Wizi wa simu mabasi ya Mikoani

Wizi wa simu mabasi ya Mikoani

telex

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2015
Posts
406
Reaction score
103
Wizi ktk mabasi ya mikoani hasahasa katika kituo kikuu cha mabasi ubungo umekua ni kero isiyo na tiba kutokana na ubunifu unaojitokeza kila kukicha.

Leo asubuhi dada mmoja aliekua akisafiri na basi moja kutoka dar es salaam kwenda mkoani mbeya amejikuta akilia kama mtoto baada ya kuibiwa simu yake ya gharama ndani ya basi hilo.

Ilikuwa hivi;

Dada huyo aliekua amekaa siti moja na kijana mmoja mtanashati na mwenye umbo la unene, kijana huyo ambae alilipa nauli ya watu wawili huku akimweleza kondakta kua yupo mwenzake atapandia kibaha maili moja, huku jamaa huyo akiwa bize kuwasiliana na huyo wa kibaha gafla alimwomba abiria mwenzake simu yake ili aendelee kuwasiliana na mwenzake kwani simu yake ilizima chaji.

Dada wa watu pasipo kujua anaibiwa alitoa simu yake ndogo aina ya nokia tochi akampatia jamaa mawasiliano yakaendelea mpaka dakika zikaisha, dada wa watu kwa huruma ya kitanzania huku gari ikiingia stendi maili moja akatoa simu yake kubwa (smartphone) akampatia jamaa ili amuelekeze ndugu yake gari ilipo, jamaa akionekana kuingiwa na jazba na hasira mpaka akasimama ili angalie nje na simu ikiwa sikioni akimwambia mwenzake njoo kwenye geti la kutokea gari inakaribia kutoka fanya haraka.

Jamaa alipoona gari inatoka alisimama kutoka kwenye kiti na simu sikioni na kushuka kwenye gari huku akimsihi dereva amsubiri kwani anaenda kumfuata mwenzake.

Dereva alisogeza basi hadi kwenye kituo cha crdb kibaha kwa lengo la kusubiri abiria wake. Huku tukiwa tunasubiri ndipo akasimama dada huyo na kudai kua jamaa kashuka na simu yake ya bei mbaya.

Takribani dakika kumi tulisubiri jamaa hakurudi safari yetu ikaendelea..

Nawasilisha.
 
Mh! sasa huo ulikua mpango au? ina maana alilipa nauli ya watu wawili ili apate njia ya kuiba? au walipanga na konda na dereva? kumbuka hii ndio Dar, unatakiwa kuwa makini sana. Pole kwake.
 
Mh! sasa huo ulikua mpango au? ina maana alilipa nauli ya watu wawili ili apate njia ya kuiba? au walipanga na konda na dereva? kumbuka hii ndio Dar, unatakiwa kuwa makini sana. Pole kwake.

hata sisi tumeingiwa mashaka na dereva na konda wake. kwa taarifa ni kwamba hawa watu wanapogundua una kitu cha thamani sana wako tayari hata kupoteza fedha kidogo ili mradi wapate chao.
 
Baadhi ya makondakta siyo waaminifu, huwa wanawafahamu fika wezi hawa, sijui wanapewa nini
 
wakati mwingine wakikuona na kitu cha thamani afu wakakuta gari uliyopanda imejaa, wanapanda basi jingine linaloongozana na nyie mkiingiia sehemu moja ya kula chakula anashuka anakuja kuchukua chake afu anarudi kwenye basi lake.
 
hata sisi tumeingiwa mashaka na dereva na konda wake. kwa taarifa ni kwamba hawa watu wanapogundua una kitu cha thamani sana wako tayari hata kupoteza fedha kidogo ili mradi wapate chao.

Hilo dili! hivi madereva wa mikoani wapaki gari kwa dk 10 eti wanamsubiri mtu ambapo hata huyo anayemcheki hawamuoni, wamekaa tu ha wapi!!, hao walipanga, huyo jamaa karudi ubungo na simu watauza na kugawana hela tu. Any way sijui lakini.
 
mpaka sasa kila mtu ktk basi hili anaamini huo ulikua mchongo wa wafanyakazi wa basi na mwizi.
 
mpaka sasa kila mtu ktk basi hili anaamini huo ulikua mchongo wa wafanyakazi wa basi na mwizi.

Huyo jamaa ni wa pale pale Ubungo na ukute huo ndio mchezo wao sikuzote, mtu hawezi lipia zaidi ya elfu 60 au 70 ya siti 2, ili akaibe kitu asichojiua atafanikiwa kupata nini siku hiyo, nadhani walimuona wakaamua kumlia njuga. Basi tena ndio hivyo tena.
 
kwa mantiki hiyo inaezekana hata nauli hajalipa ila konda katupiga changa la macho.
 
kwa mantiki hiyo inaezekana hata nauli hajalipa ila konda katupiga changa la macho.

Hakuna cha nauli hapo, ila tuache tu maadamu yameshatokea basi, tusizid kuhisi sana. Safari njema mkuu.
 
Back
Top Bottom