Juma wa Juma
Senior Member
- Jan 13, 2017
- 150
- 221
TAARIFA KWA UMMA .
THE CIVIC UNITED FRONT - CUF.
OFISI YA WILAYA - UBUNGO .
KURUGENZI YA HABARI , UENEZI , MAHUSIANO NA UMMA .
Chama Cha Wananchi Ofisi Ya Wilaya Ya Ubungo kimesikitishwa na Kile Kilicho Ripotiwa Kutokea Jana Kwenye Hotel Ya VINA Maeneo Ya Mabibo Dar - es -salaam , ambapo Imeripotiwa Kuvamiwa Kwa Mkutano Uliodaiwa Kuwa ni Wa Chama Cha Wananchi - CUF Kwenye Wilaya ya Kinondoni Jambo ambalo Si Kweli .
Ukweli ni Kwamba Chama Chetu kinazo Ngazi Zake za Uongozi Kuanzia Tawi , Kata , Wilaya na Taifa Kwa Bahati Mbaya Kikao hicho Cha Jana Hakikuwa Cha Ngazi Yoyote ya Chama Cha Wananchi - CUF katika hizo nilizozitaja hapo Juu. Pia eneo hilo la Mabibo Kwa Sasa Liko Chini Ya Wilaya Mpya Ya Ubungo ambayo Chama Cha Wananchi - CUF Kimeshaunda Uongozi Wa Kukaimu Kwa Kipindi Cha Miezi Sita Ya Kuelekea Uchaguzi Kamili wa Wilaya hiyo Mpya ambao Pia haukuwa na taarifa ya Kikao hicho Cha Jana.
Uongozi wa Chama Cha Wananchi - CUF Wilaya ya UBUNGO Umesitushwa na Kushangazwa na Kitendo Cha Mwenyekiti Wa Chama Cha Wananchi Wilaya Ya Kinondoni Kuitisha Kikao Katika Eneo la Wilaya Ya UBUNGO Bila Kutoa Taarifa Kwa Kiongozi Yoyote Wa Wilaya Zote Mbili Za UBUNGO na KINONDONI .
Jambo ambalo Wilaya Zote Mbili Kwa Pamoja Zilishalitolea Tamko Katika Taarifa Yake Kwa Vyombo Vya Habari Iliyoyolewa Kwenye Ofisi ya Wilaya ya Kinondoni Tar. 17/April/2017 Kuwa Ni Marufuku Vikao Vya aina hiyo ambavyo Havina Taarifa Kwenye Ngazi za Chama na Vinavyokiuka Katiba ya Chama Cha Wananchi.
Kikao Kilichofanyika Jana Kwenye Hoteli ya VINA Kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Wilaya Ya Kinondoni Ndg Juma Nkumbi , Lakini Pia Kilihudhuliwa Kwa Kiwango Kikubwa na Wanachama Wa Chadema ambao Waliletwa Ukumbini hapo Kwa Makundi Kutokea Maeneo Mbali Mbali ya Dar - es - salaama toka Majira ya Saa Tano za Asubuhi.
Jambo la Kusikitisha Kwa Mwenyekiti huyo Wa Wilaya ya Kinondoni ni Pale alipoacha Eneo lake la Kiutawala la Kinondoni na Kuamua Kuitisha Mkutano huo wa Waandishi Wa Habari Nje ya Eneo lake Wakati Wilaya ya Kinondoni Chama Cha Wananchi - CUF Kinazo Ofisi zake Yenyewe na Siyo za Kupangisha , Lakini Nkumbi ameshindwa Kufika Ofisini Kwake kwa Zaidi ya Miezi nane Sasa na hatimaye anaamua Kuendesha Shughuli za Chama Nje na Eneo lake la Kazi.
Kwa hili la Kufanya Shughuli za Kiwilaya Kwa Kushirikiana na Watu ambao Si Viongozi Wa Wilaya ya Kinondoni.
Yako Maswali Mengi Ya Kujiuliza : Mwenyekiti huyo alishindwa nini Kuitisha Kikao hicho Kwenye Ofisi za Chama Kama alivyofanya Katibu wake Ndg .Mohammed Mkandu Tar 17/04/2017 ?
(2) Alikuwa Wapi Siku Zote hizo Kiasi Cha Kusababisha Mambo Mbali Mbali yanatendeka huku Yeye akiwa kama Mwenyekiti wa Wilaya hana Habari ?
Mfano : Mkutano wa Wilaya Zote Mbili Uliofanyika Ofisini kwa Nkumbi ( Ofisi za CUF Wilaya ya Kinondoni ) Ulihusisha Viongozi wa Wilaya ya Ubungo ambao Yeye Nkumbi anadai Kutowatambua Bila Kujali Kama anayo Mamlaka Kwa Mujibu Wa Katiba Yetu au hana .
Chama Cha Wananchi Wilaya ya Ubungo Kinamtaka Kiongozi huyo Kukaa Kimya na Kuacha Kuvuruga Shughuli za Chama Chetu Kwenye Wilaya hiyo , Pia Kinamuonya Kuendelea Kuitisha Vikao Vya aina hiyo Kwenye Wilaya yetu na Endapo atakaidi Katazo hilo Hatutasita Kuuzuia Mkutano huo Kwa Nguvu zetu.
Pia tunasikitishwa na Kitendo Cha Kuguswa Kwa namna Yoyote au Kujeruhiwa kwa Mwandishi wa Habari au Yoyote ambaye Si Muhusika wa Tukio hilo Kwa Kuwa Chama Chetu Kipo Kwa ajili Ya Kuhakikisha amani ya Tanzania Inatunzwa na Inadumishwa Pia Usalama wa Wanahabari Mahala Pao pa Kazi Unadumishwa .
Tutumie Fursa hii Kuwaomba Radhi Wanahabari na Kuwaomba Radhi Wale Wote Waliokwazika na Kuchukizwa na Tukio hili Kwa namna Moja ama Nyingine na Kuwaomba Waendelee Kukiiamini na Kushirikiana na Chama Chetu The Civic United Front - CUF ( Chama Cha Wananchi )
HAKI SAWA KWA WOTE.
Salum Hussain Chilwa.
Mkurugenzi Habari , Uenezi Mahusiano na Umma.
CUF - Wilaya ya Ubungo.
Imetolewa Leo Tar 23/04/2017