Boutafrica
JF-Expert Member
- Dec 11, 2014
- 955
- 2,072
Muhogo tutakukumba daima
hana lolote sasa hivi ndo anajifanya kuwa na uchungu na rasilimali za nchi... aende uko..
Boss Mimi binafsi nampongeza Mhongo kwa maamuzi aliyofanya, hata kama ni kwa kushinikizwa lakini ametekeleza kile ambacho bunge lilipendekeza na ambacho wananchi walikuwa wanakisubiri kwa hamu. Ni moja ya uzalendo na uwajibikaji. Ni mategemeo yangu kuwa waliobaki au walioingia upya katika nyazfa mbali mbali wamejifunza kutoka sakata hili la escrow. Kinachonikera ambacho bado sijapata majibu yake ni fedha hizo zilizopotea, zitarudije ili ziwafae maskini vijijini na wanafunzi wanaokosa hadi chaki ya kuandikia kama hatujataja madawati ya kukalia?
prof. yuko safi na anajua nini kakifanya kwa tz na bado anamchango mkubwa dunian anahitajika pia nakuombea prof.mhongo
Muhogo tutakukumba daima
Upo sahihi kabisa. Lakini sisi tumbili kawaida yetu kuibiwa tu. Mbona dhahabu imechimbwa na kuondoka hatujafaidi lolote sana sana wazawa wamefukuzwa kwenda sehemu za mashamba yao kupisha uchimbaji, wengine wameuwawa na wengine wanakunywa maji ya sumu (mercury) lakini Muhongo hajafanya kitu hapo. anakuwa na uchungu wa mafuta na gesi wakati rasilimai nyingine inaondoka yupo yupo tu. Hao aliokuwa anawapata mikataba ya gesi ndiyo hao hao walikuwa wanachimba dahabu.Kwa tunaoelewa mambo Muhongo yupo sahihi. Norway ilipopata mafuta haikukabidhi wazawa kuendesha uchimbaji, ilileta wa USA, ila ilichokifanya ni kusomesha watu wake (pia kufungua vyuo vya Trondheim na Stavanger university) ili kusomesha wataalam. Ilichokifanya ni kuwa na umiliki kupitia serikali. Ilipofika kipindi wakaona labour force inatosha waliwafukuza wa USA na serikali kupitia STATOIL wakaendea na uchimbaji na wazawa wanachofaidi ni supporting industries (mfano vyakula, repairs za mitambo, ulinzi etc). Hiyo model iko pia uarabuni etc. sasa kwa nchi kama Tanzania hao akina mengi hawana ubavu na niwabinafsi. Model ilioichukua serikali ni sahihi, na uzuri mikataba ilishatiwa sahihi hakuna wa kubadilisha.
Kwa tunaoelewa mambo Muhongo yupo sahihi. Norway ilipopata mafuta haikukabidhi wazawa kuendesha uchimbaji, ilileta wa USA, ila ilichokifanya ni kusomesha watu wake (pia kufungua vyuo vya Trondheim na Stavanger university) ili kusomesha wataalam. Ilichokifanya ni kuwa na umiliki kupitia serikali. Ilipofika kipindi wakaona labour force inatosha waliwafukuza wa USA na serikali kupitia STATOIL wakaendea na uchimbaji na wazawa wanachofaidi ni supporting industries (mfano vyakula, repairs za mitambo, ulinzi etc). Hiyo model iko pia uarabuni etc. sasa kwa nchi kama Tanzania hao akina mengi hawana ubavu na niwabinafsi. Model ilioichukua serikali ni sahihi, na uzuri mikataba ilishatiwa sahihi hakuna wa kubadilisha.
Katika series ya zilizala la escrow linaloendlea kupukutisha vigogo,leo ktk zamu ya prof Muhongo kufungasha virago kuna maneno machache kawaachia watz kwamba yeye anaondoka lakn wananchi muwe makini na RASILIMALI YA GESI HUENDA IKAWAFAIDISHA WATU WACHACHE NA FAMILIA ZAO TU..sasa me najiulza hivi kile kiporo kimechacha kabla ya kuliwa au ndo "UKIMWAGA UGALI NAMWAGA MBOGA".