madunda boy
Member
- Mar 26, 2013
- 25
- 12
Kumekuwa na kawaida sana ya baadhi ya watendaji na wenyeviti wa vijiji kuwaibia wananchi fedha kwa kisingizio cha kuchangisha michango ya maendeleo.
Imemtokea jamaa mmoja huko Mbeya vijijini Kata ya Igawilo, kijiji cha Ifiga. Kuna bwana mmoja anayejulikana kwa moja la Komba. Huyu bwana kwa taarifa za awali ilibainika kuwa yeye ni afisa mifugo, lakini amekaimu nafasi ya Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ifiga.
Huyo Komba amekuwa akiingilia majukumu ya viongozi wa kijiji kwa lengo la kujipatia kipato kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho. Kuna jamaa mmoja alifatwa na huyo komba kuombwa Tsh. 20000 akidai ni ya kibali cha ujenzi. Lakini kwa taarifa za kule ni kwamba hakuna utaratibu kama huo bali hizo fedha huingia mifukoni mwake.
Pia amekuwa akichangisha michango kwa kisingizio cha kujenga hospitali lakini kwa taarifa za wananchi hakuna kinachofanyika.
Serikali Mbeya vijijini ijaribu kumfuatilia huyo mtu.