Wizi wa Airtel Money

Wizi wa Airtel Money

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,946
Reaction score
38,668
Usiku huu nimepita kwa wakala kupata huduma ya simu pesa.

Nimekuta varangati ambapo kuna mteja alifika (kama saa nzima iliyopita) kuweka salio katika Airtel Money. Amerejea kwa wakala akilalamika hela haijafika na amecheki salio hakuna iliyoingia. Wakala amemuonyesha ujumbe wa uthibitisho wa kutumwa hela na kutumiwa kamisheni yake.

Wakala ameamua kupiga huduma kwa wateja kuulizia, Mhudumu anakiri kuwa hela imetoka kwa wakala na hivyo hadaiwi na mteja. Lakini mhudumu anaulizwa mbona mteja hajapata salio? wakamwambia aangalie salio lakini ameangalia zaidi ya kukatwa ada hakuna fedha iliyoingia.. Baada ya wakala kumtaka mhudumu kutoa majibu kuhusu huo muamala, mhudumu akamwambia kata simu nishughulikie....

kuanzia hapo simu hazipokelewi na wamedisable option ya wakala kurejesha muamala.

Nimejisikia hasira sana.

Airtel nimethibitisha wanawaibia wateja wao na siyo mtandao wa kuaminika tena.

TCRA inashiriki kwa kufumbia macho malalamiko ya wateja wa mtandao huu
 
Hii mitandao hatari ukiambiwa mambo yanayowakuta wananchi hadi utashangaa, inatakiwa kuripoti polisi na pia TCRA , malalamiko mengi nimeyasikia ni kutoka airtel money. TCRA, chunguzeni haya mambo.
 
Nenda TCRA Kashitaki, na wakupe kibali cha kuwapeleka airtel mahakamani. Udai fidia ya usumbufu. Hela ya bure hiyo mkuu
 
Habari nyingine za kuchafuana Tu...

Huu wizi unaozungumzwa Ni highly overrated,
Hakuna Mtandao wenye Usalama wa fedha Kama Airtel money....
Kwa Mpesa naweza kuelewa hata Tigo wapo vizur pia....

Wahuni wachache wanakosa kazi za kufanya Ni kukaa Tu Na kuleta uhorojo kwenye mitandao...
 
Anaetetea mitandao hii hajaibiwa huyooo maana wanaojifanya wahudumu wezi,wale mawakala wa kusajili laini huku mtaani ndo kabisaa na mawakala wenyewe wanaibiwa sanaa ninawafahamu ndugu zangu zaidi ya watatu wameshaibiwaa
 
Hii mitandao ya simu sio yakuamini kabisa.sasa hapo bora nikuweka pesa kwa wakala ingekua umeihamisha toka bank alafu ikagoma kufika ndo ungeipata fresh.Maana unakuta salio bank limepungua na kwenye simu haijafika ukiwapigia bank wanakwambia tatizo ni mtandao wa simu,ukiwapigia mtandao wa simu wanakwambia kulikua na tatizo la kiufundi kwaiyo pesa zako zimerudishwa bank,ukicheki salio haipo.sasa iyo ela hadi uje uipate ni shida.
 
Habari nyingine za kuchafuana Tu...

Huu wizi unaozungumzwa Ni highly overrated,
Hakuna Mtandao wenye Usalama wa fedha Kama Airtel money....
Kwa Mpesa naweza kuelewa hata Tigo wapo vizur pia....

Wahuni wachache wanakosa kazi za kufanya Ni kukaa Tu Na kuleta uhorojo kwenye mitandao...
Bila shaka ww n wakala wa
Huu mtandao wa makanjanja
Unawatetea makanjanja wenzio
 
Usiku huu nimepita kwa wakala kupata huduma ya simu pesa.

Nimekuta varangati ambapo kuna mteja alifika (kama saa nzima iliyopita) kuweka salio katika Airtel Money. Amerejea kwa wakala akilalamika hela haijafika na amecheki salio hakuna iliyoingia. Wakala amemuonyesha ujumbe wa uthibitisho wa kutumwa hela na kutumiwa kamisheni yake.

Wakala ameamua kupiga huduma kwa wateja kuulizia, Mhudumu anakiri kuwa hela imetoka kwa wakala na hivyo hadaiwi na mteja. Lakini mhudumu anaulizwa mbona mteja hajapata salio? wakamwambia aangalie salio lakini ameangalia zaidi ya kukatwa ada hakuna fedha iliyoingia.. Baada ya wakala kumtaka mhudumu kutoa majibu kuhusu huo muamala, mhudumu akamwambia kata simu nishughulikie....

kuanzia hapo simu hazipokelewi na wamedisable option ya wakala kurejesha muamala.

Nimejisikia hasira sana.

Airtel nimethibitisha wanawaibia wateja wao na siyo mtandao wa kuaminika tena.

TCRA inashiriki kwa kufumbia macho malalamiko ya wateja wa mtandao huu
Haya makampuni yote yana wizi mkubwa , tumwombe Rais wetu asimamie kampuni yetu ya kizalendo TTCL kwani kuna baadhi ya watumishi wa umma walishiriki kuiua,
 
Back
Top Bottom