usanii mwingine bwana yaani katika bidhaa za selling from home mmeona RFID.
U re not serious.
Moderator fungeni hii thread hawa ni matapeli hakuna cha Toronto wala london. Hawa ni watu wa kufish privacy inforamtion za watu
Kwanza kabisa, nna-uhakika huelewi RFID ni nini, laiti ingekuwa unaelewa basi usingeihusisha na "kufish".
Pili, nakuomba tafadhali futa kauli yako ya kutuita matapeli. Napenda kukufahamisha kuwa sisi ni wafanya biashara wa halali na tunafanya biashara zetu kihalali tuna office zetu kihalali Tanzania na tumesajiliwa Tanzania kihalali na tutakuwekea anuani yetu hapa chini, ututembelee wewe na mwingine yeyote apendae na utuoneshe utapeli wetu ni nini?
Tatu, kuhusu uuzaji wa bidhaa, ya ama ziwe RFID ya ama ziwe zozote zile "from home" ni mtindo ambao unatumika dunia nzima kwa sasa na labda kwa umbumbumbu wako hilo hulielewi. Hebu tuambie, ni nini kinachomfanya mtu asiweze kuuza RFID solutions "from home"? Labda ni lugha imekupiga chenga na huelewi tofauti ya "from home" na "at home".
Ikiwa mtu anaweza kufanya kazi ya kuuza "independently", na kwa sasa huduma za mawasiliano zipo popote, si lazima uwe "ofisini", kwa nini tusiitumie fursa hiyo? na kupunguza gharama za maofisi? nadhani haupo dunia ya leo.
Nakuomba tafadhali sana rejea anuani zetu zote tunazokupa hapa chini na utembelee ofisi zetu za Tanzania na "principals" wetu huko Canada. Na kama huna uwezo wa kufika huko, unaweza kuwasiliana na ubalozi wa Canada Tanzania au ubalozi wa Tanzania Canada ili wakusaidie kutujuwa sisi ni nani na tunafanya kazi vipi.
Business Services & Consultancy Ltd., (BSC) ni Kampuni inayomilikiwa na waTanzania kwa asilimia mia moja (100%). Licha ya kuanza kuiwakilisha hii kampuni ya Falken Secure Networks ya Canada hivi karibuni, BSC kwa miaka mitatu sasa inaziwakilisha kampuni zingine 3 za ki Canada. "Snub Pro Africa Ltd. (SPA) Water Wells Drilling Company" ni moja ya kampuni ya Canada ambayo tunaiwakilisha na kuisimamia kazi zake zote za uchimbaji wa visima hapa Tanzania. Kwa kukujuza tu, SPA imesha-chimba visima vingi tu vya maji Tanzania vya Serikali na watu binafsi na hakuna "complain" hata moja mpaka dakika hii. Na inasimamiwa na kuendeshwa na wafanyakazi wa kiTanzania kwa asilimia mia moja (100%). Na hivi juzi tu tumemaliza kuchimba visima virefu vitano vya halmashauri ya Mkuranga kwa niaba ya kampuni ya EFAM ya Tanzania.
Kampuni zingine za ki Canada tunazo ziwakilisha Tanzania ni:
TEJA Food Groups
514- 42nd Ave SE
Calgary, Alberta, T2G 1Y6
Phone 403-243-3478
Fax 403-243-8989
email: "teresa@tejafoods.com"
website:
TEJA FOOD GROUP- Source for Quality Seafood Items
ISG LTD
11377 85 St. SE Calgary
Ph: 403-922-2836
Em:
aboki@shaw.ca
Tunasikitishwa sana, wakati sisi tunahangaika kutafuta kazi kwa manufaa yetu, ya Taifa letu na wa Tanzania wenzetu kwa ujumla, wanatokea watu kama wewe ambao hawajui wanachokiongea na kukurupuka tu na kutupakazia.
Tunakuomba utuulize chochote usicho kijuwa kuhusu RFID na au kuhusu sisi, kazi zetu na sisi ni kina nani na tutakufahamisha, ya ama uje ofisini kwetu au majumbani kwetu au utupigie simu, au utuandikie barua pepe au utuulize hata hapa kwenye nyuzi za JF. Lakini tafadhali, tunakutahadharisha usituharibie jina letu, kwani nna uhakika hutujui mwanzo wala mwisho na umekurupuka tu.
Anuani zetu za Tanzania ni:
Business Services & Consultancy Ltd.
Millennium Business Park,
Office No. 7, Morogoro Rd. Dar Es Salaam.
Namba zetu za simu ni: +255 22 2401154 Mobile: +255 754 484384
Email:
yourbsc2010@yahoo.com
Address za Falken Secure Networks ni hizi:
8 Golfdale Court, Suite 101
Caledon, Ontario, Canada
L7E 0B3
Tel: 1-905-880-4044
Fax: 1-519-268-8711
email:
sales@falkensecurenetworks.com
website:
Falken Secure Networks
Ahsante,
Abdul Ghafur
Managing Director
BSC Ltd.