World Economic Forum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

World Economic Forum

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ngoshwe, May 6, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimeungana na watanzania wengine wakereketwa wa nchi hii kufuatilia majadiliano yanayoendelea katika kongamano la "WEF, 2010".

  http://www.weforum.org/en/events/WorldEconomicForumonAfrica2010/Webcasts/index.htm

  Najaribu kupambanua jinsi gani viongozi wetu walivyo na upeo tofauti wa kutazama, kuyaelezea na kuyatafutia ufumbuzi matatizo mengi ya nchi zetu za kiafrika. Inasikitisha sana kuona wapo viongozi ambao wana mtazamo wa juu kabisa kwa maendeleo ya nchi zao na kuna wale ambao ni dhahiri kabisa wanatumia muda mwingi kuyatangaza matatizo ya nchi zao ambayo wanayajua na yapo kwenye ilan na mikakati ya maendeleo kama nguzo ya kuwajenga kisiasa zaidi na kujipatia umaarufu wa kuongea tuuuuu pasipo hatua madhubuti za kuyakwamua.

  Kwa mfano, wakati uchumi wa Tanzania unategemea zaidi ya asilimia 80% kwenye kilimo, nashangaa kusikia Mhe. Rais wetu anasema kuwa kwa sasa moja ya vipaumbele ni kuongeza uwezo wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (National Food Serves ) kwa kuwa tulishindwa kuwasidia wenzetu wa Kenya walipoomba msaada. Kwa mtazamo wa kiuchumi, ina maanisha kuwa Serikali imejikita zaidi katika kuhifadhi ziada bila kuwa na mikakati madhubuti ya kuwasaidia wakulima kuzalisha kuzalisha ili kupata hiyo ziada ya kuweza hata kuhifadhi kwenye hizo Hifadhi za Taifa za Chakula.

  Ukifuatilia kumbukumbu za matukio, unaweza kuona kuwa hata hiyo Hifadhi za Taifa za Chakula (National Food Reserve) imekuwa ikitumika tu kuhifadhi mazao aina ya nafaka (sana ni mahindi) tena pasipo kutimiza lengo na mbaya zaidi imekuwa ikitumiwa na wanasiasa kwa ajili ya kujipatia umaarufu hata katika kipindi ambacho hakuna njaa. Hifadhi hiyo ya chakula imekuwa pia ikitumiwa kama ghala la chakula cha misadaa wakati wa maafa zaidi na kupoteza maana yake halisi ikiwemo kusaidia kuongeza uzalishaji kwa wakulima kwa kusukuma bei za wafanyabishara binafsi na kuwa na mazao mbadala ya kuhifadhi zaidi ya mahindi..

  Isitoshe, kwa muda mrefu nchi yetu pia imeshidwa kumudu hata kukabiliana na maafa kupitia hiyo hifadhi ya chakula ya taifa na imekuwa ikitegeme pia kuagiza mahindi kutoka nje ya nchi kupitia wafanyabiashara binafsi ili kuhifadhi pia kwenye hiyo Hifadhi ya chakula (ikumbukwe pia si zaidi ya miaka saba imepita, Serikali imewahi kununua mahindi kutoka kwa majirani zetu wa Kenya "National Cereal Board" nchi ambayo haina uwezo wowote wa kuzalisha chakula kuliko Tanzania kutokana na rasimimali zake na kwa sasa hao wakenya wapo wengi hapa nchini wakinunua mzao kwa staili tofauti kwenda kuuza nje. Pia tumewahi kuagiza si mara moja mahindi toka Marekani na kwingineko duniani kwa maana kuwa hatujajitosheleza kiuzalishaji wa ndani.

  Kwa maana nyingine ni kuwa, hatuwezi kuwa na ngo la kuongeza uwezo wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula ambayo haiendani na lengo la kuwafanya wakulima wetu kuzalisha ziada, ikwemo kutowasaidia wakulima hao kuongeza ukubwa wa mashamba yao, kutumia mbinu bora za kilimo, kulima kilimo cha kibiashara na kadhalika. Vinginevyo, itakuwa ni kuishia kuwafanya wakulima wakose soko la maana kwa kuwa tuna njaa ya kitaifa na kuwazuia kuuza mazao yao nje ya nchi pale tunapodhani tuna njaa wakati ambao hatujawasaidia kwa mtaji wowote kuzalisha.

  Wakati kwa wenzetu wa Malawi wanaelezea mafanikio makubwa katika kilimo kufuatia uamuzi wa Serikali yao kutoa ruzuku ya pembejeo kwa wakulima kuanzia mwaka 2005, Tanzania ambayo imekuwa ikitoa ruzuku hiyo kwa wakulima tokea mwaka 2003, imeshindwa kabisa kuelezea mafanikio yoyte ya ruzuku hiyo ya pembejeo ambayo imekuwa ikitumia fedha nyingi za umma sasa kupitia mfumo wa vocha (Voucher system). Badala yake tunajififia kwa kuongeza wagani (extension officers) ambao wanaenda kusimamia wakulima wasio na mtaji,mashamba ya kueleweka, miundo mbinu ya umwagiliaji wala mfumo bora wa masoko!...

  Mtazamo wangu ni kuwa labda matatizo yanayofahamika kwetu huwa ndio yanatumika kwa ajili ya kuombea kura tu. Yaani hatuwezi kujifunza kutoka kwa wenzetu?.
   
 2. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2010
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bana bana bana! Pamoja na kwamba Ethiopia wanataabika na njaa...Meles ana mtazamo makini sana kuhusu maswala haya...JK kapwaya hakuna hata uhusiano na Kilimo Kwanza sijaona kama ameweza kuhusianisha hii discussion na kilimo kwanza!
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Yaani aibu tupu kwetu jamani,..Hata hiyo Kilimo kwanza sijui kama imekwisha saidi lolote kwa wakulima wetu.

  Nambuka Kauli Mbinu hii ya KILIMO KWANZA iliibuliwa na kuzinduliwa kwa mbwembwe mno lakini hata mwaka haujaisha simekuwa ziiiii. Kuna watu walitabiri kuwa ni wajanja wametengeneza njia za kujipatia umaarufu. Matatizo yote yaliyoelezwa kwenye andiko la KILIMO KWANZA kuhusu kilimo chetu ni yale yale tu ambayo unayakuta kwenye MKUKUTA, Tanzannia Develipment Vision 2010 - 2025, ILANI YA CCM 2005, MKakati wa Kilimo (Agricultural Sector Development Startegy 2001); Mpango wa Kuendeleza Kilimo (Agricultural Sector Development Programme 2003 (ASDP); Sera ya Maji ya Mwaka 2002; Sera ya Kilimo na Mifugo ya mwaka 1997; Sera ya Mifugo ya Mwak 2006; Sera ya Masoko na Mikakati mingine mingiiii ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa...  Sijui tunaenda wapi...

  Kwa mfano wakati Serikali ilipokurupuka kutoa ruzuku ya pembejeo (Fertilizer subsidy), kuongeza maafisa wa Ugani na baadae kuagiza matrekta kwa ajili ya kuwakodisha wakulima hakuna mkakati wowote wa kuwa na maeneo makubwa ya kilimo cha kibiashara, hatuna miundo mbinu ya umwagiliaji, wala masoko ya Mazao ya hao wakulima!. Kila mwaka ni hayo hayo yanayozungumwa lakini hakuna hatua chochote kinaendelea.

  Huku akijua wazi kabisa sababu za kutoendele kwetu, Mhe. anajaribu kutoa mifano ya kufananisha uchumi wa Tanzania na USA bila hata kuona tofauti kubwa ya kimaendeleo na kujua iliypo labda kama angefananisha bara zima la Afrika na USA!..na anasema "we can't do much" huku anasema "we can are not dependable on aids, kule anasema "we need to be assisted" (mpaka vandalua na dawa za malaria tusaidiwe??) ....ni nini tafsiri yake kama hatuwezi zaidi ya hapa tulipo ??? kuna haja gani ya kukutana na kujaliana changamoto zetu za kimaendeleo, duh, total contracdictions?? sijaelewa mwelekeo wa hii kitu kama Mkulu hajajipanga kihivi. Ni kama yale yale yale ya Sullivan Summit!.
   
 4. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2010
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwishoe akatoa maendeleo ya ruzuku ya pembejeo wakati imegubikwa na mizengwe ile mbaya!
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Anabahatisha hoja, hakuna kitu hapo, tena labda kama Waziri mwenye dhamana ya Sekta angeombwa aongee mwenyewe labda angeeleweka!. Si umeona mpaka Tyson (Stephen Masato Wassira) anakuna kichwa kuashiria kuwa hakuna pointi toka kwa kinywa cha mzee??, labda Tyson ndo atakuwa ametuma ki memo cha kumtaka Mhe. aelezee hayo ya ruzuku za pembejeo ambayo hayana muunganiklo kabisa na hoja za msingi wala taarifa ya kina ya mafanikio ya zoezi zima la utoaji wa hizo ruzuku kwa wakulima ambao sasa wanaombwa tena kuchangia CCM kwa sms !.
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuleta foleni kubwa mjini na kufunga baadhi ya maeneo kwa ajiri ya "mkutano huu muhimu", kwangu mimi this is just another talk show. Sitegemei kwa style ya leadership tuliyonayo kuona lolote tofauti zaidi ya sifa za kufanikisha wathungu kutoka walikotoka mpaka kuja kutua Dar Es Salaam. Mnisamehe msinitishie risasi za moto maana, huu ni mtazamo wangu ambao unabase kwenye yale ninayoyaona yakiendelea siku hadi siku.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,619
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Kila la kheri mkutano wa WEF Afrika


  [​IMG]
  Maoni ya katuni  Mkutano wa Kiuchumi wa Dunia kuhusu Bara la Afrika (WEF), unatarajia kuanza kesho jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha wakuu wa nchi na serikali kadhaa barani. Tayari maandalizi ya mkutano huo yamekamilika kwa sehemu kubwa, ikiwa ni pamoja na kuanza kuwasili kwa wajumbe wakiwemo maofisa waandamizi na viongozi.
  Mkutano huo ni mkubwa kwa kuzingatia kwamba unawashirikisha wajumbe 1,000, idadi ambayo ni kubwa.
  Kwa bahati nzuri, Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo muhimu ambao utajadili mambo mengi muhimu, yakiwemo ya uchumi kwa ujumla na utawala bora barani Afrika.
  Mkutano huo wa kwanza kufanyika katika ukanda wa Afrika Mashariki tangu ulipoanza miaka 20 iliyopita, utawahusisha Marais Armando Emilio Guebuza (Msumbiji), Paul Kagame (Rwanda) na Ali-Bongo Ondimba (Gabon). Wengine ni Hifikepunye Pohamba (Namibia), Boni Yayi (Benin), Jacob Zuma (Afrika Kusini) na mwenyeji wao, Jakaya Kikwete (Tanzania).
  Mbali na marais hao, atakuwepo pia Makamu wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein na Mawaziri Wakuu, Morgan Tsvangirai (Zimbabwe), Raila Odinga (Kenya), Meles Zenawi (Ethiopia) na Mizengo Kayanza Pinda (Tanzania).
  Mkurugenzi wa WEF katika Afrika, Katherine Tweedie, alisema katika mkutano huo, pia wadau wengine katika uchumi na maendeleo ya jamii watakuwepo kujadili dhima inayosema `kurejerea mkakati wa ukuaji Afrika’.
  Alisema viongozi hao na washiriki wa WEF, pia watajadili masuala ya kijamii yatakayochagiza kupata msingi bora wa Afrika ya baadaye kwa mtazamo wa kidunia.Baadhi ya mada zitakazojadiliwa ni elimu ya juu, kurejerea ushindani barani Afrika, Waafrika bilioni moja ni fursa ama hatari?
  Nyingine ni muingiliano wa kikanda, hali ya rasilimali za asili ifikapo 2030, vikwazo dhidi ya ukuaji wa fursa za Afrika, ushirikiano wa India na Afrika, vita, amani na haki ya ulinzi. Ratiba ya WEF inaonyesha kuwa Rais Zuma ataelezea kuhusu ujenzi wa Afrika Kusini wakati na baada ya mashindano ya Kombe ya Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
  Aidha, kutakuwepo na mada kuhusu Zimbabwe, ambayo pamoja na mambo mengine, itagusa hali ya baadaye kiuchumi, hususan baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa. Mjadala huo pia utachangiwa na Waziri wake Mkuu, Tsvangirai.
  Rais Kikwete atashiriki mijadala kuhusu dira mpya ya kilimo barani Afrika na kufungua fursa za ukuaji uchumi barani.
  Rais Guebuza wa Msumbiji atafungua warsha kuhusu mfumo mpya wa ushirikiano kwa maendeleo ya kiuchumi barani, wakati Odinga atashiriki kujadili sayansi na teknolojia dhidi ya uendelevu, ukuaji na maendeleo.
  Pia Marais Zuma, Kikwete na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Makazi Duniani (UN-Habitat), Anna Tibaijuka, ni miongoni mwa watakaojadili mada ya ubunifu wa wajibu wa Afrika katika uchumi mpya wa dunia.
  Mada muhimu ya demokrasia ya baadaye barani Afrika, itajadiliwa pia Raisi wa Bunge la Pan-African kutoka Afrika Kusini, Idirsaa Moussa.
  Kimsingi, mkutano huo unawakutanisha viongozi wa kisiasa na watu wengine mashuhuri katika bara hili na hiyo inaleta matumaini kwamba mataifa ya Afrika sasa yamefikia mahali na kuona umuhimu wa kujadili masuala muhimu kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa watu wao kiuchumi, kisiasa na kijamii.
  Tunasema hivyo kutokana na miaka ya nyuma viongozi wa nchi na serikali za Afrika kukutana na kujadili kuhusu utatuzi wa migogoro iliyokuwa inatokana na vita.Tunawashauri wajumbe wa mkutano huo kuyajadili masuala yaliyopangwa kwa kina na kwa uwazi ili changamoto zitakazobainika ziweze kurekebishwa.
  Baadhi ya nchi zinafahamika kwamba zinakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa utawala bora hivyo tunawashauri wawakilishi wake katika mkutano huo kupokea ushauri watakaopewa na kuufanyia kazi.
  Nchi itakayokataa kupokea changamoto hizo, itakuwa inajidanganya kwa kuwa dunia ya leo ya utandawazi nchi yoyote haiwezi kupata maendeleo ya kiuchumi ikiwa itakaidi kuheshimu misingi ya demokrasia na utawala bora.
  Matumaini yetu ni kwamba yatakayojadiliwa na kukubaliwa yatakuwa ni msimamo wa pamoja wa mataifa hayo. Tunawakaribisha wajumbe na tunautakia mkutano huo mafanikio.  CHANZO: NIPASHE
   
 8. J

  Jafar JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkutano umeisha - swali langu kubwa ni kuwa tumefaidika na nini?
  What have we benefited and what have we learnt?
   
 9. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hicho kichwa umekitendea haki kabisa kukifagilia jana kimetema point sana, simple and clear, alikuwa ana hit point direct hakuna mh mh mh, na alikuwa anatema data kama Magufuli. Nafikiri atakuwa star kwenye hii mkutano akifwatiwa na Odinga.
   
 10. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Hivi kwa nchi iliyo na rushwa iliyokithiri kama Tanzania, rushwa iliyotapakaa toka ngazi za juu kabisa za uongozi hadi watendaji wadogo kabisa - toka kwa waziri mpaka mfagiaji - ni maendeleo ya mamna gani unayodhani yanaweza tokea? Tanzania ikiendelea itakuwa miujiza!

  Hamna mpango wowote wa maendeleo unaoweza kufanikiwa kupita kwenye pori nene la rushwa lilojaa ubadhilifu, ubinafsi, ufisadi na kila mamna ya kukumbatia umasikini.

  Unapoamka asubuhi, fikiria maendeleo yako binafisi, la hasha kama unataka kuendeleza nchi basi anza na kupambana na rushwa kwanza, vinginevyo ni kupoteza muda.

  Ni kitu gani Tanzania haina ambacho WEF inaweza leta kusababisha maendeleo?

  Nakumbuka mama yangu aliniambia "Hakuna kitu kibaya kama laana!" Sasa nimekua na nimeona ukweli.
   
Loading...