Ya balozi Mwapachu na unafiki wa UVCCM

Chigwiye misi

Member
May 31, 2012
74
41
Wasalaam wanabodi,
Nianze kwa kutoa masikitiko yangu yenye pongezi ndani yake(nasikitika na kupongeza) kwa balozi Juma Mwapachu kwa kitendo chake cha kuamua kutuonesha watanzania haswa vijana rangi halisi za hawa wazee wetu ambao wakati mwingine tunajenga ufuasi kwao pasi kuwafahamu kiundani wakoje,eti ndani ya nusu mwaka mwandiplomasia huyu ameshauona ubaya na uzuri wa CCM,ubaya na uzuri wa ukawa,ubaya na uzuri wa magufuri na ubaya na uzuri wa lowasa!huyo ndiye mwapachu mtanga kunani,
Niendelee na bandiko langu,mwapachu katoka na kurudi kwenye chama chake,wakaja UVCCM na unafiki wa hali ya juu haswa,UVCCM wakaja na matamko uchwara yaliyobeba kile kinachoitwa eti mwapachu asipokelewe "msaliti" huyu!
Ebo!mwapachu pamoja na kukosa dira kwake,kwangu mimi huyu ni bora kuliko hawa UVCCM matamko,hivi UVCCM chini ya sadifa Juma hamis na shaka hamud shaka ninyi kwenu msaliti ni mwapachu tu?Mbona hatujasikia matamko na pengine hata kuwachukulia hatua vijana waliomtukana mgombea wenu wa urais ambaye kwa sasa ni rais ndg magufuri,imekuwaje yule mwanamama aliyekuwa katibu wa uvccm pale arusha aitwae mwajuma rashid ambaye alimtukana wazi wazi magu leo mmemkumbatia ofisini?uvccm chini ya sadifa na shaka wanajua fika kua mwajuma rashid ndiye aliyekuwa akiwahujumu kwa kueneza propaganda ovu kwa vijana wa arusha kuwa wasihudhurie mikutano ya mgombea wa ccm wa wakati huo ndg magu kwa kile alichowaambia vijana hao kua wajifunze kupenda "chao"(bila shaka alimaanisha vijana wa ccm arusha wakae mlengo wa lowasa na ukawa),ndani ya uvccm ya sadifa na shaka hakuna asiyejua kuwa mwajuma ndiye alikuwa akivujisha siri za ccm mkoa wa arusha kwa kambi ya lowasa,lakini leo kwa sababu ya kuendelea kuwepo kwenye payroll ya lowasa uvccm makao makuu wamekaidi mpaka maagizo ya chama yaliyoelekeza kuwa mwajuma awekwe kando na asijihusishe na masuala yoyote ya jumuiya na chama kwa ujumla(afukuzwe),lakini mpaka bandiko hili linakuja hapa mwajuma yupo makao makuu ya uvccm na anaingia vikao vyote nyeti vya uvccm!huku akiwa na kinga ya kutoguswa toka kwa shaka hamud shaka,kuna usaliti gani zaidi ya huu?
Jumuiya inanuka rushwa na wizi usiomithilika(kuna siku nitaleta bandiko hapa juu hili la wizi na rushwa),kuna usaliti zaidi ya huu?hivi kati ya mwapachu na hawa uvccm nani msaliti haswa?
Kama nia yenu ni kuondoa wasaliti iweje wakuu wa idara za uvccm wameendelea kuchukua fedha kwa edward lowasa na kuzitumia kujiandaa na uchaguzi wa 2017?
Kuna usaliti gani zaidi ya huu?nauliza kuna usaliti gani zaidi ya ule wa Kaimu katibu mkuu na rafiki yake mkuu wa idara ya utawala kuendelea kulamba miguu ya lowasa kila uchao ili mpewe fungu la kufanikisha kile mlichokiita mkakati wa kuendeleza mtandao wa lowasa ndani ya uvccm na ccm kwa ujumla?
Ushauri wangu kwa uvccm kama mnataka na mnapenda kina mwapachu wasipokelewe kwa kigezo cha usaliti,anzeni kwanza kuwafukuza wasaliti mlionao ndani ambao wanafahamika kwa sura,majina na nyendo zao.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom