quot],[/FONT][FONT=&quot]Thandi Modise[/FONT][FONT=&quot],[/FONT][FONT=&quot]Enoch Godongwana[/FONT][FONT=&quot],[/FONT][FONT=&quot]Bathabile Dlamini[/FONT][FONT=&quot] [/FONT][FONT=&quot]na [/FONT][FONT=&quot]Tony Yengeni[/FONT][FONT=&quot].[/FONT] [FONT=&quot]Habari hizi zimekanushwa na watuhumiwa ambao miongoni mwao (mfano Bw. Tokyo Sexwale) wamemlaumu Rais Jacob Zuma kwa kutozungumzia suala hili kwa nia ya kukanusha kuwepo kwa njama hizo.[/FONT] [FONT=&quot]2.2 [/FONT][FONT=&quot]HALI YA KIUSALAMA[/FONT] [FONT=&quot]Hali ya usalama nchini Afrika ya Kusini kwa ujumla ni mbaya sana. Matukio ya uhalifu wa kutumia silaha majumbani, ofisini na sehemu za starehe na biashara ni ya kawaida sana. Aidha, kuvamiwa na majambazi barabarani nayo ni matukio ya kawaida mno.[/FONT] [FONT=&quot]Kinachoufanya uhalifu wa Afrika Kusini uwe wa kipekee na kutisha zaidi ni kwamba mara nyingi unaambatana na matendo ya kutishia maisha na ya ukatili kama vile kuua, kubaka na mateso mengine mengi. [/FONT] [FONT=&quot]Taarifa mbalimbali za kitafiti katika masuala ya uhalifu, zinaitaja Afrika ya Kusini kama taifa linaloongoza kwa uhalifu duniani ambalo haliko vitani. [/FONT] [FONT=&quot]Pamoja na kwamba matukio ya uhalifu yanahusu watu na makundi mbali mbali, katika siku za karibuni kumejitokeza wimbi la uhalifu unaolenga zaidi maafisa wa Balozi mbalimbali wanapokuwa maofisini, majumbani na hata barabarani wakiwa wanaendesha magari.[/FONT] [FONT=&quot]Hali hii mbaya ya usalama imeugusa pia Ubalozi na maafisa wa Ubalozi wetu ambapo katika miaka michache iliyopita yametokea zaidi ya matukio kumi yaliyowahusu likiwemo tukio baya zaidi la Desemba 2007 ambapo aliyekuwa Balozi, Mheshimiwa Emmanuel Mwambulukutu na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi walivamiwa na kuumizwa vibaya.[/FONT] [FONT=&quot]2.3 [/FONT][FONT=&quot]HALI YA KIUCHUMI[/FONT] [FONT=&quot]Hali ya kiuchumi ya Afrika Kusini inaridhisha. Afrika Kusini inaendelea kuwa ndilo Taifa lenye uchumi mkubwa kuliko nchi zote za Afrika ikiwa na GDP ya karibu USD Bilioni 290 na pato la wastani la USD 5,800 kwa mtu. Hii ni takribani robo ya uchumi wote wa Afrika na karibu 40% ya ukubwa wa uchumi wa Afrika chini ya Jangwa la Sahara. Afrika Kusini ni nchi ya 25 kwa utajiri duniani. Aidha, Afrika Kusini ina akiba ya fedha za kigeni na dhahabu ya kiasi cha USD Bilioni 45.52.[/FONT] [FONT=&quot]Sekta zinazoongoza katika kuchangia uchumi ni sekta ya huduma kama vile mabenki, bima, utalii n.k ikifuatiwa na viwanda na madini. Viwango vya sekta ya huduma vya Afrika Kusini ni vya hali ya juu sana kiasi kwamba Soko la Mitaji la Johannesburg ni miongoni mwa 15 bora zaidi duniani kwa maana ya “market capitalisation” na sekta ya mabenki iko katika sekta 10 bora zaidi duniani. Hali ya miundo mbinu nayo ni ya kisasa na iko katika viwango vya kimataifa.[/FONT] [FONT=&quot]Licha ya takwimu hizo za kuvutia, katika miaka ya karibuni Afrika Kusini kama zilivyo nchi nyingi duniani ilikumbwa na kutetereka kwa uchumi kutokana na kuyumba kwa uchumi duniani. Kutokana na sababu hiyo, Afrika kusini ilitangaza kuwa imeingia rasmi kwenye “recession” mwezi Mei 2009 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1992.[/FONT] [FONT=&quot]Pamoja na kwamba tayari Afrika Kusini imeondoka katika “recession” athari zilizotokana na kuyumba kwa uchumi bado zinaendelea kuonekana hususan katika ajira ambapo viwanda na sehemu nyingine za uzalishaji zililazimika kupunguza wafanyakazi kutokana na kupunguza uzalishaji uliosababishwa na kushuka kwa mahitaji kutoka kwa watumiaji wa bidhaa duniani. Ukosefu wa ajira kwa sasa ni asilimia 24.3 na hivi karibuni nchi hii ilitajwa kuwa ndiyo nchi yenye pengo kubwa kati ya matajiri na masikini ikiipiku Brazil. [/FONT] [FONT=&quot]Ili kukabiliana na changa moto za kukuza uchumi Serikali ilitangaza mpango mpya wa kukuza uchumi “New Growth Path”. Mpango huu unakusudia[/FONT] [FONT=&quot]4.0 [/FONT][FONT=&quot]UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI[/FONT] [FONT=&quot]Uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini umendelea kuwa mzuri hasa tangu Rais Jacob Zuma awe Rais wa ANC na baadaye Rais wa Nchi. Uhusiano huu umezidi kukua katika nyanja zote yaani kisiasa na kiuchumi (vitega uchumi, biashara na utalii).[/FONT] [FONT=&quot]4.1 Uhusiano wa Kisiasa[/FONT] [FONT=&quot]Serikali ya Rais Jacob Zuma na chama chake cha ANC wameonyesha kuwa na nia njema (good will) na Tanzania katika matamshi na vitendo vyao. Kwa mfano mara tu baada ya Rais Zuma kuchaguliwa kuwa Rais wa ANC alifanya ziara nchini Tanzania na katika ziara hiyo aliongozana na ujumbe mkubwa uliojumuisha viongozi karibu wote wa ngazi ya Juu wa ANC (i.e. wajumbe wa Sekretarieti). [/FONT] [FONT=&quot]Tuliambiwa wakati ule kuwa ujumbe ulioongozana na Rais Zuma nchini Tanzania ulikuwa ni mkubwa kuliko ilivyowahi kutokea kwa sababu Tanzania ni nchi muhimu sana katika mtizamo wa Rais Zuma. Wakati wa Ziara hiyo Rais Zuma ailitamka kuwa hakuna nchi yeyote inayoweza kudai kuwa ilitoa mchango mkubwa katika harakati za mapambano dhidi ya Ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini kuliko Tanzania. Hii ni kauli ya kwanza kutolewa hadharani na kiongozi yeyote wa Afrika Kusini.[/FONT] [FONT=&quot]Tangu wakati huo Rais Zuma amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Tanzania na alitoa mchango mkubwa katika kuiwezesha Tanzania kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa World Economic Forum on Africa uliofanyika nchini Tanzania mwaka jana. Rais Zuma binafsi na Mawaziri kadhaa kutoka Serikali yake walihudhuria siku zote za mkutano huo.[/FONT] [FONT=&quot]Tangu Rais Zuma awe Rais wa Afrika Kusini, Serikali yake imekuwa ikitaka kukuza zaidi mahusiano baina yake na Tanzania hususan kupitia Kamisheni ya Uchumi ya Marais (Presidential Economic Commission). Katika hili Serikali ya Afrika Kusini mara tatu walituma mwaliko kwa Tanzania kufanya mkutano wa Pili wa Kamisheni lakini hadi haikuwezekana kufanya hivyo kutokana na sababu za kutooana kwa ratiba za pande mbili. Aidha, ni kutokana na ‘initiatives” za serikali ya Afrika Kusini za kutaka kuimarisha zaidi uhusinao baina yake na Tanzania ndiyo maana ilipendekeza kuundwa kwa Bi-National Commission ambayo mkataba wake utasainiwa wakati wa ziara hii.[/FONT] [FONT=&quot]4.2 UHUSIANO WA KIUCHUMI[/FONT] [FONT=&quot]4.2.1 Vitega Uchumi[/FONT] [FONT=&quot]Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) hadi Desemba 2010 kulikuwa na makapuni 178 ya Afrika Kusini yaliyokuwa yamewekeza nchini Tanzania jumla ya mtaji wa USD 592.82 milioni na yakiwa yameajiri wafanyakazi 18,438.[/FONT] [FONT=&quot]Hivi sasa Afrika Kusini ni nchi ya saba katika kuwekeza nchini Tanzania na m[/FONT][FONT=&quot]akampuni yake yamewekeza katika takribani kila sekta ya uchumi kama vile mabenki (ABSA na STANBIC), mawasiliano (VODACOM), viwanda (ILLOVO na SABMiller), nishati (ENGEN na ORYX), mahoteli (SOUTHERN SUN na WHITESANDS HOTEL), ujenzi (GROUP FIVE), madini (TANZANITE ONE), maduka (SHOPRITE na GAME) n.k.[/FONT] [FONT=&quot]Miongoni mwa makampuni makubwa ya Afrika Kusini yaliyowekeza nchini Tanzania ni pamoja na: VODACOM, SABMiller, ABSA (NBC), Ilovo Sugar, Southern Sun Hotel, Silversands Hotel, Kwanza Bottlers, Engen, Oryx na Business Connexion. [/FONT][FONT=&quot][/FONT] [FONT=&quot]4.2.2 Uhusiano wa Kibiashara[/FONT] [FONT=&quot]Biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini imezidi kukua mwaka hadi mwaka ingawaje urari wa biashara umezidi kuwa hasi kwa upande wa Tanzania. [/FONT] [FONT=&quot]Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mwaka 2010 Tanzania iliuza nchini Afrika Kusini bidhaa zenye thamani ya USD milioni 433 na kununua kutoka Afrika Kusini bidhaa zenye thamani ya USD milioni 771 ikiwa ni hasi ya USD milioni 338 kwa upande wa Tanzania.[/FONT] [FONT=&quot]Hata hivyo takwimu hizi zinatofautiana kwa kiasi kikubwa na takwimu za Wizara ya Biashara na Viwanda ya Afrika Kusini ambazo zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2010 Tanzania iliuza nchini Afrika Kusini bidhaa zenye thamani ya USD milioni 69 na kununua kutoka Afrika ya Kusini bidhaa zenye thamani ya USD milioni 587 ikiwa ni hasi ya USD milioni 519. Kwa takwimu hizi inaonyesha Afrika Kusini inaiuzia Tanzania takribani mara tatu zaidi ya inavyonunua.[/FONT] [FONT=&quot]4.2.3 Utalii[/FONT] [FONT=&quot]Jitihada mbali mbali zinazofanywa na Ubalozi na Serikali kwa ujumla zimesaidia kufanya Tanzania izidi kujulikana nchini Afrika Kusini. Hali hii imewezesha idadi ya watalii kutoka Afrika Kusini kwenda Tanzania izidi kuongezeka kila mwaka. Idadi ya watalii wa Afrika ya Kusini imeongezeka kutoka watalii [/FONT][FONT=&quot]9,738 mwaka 1996 na kufikia watalii 28,721 mwaka 2008 kabla ya kushuka kidogo na kufikia watalii 25,586 mwaka 2009.[/FONT] [FONT=&quot]5.0 [/FONT][FONT=&quot]UANZISHAJI WA TANZANIA-SOUTH AFRICA BI-NATIONAL COMMISSION (BNC) NA KUTIWA SAINI KWA MIKATABA MINGINE YA KISEKTA[/FONT] [FONT=&quot]Inatarajiwa kuwa katika ziara hii ya Kiserikali, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Afrika Kusini watasaini mkataba wa makubaliano wa kuanzisha kamisheni ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili yaani “the Agreement Between the Government of the United Republic of Tanzania and the Government of the Republic of South Africa on the Establishment of the Bi-national Commission”[/FONT] [FONT=&quot]Mkataba huu ulipendekezwa na Serikali ya Afrika Kusini, ukajadiliwa na pande mbili kwa zaidi ya mwaka mmoja na hatimaye kukubaliwa. Mkataba huu utarithi mkataba mkuu wa ushirikiano baina ya nchi zetu mbili ambao ulitiwa saini tarehe 22 Septemba 2005 yaani “the Presidential Economic Commission”.Aidha, kutiwa saini kwa mkataba huu mpya kutafuta mkataba unaojulikana kama “the General Agreement on Economic, Scientific, Technical and Cultural Fields” uliotiwa saini tarehe 5 Oktoba 1995.[/FONT] [FONT=&quot]Tofauti kubwa kati ya Presidential Economic Commission (PEC) na Bi-National Commission (BNC) ni kuwa wakati PEC ilikuwa inashughulikia masuala ya uchumi tu na ilikuwa chini ya uratibu wa Wizara za Viwanda na Biashara za nchi mbili, BNC itakuwa na masuala karibu yote ya ushirikiano na itakuwa chini ya uratibu wa Wizara za Mambo ya Nje. Aidha. BNC itaunda kamisheni nyingine nne zitakoratiba ushirikiano katika Uchumi, Masuala ya Kijamii, Siasa pamoja na Ulinzi na Usalama.[/FONT] [FONT=&quot]Licha ya mkataba wa kuanzisha Bi-National Commission inatarajiwa kuwa katika ziara hii Mawaziri wanaohusika wa pande mbili watasaini mikataba mingine ya kisekta kama ifuatavyo:[/FONT] [FONT=&quot] i. [/FONT][FONT=&quot]Cooperation in the field of agriculture[/FONT] [FONT=&quot] ii. [/FONT][FONT=&quot]Cooperation in transport related matters[/FONT] [FONT=&quot] iii. [/FONT][FONT=&quot]Cooperation in Bilateral Air Services (BASA)[/FONT] [FONT=&quot] iv. [/FONT][FONT=&quot]Cooperation in mutual assistance between customs administration[/FONT] [FONT=&quot] v. [/FONT][FONT=&quot]Cooperation in the field of social evelopment[/FONT] [FONT=&quot] vi. [/FONT][FONT=&quot]Cooperation in water resources[/FONT] [FONT=&quot] vii. [/FONT][FONT=&quot] Cooperation in the field of arts and culture[/FONT] [FONT=&quot]6.0 [/FONT][FONT=&quot]USHIRIKIANO KATIKA MASUALA YA NJE, ULINZI NA USALAMA[/FONT] [FONT=&quot]Tanzania na Afrika ya Kusini ina mashirikiano mazuri katika nyanja masuala ya kimataifa, ulinzi na usalama hususan katika mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na jumuiya ya kikanda. Nchi hizi mbili kama ambavyo zilishirikiana wakati wa ukombozi zinashirikiana vizuri katika kulinda usalama wa mipaka ya nchi zetu kwa kuhakikisha usalama na hifadhi ya wananchi kwa kupambana na uhalifu wa kimataifa na biashara za mihadarati.[/FONT][FONT=&quot] [/FONT][FONT=&quot]Nchi hizi mbili pia zinashirikiana kutokana na tishio la uharamia katika bahari ya hindi nchi zetu. Mashirikiano haya yanajumuihsa kukabiliana na majanga mbalimbali. [/FONT] [FONT=&quot]7.0 [/FONT][FONT=&quot]DIASPORA COMMUNITY[/FONT] [FONT=&quot]Idadi kamili ya watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini haijulikani lakini inakisiwa kuwa ni wengi.[/FONT] [FONT=&quot]Watanzania hawa wamegawanywa katika makundi makuu matano:[/FONT] · [FONT=&quot]Wataalamu (professionals)[/FONT] · [FONT=&quot]Wanafunzi[/FONT] · [FONT=&quot]Wafanyabiashara wadogo wadogo[/FONT] · [FONT=&quot]Wazamiaji (stowaways)[/FONT] · [FONT=&quot]Wafungwa [/FONT] [FONT=&quot]Wataalamu (professionals)[/FONT] [FONT=&quot]Kwa upande wa wataalum, kuna watanzania wengi ambao ni wakufunzi/wahadhiri wa vyuo vikuu, madaktari wa tiba na wataalamu wengine wanaofanya kazi serikalini na katika mashirika na makampuni ya serikali na sekta binafsi katika nyanja mbali mbali.[/FONT] [FONT=&quot]Wengi wa watanzania hawa wanafanya kazi nzuri sana na kulitukuza jina la Tanzania kwani wameonyesha ueledi wa hali ya juu na kutunikiwa nishani za aina mbali mbali. [/FONT] [FONT=&quot]Wanafunzi[/FONT] [FONT=&quot]Idadi ya wanafunzi wa kitanzania wanaosoma nchini Afrika Kusini inakadiriwa kuwa zaidi ya 1,000. Wanafunzi hawa wako katika ngazi mbali mbali za elimu yaani kuanzia na shule za awali, shule za msingi, shule za sekondari hadi vyuo vya elimu ya juu.[/FONT] [FONT=&quot]Hivi sasa karibu kila chuo kikuu cha Afrika Kusini kina wanafunzi wa Kitanzania wanaochukua shahada za kwanza na zile za uzamili. Vyuo vinavyoongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi wa aina hiyo ni Univesrity of Cape Town, University of Pretoria, University of Western Cape, Univesity of Witswatersrand, University of South Africa, Univesity of KwaZulu Natal, Tshwane Univesity of Technology, University of Monash, University of Stellenbosch, University of North West na University of Johannesburg. [/FONT] [FONT=&quot]Wafanya Biashara wadogo wadogo [/FONT] [FONT=&quot]Wapo vijana wengi wa Kitanzania wamekuja hapa nchini na kuanza kijishughulisha na biashara ndogo ndogo. Hawa wamesambaa nchi nzima. Wengi wao wamekuwa wakifanya biashara kinyume cha sheria na hivyo wamekuwa wakikabiliana na vyombo vya dola na hata wakati mwingine wamekuwa wakirejeshwa nyumbani. [/FONT] [FONT=&quot]Wazamiaji [/FONT] [FONT=&quot]Kuna idadi kubwa ya wazamiaji wa kitanzania nchini Afrika kusini kiasi kwamba kwa wastani kila mwezi idadi ya wazamiaji 50 wanarudishwa nyumbani na Serikali ya Afrika Kusini baada ya kukamatwa na kutambuliwa na Ubalozi. Aidha, kwa wastani Ubalozi unatoa Hati za Dharuara za Kusafiria (ETD) 100 kila mwezi kwa watanzania wanaoishi Afrika Kusini wanaotaka kurudi nyumbani lakini hawana hati za kusafiria.[/FONT] [FONT=&quot]Katika kundi la wazamiaji kuna watanzania kadhaa ambao “wamejilipua” kwa kujisajili hapa Afrika Kusini kama wakimbizi wa Kirundi na Kisomalia. Hata hivyo, watanzania hawa wanapopata matatizo wanatarajia Ubalozi uwasaidie.[/FONT] [FONT=&quot]Wafungwa [/FONT][FONT=&quot][/FONT] [FONT=&quot]Wapo Watanzania wanotumikia vifungo mbali mbali hapa nchini. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara inayoshughulikia wafungwa nchini mwaka 2009 kuna Watanzania wapatao 300 wanaotumikia vifungo magerezani. Wengi wao wamefungwa kutokana na makosa mbali mbali hasa yale ya wizi, madawa ya kulevya, kugushi nyaraka, kupigana. [/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]8.0 [/FONT][FONT=&quot]MKUTANO WA WAFANYABIASHARA (TANZANIA-SOUTH AFRICA BUSINESS FORUM)[/FONT] [FONT=&quot]Ubalozi kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara na Viwanda ya Afrika Kusini umeandaa mkutano wa wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini utakaofanyika wakati wa ziara hii ya kiserikali, tarehe 19 Julai 2011. Wakati Ubalozi ndio uliotoa wazo la kuafanyika kwa mkutano huu, Wizara ya Biashara na Viwanda ya Serikali ya Afrika Kusini itabeba gharama zote za mkutano huu.[/FONT] [FONT=&quot]Mkutano huu utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Royal Elephant Hotel, Centurion, Pretoria utawakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wa Afrika Kusini.[/FONT] [FONT=&quot]Washiriki kutoka Tanzania wanatoka katika makundi mawili makubwa ambayo ni taasisi za Kiserikali na sekta binafsi. Baadhi ya taasisi za kiserikali zitakazoshiriki ni: Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na uwezeshaji), Wizara ya Viwanda na Biashara, TIC, NDC, SUMA-JKT, TPA, TTB, TNBC, kwa upande wa sekta binafsi kuna washiriki kutoka maeneo mbalimbali. [/FONT] [FONT=&quot]Sekta zilizopewa kipaumbele katika mkutano huu ni pamoja na kilimo na mifugo, miundo mbinu, utalii, nishati na madini na mawasiliano.[/FONT] [FONT=&quot]Inatarajiwa kuwa Waheshimiwa Ma-Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Jacob Zuma watashiriki katika mkutano huu wakati wa mchana (saa 7.00) kwa kuzungumza na washiriki na kula nao chakula cha mchana.[/FONT] [FONT=&quot]9.0 [/FONT][FONT=&quot]HITIMISHO/MAPENDEKEZO[/FONT] [FONT=&quot]Ziara hii ni fursa ya maalum kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na Afrika ya kusini hasa kwa kuwa mashirikiano ya nchi mbili hizi ni ya kina na ya muda mrefu. Afrika ya Kusini imepiga hatua kubwa kiteknologia na kisayansi ambapo Tanzania inaweza kufaidika nayo. Tayari kuna makampuni makubwa ama yanafanya biashara Tanzania au yanakusudia kufanya hivyo, kwa sababu hiyo kuna haja ya kuwa na wataalam waliopata mafunzo hapa. Ingekuwa vema tukawa na mfumo rasmi wa mafunzo kwa watanzania ili kutumia maendeleo hayo ya kisayansi na kiteknologia kuendeleza nchi yetu. [/FONT] [FONT=&quot]Ungeundwa mfuko wa elimu maalum (strategic studies) ambapo Tanzania itagharamia nauli na wakati Serikali ya Afrika ya Kusini igharamie mafunzo. Washiriki wa mafanzo hayo wawe in wataalam wa kuendeleza mashirikiano tunayotaka toka Afrika ya Kusini. Tayari Wizara kadhaa za nchi hii ikiwemo Wizara za Mambo ya Nje, Wizara ya Ulinzi na Usalama wanatoa nafasi kadhaa za mafunzo. Ingekuwa vyema kuwa na utaratibu rasmi. Mheshimiwa Rais ikiridhiwa na pendekezo hili anaweza kuligusia wakati wa mazungumzo ya faragha ili lifanyiwe kazi.[/FONT] [FONT=&quot]Afrika ya Kusini ingependa kushirikiana na Tanzania katika kuhifadhi historia ya ukombozi. Mheshimiwa Rais amhakikishie mwenyeji wake kuwa Tanzania iko tayari kuendeleza azma hiyo ambayo ni muhimu kwetu pia.[/FONT] [FONT=&quot]Ikimpendeza Mheshimiwa Rais angetumia fursa hii naye kumualika mwenyeji wake Mheshimiwa Rais Zuma kutembelea Tanzania mapema mwakani. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]IMETAYARISHWA NA UBALOZI WA TANZANIA,[/FONT]
  [FONT=&quot]PRETORIA, AFRIKA KUSINI, JULAI 2011[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Hiyo mikataba ndo inayotumaliza kabisa, coz inasainiwa bila kufanyiwa upembuzi wowote.
   
Loading...