Kweli mkuu hawa Tigo wanashirikiana na wezi wa mitandaoni, Nilikopaga kwenye kampuni hizi za Mitandaoni baada ya siku ya kulifa haijafika nikaanza kutishiwa na kutukanwa na wakatuma sms kwenda kwenye namba za watu wangu wa karibu,Sasa mimi sikuwalipa, Sasa kuna siku nikatumiwa pesa nyingi kidogo kwenye line yangu ya Tigo baada ya Dakika tano kampuni niliyokopa wakaanza kunipigia simu ya kuniambia niwalipe deni lao toka siku hiyo nikajua Tigo wanashirikiana na Wezi wa Mitandaoni kutoa Taarifa za Wateja wao, nahisi hawa Tigo wanatoa Taarifa za Wafabiashara wapya waliofungua Tigo pesa mpya kwa Wezi ili waende wakawaibie.