Wrong number imenivurugia ndoa

Wrong number imenivurugia ndoa

INSONSILE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
1,869
Reaction score
2,734
Jamani, mwenzenu nimevurugwa mpaka nimevurugika,Jana nilirudi kutoka kazini nimechoka sana. Na ninapolala huwa sipendi kukaa na simu kitandani kwa kujua ina madhara kiafya. Ila niliweka mlio wa vibration kwa sababu sipendi makelele ya simu ninapokuwa nimelala. Ilipofika mida ya saa nne na nusu au tano kasoro, simu ikavibrate.

Mke wangu akanishtua kuwa simu yangu inaita. Basi kwa sababu ya uchovu sikutaka kuamka, nikamwambia aniletee. Aliponiletea akawa amefungua na kuona kuna sms imeingia. Akaisoma. Sikuona tabu maana siku zote huwa anachukuaga tuu simu yangu na anaweza kukaa nayo kadiri aonavyo yeye na akipenda anapitia whattsapp au sms inbox au kucheza games kwa uhuru bila tatizo lolote.

Sasa jana Message iliyoingia ni ya kimapenzi kutoka kwa new number sms yenyewe inasema, "Nimelala mpenzi wangu, naamini na wewe pia umelala, uniote umenikumbatia, si unaona baridi hii? I wish ungekuwa hapa jamani leo nina hamu ile mbaya..." Ghafla mke wangu anabadilika sura na maongezi. Nikarushiwa maswali yaliyojaa ghadhabu kama mvua ya mawe. Nikaiomba nione kucheki namba mpya, daaah nikapigwa butwaa.

Nikasema isiwe tabu, ngoja tuende tigopesa tujaribu kama tunatuma pesa ili tujue jina. Kweli tulipata jina, wala hata silijui la wapi, nikaona isiwe tabu, ngoja nimpigie nimwulize. Mara wife akanyang'anya simu apige yeye mwenyewe. Ilivyopokelewa tu yaani hata mtu upande wa pili hajajitambulisha vizuri kashushiwa mvua ya matusi, vijembe na vitisho kibao.

Honestly nilipanic sana. Heri ingekuwa ni mtu ninayemfahamu au ni mchepuko wangu ningejisikia guilty. Lakini ukweli simfahamu huyo mtu. Baada ya kukata simu, nikageuziwa mashitaka, kuwa namfahamu ila nimefanya makusudi kutokusave namba, na huyo mwanamke anajifanya kakosea ili kuepuka zali.

Daah nikajieleza nijitetee lakini wapi, hapakukalika wala kulalika. Tumeamka asubuhi vurugu mechi, sasa nikipiga ile namba hapokei tena sijui ni woga wa kutukanwa. Jamani hebu vaeni kiatu changu alafu mnishauri nifanyeje mwenzangu anielewe? Mpaka sasa sijajua huyo aliyetuma sms yuko wapi? ila nimechukua tuu namba na jina lililosajiliwa nalo kwenye tigo pesa.

Sijawahi kupata zali kama hili
 
Sasa mkuu unapanic nini wakati humfahamu.... Kuwa mpole hawezi kosea tena ashatukanwa huyo.......

Ama unataka kumuomba msamaha kwa kutaka kuvuruga ndoa yako?
 
Kama mwanamke, kamshughulikie ujue unatukanwa kihalali.Mbona mwenzio alisingiziwa anatoka na dancer wa Domo, akaacha ndoa akafanya kweli? Cha gamka brother!!!
 
mtafute uchepuke nae yale matusi ya mkeo yawe yameenda kihalali!
 
Pole sana huna la kufanya zaidi ya kumhakikshia mkeo huyo mwanamke humjui na hujawahi kuwa na mawasiliano naye ya aina yoyote ile.

Hawa wanaopiga simu/kutuma text messages kwa kukosea namba ni hatari sana makosa yao yanaweza kabisa kusababisha uchumba au hata ndoa ivunjike/kuweka dosari kubwa sana kwa kukosea namba iliyokusudiwa.
 
Asante sana BAK, USHAURI wako ni nmzuri na unatia faraja. Nasikitika humu JF kuna watu mara zote wanaleta jokes, utadhani wanaishi mbinguni. Kuna mmoja hapo juu anasema nimtokee, hivi assume huyo mtu yuko mwanza na mimi niko tunduma. Hivi nimtokee nadhani ni zaidi ya uchizi. Ngoja yawakute ndo mtajua tamu na mbichi. Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza. Endeleeni kuishi ulimwengu wa Isidingo

Asante sana BAK kwa mara nyingine.
 
Last edited by a moderator:
Kama hataki kuelewa achana naye aungue na moto mwenyewe.
 
Pole sana mkuu jitahidi kuwa karibu na mkeo taratibu ataelewa.
Na Mungu si athuman,inaweza nayeye ikamtokea,
Mwambie unamaanisha na wewe ikikutokea nawe nikutilie mashaka.
 
Kweli hivyo viatu vyako ni ngumu kuvivaa
ila unachoweza kufanya mpaka sasa ni kumtuliza au kumuacha bibie atulie kwanza then

umwambie tena kwamba hi namba siijui na kwakua sio kqeli na bibie apokei simu basi tusubiri uone kama atatuma tena
trust me kwa kuwa wewe ni mkweli Mungu atazimama upande wako
 
Mbona ishu ya kukosea namba inatokeaga sana tu, unless ulishawahi kumchiti ndo maana anachukulia kweli
 
Inaonekana huaminiki ndo maana mwenzio hakuelewi, pole sana
 
Mwachie simu yako akae nayo just for 1week ili apate kuamini kweli alikosea namba la sivyo atajua bado mnaendelea kuwasiliana
 
Pole sana huna la kufanya zaidi ya kumhakikshia mkeo huyo mwanamke humjui na hujawahi kuwa na mawasiliano naye ya aina yoyote ile. Hawa wanaopiga simu/kutuma text messages kwa kukosea namba ni hatari sana makosa yao yanaweza kabisa kusababisha uchumba au hata ndoa ivunjike/kuweka dosari kubwa sana kwa kukosea namba iliyokusudiwa.

Au kifo kabisaaa!
 
Hawa wenye jazba km hizi nina uzoefu nao. Pole
 
Mkuu attitude ya baadhi ya wanachama humu pale mtu ana tatizo lake na anaomba ushauri inasikitisha sana. Sijui ni akili ya kitoto, uhayawani au vyote? Pole sana. Muonyeshe huu uzi kama huoni noma inaweza kusaidia katika kupunguza hasira zake.

Asante sana BAK, USHAURI wako ni nmzuri na unatia faraja. Nasikitika humu JF kuna watu mara zote wanaleta jokes, utadhani wanaishi mbinguni. Kuna mmoja hapo juu anasema nimtokee, hivi assume huyo mtu yuko mwanza na mimi niko tunduma. Hivi nimtokee nadhani ni zaidi ya uchizi. Ngoja yawakute ndo mtajua tamu na mbichi. Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza. Endeleeni kuishi ulimwengu wa Isidingo

Asante sana BAK kwa mara nyingine.
 
Pole sn ndugu yng.kwnz jaribu kuwa mpole kuwelewa mkeo n atakulewa 2,kwn kwa sasa itkuwa n vigumu kukuelewa kwn bdo ana joto la wivu,ww kaa chini mueleweshe mwsho wa cku ukwel unabaki n uongo unajitenga.izo n changamoto ktk ndoa kabiliana nazo kaka.
 
Mwachie simu yako akae nayo just for 1week ili apate kuamini kweli alikosea namba la sivyo atajua bado mnaendelea kuwasiliana

Kwani hakuna njia nyingine ya kuwasiliana zaidi ya mke kuachiwa simu? Unaishi dunia gani weye?
 
Chukua BIBLIA (kama mkristo) Au QUR'AN (kama Ni Muislam) Weka Kichwani Mwako Anza Kutoa Viapo Vikali Ukiwa Serious Kua Huyo Mdada Amekosea Tu Namba Si Mpenzi Wako Hamna Uhusiano Nae Na Wala Humjui. Njia Hii Kidoogo Inaweza Kukusaidia Kurudisha Ka Iman Yake Kwako.
Pole Sana Mkuu.
 
Kwani hakuna njia nyingine ya kuwasiliana zaidi ya mke kuachiwa simu? Unaishi dunia gani weye?


Hapo napo neno.
Nimeshawahi kusoma hapa JF, na pia nimeshaona kwa baadhi ya watu tunafanya nao kazi. Mtu ana simu ambayo hata wife hajui. hiyo simu inakaa kwa ofisi tuuu au kwingineko lakini haikanyagi home. Wengine wana fb accounts fake, email fake, yaani kila kitu fake. Akifika home wife hata akague simu au akae nayo siku mbili, zitaingia simu official tu.

Kalagabao
 
Back
Top Bottom