fakhbros
JF-Expert Member
- Sep 14, 2013
- 382
- 654
Nimezaliwa miaka 38 iliyopita katika kijiji cha Ruzinga Zamani ikiitwa kata Buyango
Wakati huo halikuwepo jimbo la nkenge wala wilaya ya Misenyi maeneo haya yalikuwa katika wilaya ya Bukoba vijijini
Wakati nakuwa nikiwa na umri wa miaka mitano nilijumuika sana na vijana wenzangu katika michezo ambayo iliendana na umri wetu
Hatukucheza mpira sababu haukuwa utamaduni wetu
Pia hatukujua kutengeneza manati kwa sababu kila mmoja aliiheshimu baiskeli ya nyumbani kwao
Enzi hizo palikuwa na Baiskeli aina ya swala, na familia tajiri ilikuwa inamiliki baiskeli aina ya phonex
Nakumbuka wakati huo pale kijijini nyumbani kwetu ndio palikuwa na Redio kila siku ya jumapili rafiki zake na baba walikusanyika pale nyumbani na baba aliwawekea music wote siku hiyo wangekesha pale
Baba alikuwa na aina nyingine ya kifaa cha music ambacho kiliitwa santuli hii santury iliwekewa sindano baada ya kupachikwa CD yake kisha ilipokuwa inazunguka mziki mzuri ulisikika kutoka mle ndani ya santuli
Baada ya kuanza primary pale Ruzinga primary school nilitamani sana kujua kuandika barua kwa maana wakati ule aliejua kuandika ndie alikuwa anauza duka la kijiji kila mmoja alimheshimu sana pale kijijini kutokana na hiyo Kazi yake
Nakumbuka pale tulipokuwa shuleni walimu walikuwa wakituambia kuwachanjia kuni na wasichana walipangiwa Kazi yakuwachotea maji walimu hasa wale ambao waliishi maeneo ya shule
Hatukujari kufanya Kazi hizo na hata wazazi waliona ufahari sisi kuwafanyia Kazi walimu
Nakumbuka siku nilipokuwa darasa la tano nilimuandikia barua ya mapenzi msichana ambae nilikuwa nampenda jina lake akiitwa Janeth
Niliandika hivi:
John Lupia mugisha
S.L.P 25 RUZINGA
Bukoba
Barua kwa Mpenzi wangu
Janeth'
Kwanza kabisa salam, Ama baada ya salam nataraji haujambo na mzima wa afya
Janeth tambua mungu alipo amua kuumba mbingu alijua kuwa lazima kuwepo kiumbe kitakacho ipoza pindi itakapokuwa imechemka kutokana na joto la jua,
Janeth napenda kukufahamisha kuwa mwenzio moyo wangu umekufa nakuoza juu yako
Napenda ulivyo, hasa midomo yako iliyochongoka kwa mpangilio kama karatasi za daftari la hisabati
Kila nikuonapo unanifanya kukosa raha kwa jinsi ninavyokupenda, Nakuomba unikubalie ili niweze kuwa Mpenzi wako
Endapo utakubali ombi langu sintokuandika tena pale utakapo piga kelele darasani kama ujuavyo Mimi ndio monitor wa darasa letu
Janeth amini barua hii nimeiandika kwako ili kukuonyesha jinsi ninavyo kupenda ukinikukubalia ombi langu tukitoka darasani nitakupatia zawadi ya Kabaraghara..
Ni Mimi akupendae
Hii barua ilikuja kupelekwa kwa mwalimu mkuu na Janeth hatimae nilichapwa viboko 22 na kuondolewa katika nafasi ya umonitar wa darasa
Lakini sikukata tamaa baada ya kufika darasa la saba Janeth alikubali ombi langu la darasa la tano na siku ya graduation ya kuhitimu std seven Janeth na Mimi tulikesha nyumbani kwa shangazi
Hakika ya kale ni dhahabu hata kama ni feki...
Vipi wewe na Janeth wako unakumbuka nini?