CCM imejaa wasanii na wahuni. Masha alipoitwa kuja kushughulikia swala la Bashe, alipoulizwa kuhusu swala hilo, aliwajibu waandishi wa habari kwamba swala la uraia wa Bashe halina utata. Walipotaka afanunue alimaanisha nini, alikwepa swali na kurudia kusema swala hilo halina utata. Hapo aliwaacha solemba waandishi wakiwa hawajui kwamba Masha anakubaliana na CCM au anakubaliana Idara ya Uhamiaji?
Ninashangaa kusoma barua hiyo akisema kwamba Bashe ni Raia halali wa Tanzania. Kwanini hakutoa firm statement kama hiyo tangu siku ya kwanza alipoulizwa?
Conclusion ni moja, Kikwete, Kamati ya Maadili, CC na Masha mwenyewe, wote walijua nini kilikuwa kinaendelea. Kwa kifupi Bashe hakuwa anatakiwa na ili kummaliza kabisa, makatibu wote wa matawi waliokuwa wanamuunga mkono wakati wa kura za maoni, some of them wamehamishwa na wengine kutishiwa kwamba Kigwangala asiposhinda watashughulikiwa.
On the other hand, Bashe mwenyewe ameishaanza kusukuma tuhuma kwa viongozi wake wa Mkoa kwamba ndo walimpikia majungu. Lakini hajui hizo tuhuma zilizopikwa zilianzia wapi au malengo yake yalikuwa ni nini. Inawezekana anaweza kuwa anakwepa more msuguano na UVCCM, Riz1, na Mkulu. Sasa ili abaki salama inabidi atafute mchawi mwingine, maana hawa waliomroga (Riz1 na Malisa) hana ubavu nao na amegundua kwamba alicheza na moto, na akiendelea kucheza nao utamuunguza zaidi na kummaliza kabisa.
Hata kama atabaki CCM bado hawezi kuwa na nguvu kama aliyokuwa amejikusanyia, ataanza kuogopwa na hivi amejiweka mbali na Kampeni ndio anajipalia makaa zaidi. Aangalie ustaraab wa kujiunga na chama kingine, vinginevyo ndoto ya una siasa ndo inaweza kuwa imeota mbawa.
Ndiyo CCM hiyo bana .... ina wenyewe!