Wrf model

sellonlatbox

Member
Joined
Jul 10, 2012
Posts
57
Reaction score
18
Wakuu ni kwenye vyuo vipi au taasisi zipi hapa Tanzania wanatumia Weather Research and Forecasting (WRF) model ukiacha Tanzania Meteorological Agency (TMA)?

Kidogo kuhusu hii model, inapart kubwa nne (blocks) na block ya nne inahusu uandikaji wa results.
Hivyo basi nimejaribu kuirun kwa eneo la longitude kuanzia 28E-50 E na latitude 14S-4N, tarehe kuanzia 00hr 25/12/2012 hadi 00 hr 26/12/2012 (24hrs), model inaandika taarifa/results (variables/parameters) kwenye file yenye extension(.ctl),na data kwenye file lenye extension (.dat).
Najaribu kuiattach ili tuweze ona kuwa idadi ya variables vars ni 98, na ni tofauti tofauti na ambazo zinaweza kutumika kwa kazi na tafiti tofauti tofauti.

 

Attachments

Mkuu shida yangu kubwa ni kufahamu sehemu na wadau ambao wanatumia hiyo model iwe kwenye tafiti zao, kazi za kila siku (maofisini) au vyuo ( kama wanafundisha au na kutumia hiyo model) .
 
Wakuu ni kwenye vyuo vipi au taasisi zipi hapa Tanzania wanatumia Weather Research and Forecasting (WRF) model ukiacha Tanzania Meteorological Agency (TMA)?

hebu vitaje vyuo vya Hali ya hewa unavyovijua wewe hapa Tanzania.
 
unaweza anzia pale DIT wana supercomputer ambayo inaweza fanya hizo kazi kama weather forecasting,labda wao watakupatia information zaidi.
 
hebu vitaje vyuo vya Hali ya hewa unavyovijua wewe hapa Tanzania.
Mkuu sijui kama kuna chuo cha aina hiyo ila inawezekana sikutoa maelezo ya kutosha kuhusu hiyo model. Wakati wanaianzisha malengo makuu ilikuwa itumike kwenye mambo ya hali ya hewa lakini kwa sasa ni zaidi ya hali ya hewa, inatumika kwenye tafiti tofauti tofauti zikiwemo zinazohusu mambo ya mazingira, ecology, air quality over urban areas,aerosols, ozone, atmospheric chemistry n.k..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…