justo james
Member
- Apr 29, 2011
- 7
- 0
Habari ya leo wana JF wenzangu, najua kwa sasa macho yote ya watz yapo kwenye suala la posho na tumesahau kabisa kuhusu mkwara aliowachimba DK. Slaa na Mch. Mtikila, ninachojiuliza ni mbona alitoa siku saba na kwamba wasipomuomba msamaha atakwenda mahakamani, mpaka leo siku saba hazijafika au? Mpaka leo sijaona yeyote kati ya hao akiomba msamaha wala Ridhiwani akienda mahakamani kuwashitaki. Inaonyesha walichosema ni ukweli mtupu. Nakumbuka Dk. Slaa alimwambia utakuwa umevunja rekodi ya mafisadi waliosema watatupeleka mahakamani wakaishia kukaa kimya. So nazidi kuiamini CDM kwamba hawakurupuki katika habari wanazowapa watz, wanajipanga kwanza na wanahakikisha kuwa data ni za kweli kisha wanazirusha hewani.