Ya Arusha Na 'Mazungumzo Baada Ya Habari' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Arusha Na 'Mazungumzo Baada Ya Habari'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jan 17, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,  ZAMANI kwenye Radio Tanzania, moja ya vipindi maarufu kilikuwa ’ Mazungumzo Baada Ya Habari’. Ni moja ya nyenzo za Serikali kufikisha ujumbe kusudiwa kwa umma. Ni kupitia mazungumzo yale ya dakika tano yalioandaliwa kwa umakini mkubwa, umma uliweza, mathalan, kufahamishwa ni nani adui wa umma na hitimisho la nini cha kufanywa. Hizo zilikuwa kazi za makada ’ waliokunywa maji ya bendera!’. Unazungumzia majina kama akina Paul Sozigwa na David Wakati. Ni akina Paul Sozigwa, waliowafanya, watoto wa wakati huo, waamini , kuwa Idi Amin alikuwa aina ya nyoka!

  Wakati umebadilika. Yaliyotokea Arusha ni kielelezo cha wakati uliobadilika. Siku mbili hizi, kwenye runinga na redio tunaona na kusikia kinachofanana na Mazungumzo Baada ya Habari ya enzi za akina Paul Sozigwa. Hapa wapanga mikakati wanakosea.


  Tanzania ya miaka 1970 si ya 2011. Ndio maana ya umuhimu wa kubadilika na kwenda na wakati. Kwa dola, kuna wakati inahitaji kuonyesha ukali, na kuna wakati inatakiwa ionyeshe upole. Kwa kilichotokea Arusha na jinsi Watanzania na dunia walivyoipokea habari ile ya raia wasio na silaha kuawa kwa risasi za moto na wengine kujeruhiwa, basi, dola inatakiwa kutambua mapungufu yaliyotokea. Kwa namna yake, kama alivyofanya Mh. Rais, kuonyesha masikitiko yake na kutoa matumaini ya baadae, kuwa jambo hilo laweza kuwa ni historia.


  Lakini, tatizo la nchi zetu hizi ni kuongozwa na vyama dola. Hili la Arusha limefanywa kuwa siasa zaidi. Na hapa hakuna cha udini bali udini unaoingizwa na wanasiasa kwenye siasa kwa maslahi ya kisiasa.  Na kinachojitokeza sasa ni mapambano ya kutamfuta mshindi. Hapa sasa anatafutwa nani zaidi kati ya CCM na CHADEMA? Jibu ni jepesi. Hakuna aliye zaidi. Ndio, hakuna mshindi. Kwa kilichotokea Arusha, kama nchi ,tumeshindwa. Jumuiya ya Kimataifa inatushangaa,siye tuliopigiwa mfano sasa tunafanana na tunaanza kuachwa na hao walioambiwa waige mfano wetu.


  Katika nchi zetu hizi mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi ya kisiasa badala ya kitaifa. Kule Arusha tumewasikia Dr Slaa na Ndesamburo (CHADEMA) wakitoa kauli za kuchochea hamasa za wafuasi wao. Walipaswa, wakiwa majukwaani, kuwa makini zaidi katika kuchagua na kuchambua kauli zao.


  Na kule Arusha tumewasikia pia akina Makamba na Chatanda ( CCM). Walipaswa pia kuchagua na kuchambua kwa makini kauli zao. Kwa kilichotokea Arusha si CHADEMA inayojitafutia umaarufu, bali ni CCM inayoipa umaarufu CHADEMA. Ni kwa maamuzi kama yale ya kuzuia maandaamano na kauli kama zile za akina Makamba na Chatanda ndizo zinazoisaidia CHADEMA kupanda chati kitaifa na hata Kimataifa.


  Na hakika, ni CCM itakayoifanya amani ya nchi yetu ishamiri. Na ni CCM hiyo hiyo itakayoifanya amani ya nchi yetu iporomoke. Nimepata kuandika, kuwa CCM, baada ya uchaguzi wa mwaka huu, ina jukumu la kuongoza mchakato wa mabadiliko ilikiwamo mabadiliko makubwa ya Katiba. Ukiangalia kilichotokea Arusha, unayaona mapungufu ya Kikatiba yaliyopelekea utaratibu na usimamizi wa uchaguzi wa Umeya ujengeke katika mazingira ya kutoaminiana na hatimaye maandamano na polisi kuingia kwenye vurugu na waandamanaji.


  Dalili za kuwepo kwa sintofahamu na vurugu zilionekana mapema. Edward Lowassa, pamoja na yote tunayomwandika, lakini, katika hili la Arusha ndiye mwanasiasa, kwa mtazamo wangu, aliyeonyesha na anayeendelea kuonyesha ukomavu wa hali ya juu katika kipindi hiki cha malumbano ya kisiasa. Kwa la Arusha, Lowassa ameonyesha uwezo wa kusoma alama za nyakati.


  Lowassa aliona kile ambacho kingetokea. Akasema hadharani: Kuwa Arusha inaelekea kuwa Ivory Coast, pande zinazohusika zimalize tofauti zao kwa mazungumzo. Ndani ya chama chake kuna waliombeza.Sikushangaa.


  Kwa kuhitimisha. Watanzania tutambue ukweli, kuwa demokrasia yetu bado changa. Tumefanya chaguzi zenye walakini mwingi, ni sehemu ya kujifunza. Na sasa tuna fursa ya kuandaa Katiba itakayotufanya tujenge misingi imara ya demokrasia yetu.


  CHADEMA iukubali ukweli, kuwa Uchaguzi uliopita umeshapita. Kwamba Serikali iliyo madarakani kwa sasa ndio hiyo inayoongozwa na JK kama Rais. Hatuna Rais mwingine. Hatuna Serikali nyingine.


  Na CCM nayo iukubali ukweli, kuwa wakati umebadilika na kuwa wananchi wanaukubali upinzani. Na kwamba kwa sasa, CHADEMA ndio chama kikuu cha upinzani kikifuatiwa na CUF. Vyama hivi na vingine vyenye uwakilishi bungeni, vina lazima ya kushirikiana katika mambo ya msingi na yenye maslahi kwa taifa letu.


  Hizi si zama za Mazungumzumzo Baada Ya Habari, bali, Mazungumzo Kabla na Baada Ya Habari, kwa kutanguliza maslahi ya nchi tuliyozaliwa.
  Maggid
  Dar es Salaam
  17, Januari, 2011
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Majjid mimi nakuunga mkono kwa 100% makala yako imetulia na ulikiandika ndio ukweli wenyewe, wala ukutaka kuufurahisha upande wowote ulichokifanya ni kuangalia Tanzania kwanza vyama baadae.
  Swali: sina mashaka yoyote na upeo wako mkubwa, lakini bado najiuliza, na swali hili sitaki alijibu mchangiaji mwingine bali wewe mwenyewe, hivi ukifika wakati wa uchaguzi akili zenu huwa mnakwenda kuzifungia kwenye stoo gani? maana uchaguzi ukiisha naona akili zenu mnakuwa mmezirudisha vichwani mnakuwa waandishi wenye weredi, kama tatizo ni pesa mseme ili tuwaanzishie mfuko wa kuwasaidi waandishi huru ili muache kufanywa kama condom! nasubili ufafanuzi wa hili, nitarudi kwenye topic.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mpeleee uliyemwingiza madarakani na kumtetea! Au si mwelewa! Mimi bado nasisitiza raisi wangu ni dr slaa nasubili lolote aniambie nifanye ntafanya tuu!
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  Matola asante sana kwa swali lako na mimi nilitaka kuuliza hivi huyu si yule Maggdi wa wakati wa uchaguzi kama tatizo lake ni pesa basi tatizo hilo hilo analoliona kwa wanasiasa na yeye analo aanze kwanza yeye mwenyewe kujirekebisha. Otherwise all in all ametoa mada nzuri.
   
 5. m

  maggid Verified User

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Quinine,
  Asante sana kwa swali lako. Wakati wa chaguzi ndio wakati ambao huwa mgumu sana kwangu. Akili yangu huchemka zaidi. Tatizo letu Watanzani ni ushabiki. Hutokea mara kadhaa, makala moja ninayoiandika hutafsiriwa tofauti kulingana na miwani ya msomaji. Kama ni miwani ya CCM, CHADEMA, CUF na wengine. Au miwani ya Uislamu na Ukristo.
  Tatizo lingine kuna wanaotaka kusikia wanachotaka kusikia. Kusoma wanachotaka kusoma. Ni hulka pia ya mwanadamu. Tumejenga utamaduni wa kuwekana kwenye makabati. Ukimsikia mtu katoa maoni yake, basi, unakimbilia kumtafutia kabati lake, iwe CCM, Chadema, CUF, dini, kabila na mengineyo. Watanzania tumelisahau kabati muhimu sana. Kabati la TANZANIA. Inahusu kutanguliza maslahi ya nchi yetu.

  Uniamini, kuwa nimeandika makala kwa miaka 20 na zaidi sasa. Katika kila ninachofanya, najiuliza kwanza: Kina maslahi kwa taifa? Hakuna hata siku moja nimepokea bahasha ili niandike jambo kwa manufaa ya mwanasiasa au chama cha siasa. Mwenye ushahidi wa kinyume na ninachokisema, aje nao.
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  Maggid

  Wakati wa uchaguzi nilikuwa nafuatilia sana mada zako hasa ulivyokuwa unaripoti habari za Iringa hakuna haja kukumbushana ulikuwa biased kitu ambacho kwa mwandishi kurudisha imani huwa kitu kigumu sana ni kama gazeti la Rai lilivyopoteza wasomaji. Ndiyo maana wengi leo wanakushangaa kuja na maneno haya. Inavyoonekana uko ki maslahi binafsi zaidi ya maslahi ya taifa.
   
 7. m

  maggid Verified User

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Quinine,
  Huo ni mtazamo wako, ni tafsiri yako. Wakati mwingine tunatofautiana, ndio demokrasi hiyo.
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye RED mkuu kuwa makini sana, watu tuna video clip za watu wote wanaochukuwa pesa kwa manji, na ndio maana kelele za Mtikila kosa alilofanja ni kukubali kusainishwa petty cash vocher na Rostam Aziz, kwa sisi wafuatiliaji wa hard news tunaelewa kila kitu kinchoendelea, kulikuwa na Mzee mmoja anaitwa Yusuf Halimoja huyu alikuwa mwandishi wa makala makini sana, lakini yaleyale njaa na akili haviwezi kwenda pamoja.
  Hivi leo Deodatus Balile na Manyerere Jackton unadhani wanaheshimika tena kwenye ulimwenu wa media? mbona Jenerali Ulimwengu ameweza kukomaa kwamba hawezi kutumiwa kama condom na watawala uchwara na heshima yake imebaki juu? na mungu amemuongezea riziki Jenerali sasa hivi anang'ara.
  Majjid nafsini mwako najuwa unajisuta, tubu kwa mungu wako zaliwa upya kataa kutumika, usiwe kama Michuzi yule ni wakala wa ccm ametokea daily news kwahiyo mimi simshangai.
   
 9. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hili nalo neno!! Kutumiwa kama condom. Mara moja unatupa mpaka utakapohitajiiii!!!
  Duh...
   
 10. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa akina majid type bure kabisa,gwiji wa habari anayeweka utanzania mbele bila kujali ni kipindi cha mavuno(uchaguzi) au urafiki ni JENERALI TWAHA ULIMWENGU kwa kweli mungu ampe maisha marefu labda type za kina majid watajifunza kitu
   
 11. Ngoreme

  Ngoreme Senior Member

  #11
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  majid si kweli uko biased sana kwani habari zipo huku tu kana ya ziwa hakuna kuna habari nyingi makara za mazingira huzioni njoo serengeti umuone mwekezaji anavyowafanya wananchi wanapigwa risasi na kupigwa vibaya na walinzi wake sasa majid ona na hili si unakalia makala za kisiasa tu funguka
   
 12. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Umemaliza uandishi wa Habari za Kikwete baada ya Bahasha?
  Uandishi wa kimsimu kama huu sio mzuri, Moyo wako hauna dhamira ya kweli

   
 13. U

  UMPUUTI Member

  #13
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka mimi kimsingi nimevutiwa na hoja za mada yako kuhisiana na hali halisi ya siasa za nchi yetu na kwamba nini kifanyike ili tofauti za kiitikadi na kimtazimo zisiyumbishe utaifa wetu. Lakini hili lingine linalokuhusu maadili yako binafsi ni budi ukalifanyia kazi ili kujisafisha mbele ya wadau.Narudia, ujumbe uliomo ndani ya mada yako umetulia!!
   
 14. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Kaka ujumbe mzuri sana. Ila haukupaswa kutolewa na watu kama Majjid au Balile. Hawa ni watu waliosaidia Tanzania ichafuke kisiasa. Ni kama leo Maro wa Böngofleva aanze kulia ugumu wa maisha wakati alikuwa kila jukwaa akiwaimbia mafisadi. Hauwezi kusingizie eti ni Uhuru wako na Demokrasia. Huo ni upuuzi,hamna demokrasia inayotetea wahujumu,mafisadi na madikteta. Ukitaka kuikosoa Ccm na Makamba basi uiombe samahani Chadema na Dr.Slaa ambao muda mrefu wanawakosoa mafisadi ili wanakwamishwa na watu kama majjing na balile ambao tangu mwanzo hawaitaki chadema iwakosoe mafisadi wanaofanikisha mkate wa akina balile na mjengwa. Hapa nadhani uje kivinginevo na si kuikosoa ccm. Ni bora ungeendelea kwa kuikosoa chadema kwa machafuko ya Arusha bila kuiongelea ccm na chitanda,watu wangekuelewa vizuri. Unaangalia maneno ya makamba baada ya machafuko badala ya kuangalia kwanini machafuko?UMEYA. Au unatibu madhara badala ya kutibu dalili. Narudia thread nzuri kama hii haikupaswa kutoka kwa majjid,unless and until atueleze kama mgao kutoka kwa mafisadi umeisha. Hamna uzalendo wowote hapo. Mungu ibariki Tanganyika!
   
 15. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #15
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  let us give him a benefit of doubt, nadhani anastahili kupewa second chance! Am impressed with today article, swali je ataendelea to put his country first daima? It is just matter of time wandugu zangu
   
 16. m

  maggid Verified User

  #16
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Executive,

  Unadhani nastahili kupewa second chance! Asante sana. Na kuna wanaodhani ni Watanzania na Wazalendo zaidi kuliko wenzao. Je, kuna anayekumbuka Mkapa alipokuwa Tabora mwaka 1997 aliwaambia nini wenye vyombo vya habari vilivyoisakama Serikali yake? Na kwa nini? Historia ni Mwalimu Mzuri. Na mwuungwana kama hana hoja, hukaa kimya.
   
 17. A

  Anold JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Thanks. It is very true!
   
 18. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Turejee kwenye mada!
  Mazungumzo Baada Ya habari ya Arusha nimeyaona na nimeyasikia. Comments;
  a) Miaka ya 70 na 80 niliyasikia Radio Tanzania (RTD) na ilikuwa ni kwa interest ya Watanzania, haya ya Arusha nimeyasikia nakuyaona TBC1, TBC Taifa, Radio One, ITV n.k haya yamelipiwa kaka!! ..yaani yamekuwa dili badala ya fedheha kwa Taifa.
  b) Mazungumzo haya hayakuandaliwa na wahariri wa vyombo husika vya habari ni bali ilikuwa ni presentation au kama movie iliyotafsiriwa
  c) Lengo la mazungumzo hayo ni kuonyesha nguvu ya jeshi la polisi dhidi ya raia wa Tanzania wengine wasiofahamu hata milio ya risasi zaidi ya iliyoko kwenye sinema
  d) Madhumuni ya mazungumzo hayo ni kuhalalisha mauaji ya Watanzania wasio na hatia na kupotosha umma wa Watanzania juu ya mauaji yaliyofanywa na polisi

  Haya yote ni tofauti na mazungumzo ya miaka hiyo yaliyolenga kutujengea maadili na umoja wa kitaifa. Kwa haya ya arusha yanatujengea uhasama, chuki na mgawanyiko wa kifikra na kiitikadi.

  Shame!!
   
 19. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  naomba msaada wa kuelimishwa, ni kipi kilipotoshwa katika mazungumzo haya? si kweli raia waliandamana kuelekea kituo cha polisi kwa lengo la kuwatoa viongozi wao kwa maelekezo ya Slaa? au polisi walifuata raia nyumbani kwao wakawamiminia risasi kisha wakatengeza sinema yao na kuionesha TBC?
   
 20. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Maggid!!! how do you convince me that a THIEF should be honored as MR PRESIDENT? - Kulikubali hili ni kukubali kutokuendelea! haya la Kikwete limepita na hili la MEYA je? CCM walibipu kwenye uraisi, raisi wangu DR SLAA akafunika kombe mwanakharamu apite, wakadhani ni masikhara! hili la arusha no ways!!!!!!!!!!rudi kajipange upya! heri kuishi maisha mafupi lakini mazuri!
   
Loading...