Wizi/Utapeli/ubabaishaji wa Vodacom!

Wizi/Utapeli/ubabaishaji wa Vodacom!

Ta Nanka

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Posts
1,350
Reaction score
2,083
Inafahamika kwamba ukiwa na kifurushi cha cheka cha voda, mfano cha saa 24, ukinunua kifurushi kingine kabla ya muda wa saa 24 kuisha dakika za maongezi/sms/MB zinaongezeka juu ya zile zilizokuwemo bado kwenye kifurushi.

Lakini saa 24 zikifika hata kama ukikuwa bado na dakika za maongezi/sms/MB vyote "vinaliwa". Sasa hapo ndo voda huwa wananipa kichefuchefu! Kifurushi kinaisha saa 6 na dakika 2 na bado kina dakika za maongezi/sms/MB za kutosha.

Tangu saa 5 na nusu nahangaika kununua kifurushi mpaka muda wa kuisha kifurushi bado sijafanikiwa. Jibu ni kuwa "..ombi lako linashughulikiwa...".

Cha ajabu nikiuliza salio la cheka najibiwa na muda wa kifurushi kuisha ulipofika wala taarifa haikuchelewa kwamba tayari imekula kwangu!! Huu ni upuuzi. Huu ni wizi!

Huu ni mfano mmoja kati ya mingi ya wizi/utapeli/ubabaishaji wa mitandao ya simu ikiongozwa na vodacom. Ndio hapo navurugwa kusikia eti kuna watu ambao wana mamlaka na wangeweza kufanya jambo juu ya wizi huu, lakini sijawasikia/kuwaona wakifanya chochote halafu leo wanataka "urahisi".

Usipoonesha umahiri kwenye mambo "madogo" kiherehere cha kutaka uaminiwe kwa mambo makubwa na mazito zaidi cha nini!!
 
Nahangaika kujiunga na cheka muda wote najibiwa ombi lako linashughulikiwa, VODACOM NJOONI HAPA MTOE MAELEZO
 
Mkuu unachosema ni kweli hiyo issue na mimi iliwahi nitokea,ila wacha tuwatoe ccm madaraka kwanza coz hatuwezi pata mabadiliko chini ya ccm na corrupt goverment yake hata ukipiga kelele ni bure tu
 
Daaah hata mimi muda huu wamenifanyia hivyo hivyo.nilikuwa naongeza vocha kwa ajili ya kujiunga na
kifurushi ili dakika na mb zilizokuwepo niziongezee nikatumia msg ombi langu linashughulikiwa mpaka muda umekwisha wameshalamba dakika zao na mb zao. KWELI HAWA JAMAA WA VODA NI SHIDAAAAAAAAA
 
Mkuu ukisema ufikilie wizi na ulanguzi wanotufanyia hawa jamaa wa mitandao kama vodacom , 0713 , @ex- Zaina unaweza ukapasua simu yako kwa kisirani.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ukisema ufikilie wizi na ulanguzi wanotufanyia hawa jamaa wa mitandao kama vodacom , 0713 , @ex- Zaina unaweza ukapasua simu yako kwa kisirani.
Vodacom imekua pasua kichwa kweli hata maduka yao mawili yaliyokua kariakoo mtaa wa Kongo na Uhuru wameyafunga hivyo ukiwa kariakoo hakuna huduma zao.
 
Last edited by a moderator:
Kwani hamjui maana ya slogan yao?Vodacom Kazi ni kwako..maana yake ni it's up to you(utajiju)
 
Wezi wakubwa hawa,hawajui umuhimu wa wateja wa sh enz sana,wanatuibia tukiona,hata kama kuna shida ya mtandao,kuna haja gan ya kutukata bila sababu?kwann mnaziiba na hamzirudishi?turudishien hela zetu
 
Inafahamika kwamba ukiwa na kifurushi cha cheka cha voda, mfano cha saa 24, ukinunua kifurushi kingine kabla ya muda wa saa 24 kuisha dakika za maongezi/sms/MB zinaongezeka juu ya zile zilizokuwemo bado kwenye kifurushi.

Lakini saa 24 zikifika hata kama ukikuwa bado na dakika za maongezi/sms/MB vyote "vinaliwa". Sasa hapo ndo voda huwa wananipa kichefuchefu! Kifurushi kinaisha saa 6 na dakika 2 na bado kina dakika za maongezi/sms/MB za kutosha.

Tangu saa 5 na nusu nahangaika kununua kifurushi mpaka muda wa kuisha kifurushi bado sijafanikiwa. Jibu ni kuwa "..ombi lako linashughulikiwa...".

Cha ajabu nikiuliza salio la cheka najibiwa na muda wa kifurushi kuisha ulipofika wala taarifa haikuchelewa kwamba tayari imekula kwangu!! Huu ni upuuzi. Huu ni wizi!

Huu ni mfano mmoja kati ya mingi ya wizi/utapeli/ubabaishaji wa mitandao ya simu ikiongozwa na vodacom. Ndio hapo navurugwa kusikia eti kuna watu ambao wana mamlaka na wangeweza kufanya jambo juu ya wizi huu, lakini sijawasikia/kuwaona wakifanya chochote halafu leo wanataka "urahisi".

Usipoonesha umahiri kwenye mambo "madogo" kiherehere cha kutaka uaminiwe kwa mambo makubwa na mazito zaidi cha nini!!

Ndo hivo na hapo walikuchelewesha maksud ili mda uishe. Na walivo washenz sometym mda ukiisha hawakwambii km ukipiga na ukawa una salio lingine wanakukata then ndo wanakutumia msg kuwa ndugu mteja kifurush chako kimeisha
 
vodacom ni matapeli na wezi wakubwa sana kwani hata mm mwenyewe leo nimeweka kifurushi cha internet kwani nimeona kama nimeunganishwa zaidi ya kuambiwa subiri tutakuunganisha halafu kuja kucheki salio nikaona wamelamba hela yote sijui wanafikiri hatuna kazi na hizo hela tunazoweka humo kwa simu? wanaekera wanaudhi kabisa hawa ngoja niwahame nijaribu hii mitandao mipya ya smart nione kama nayo ni kama hawa VODAKOM wanatunyonya wanatuibia hebu muje huku mjibu tuhuma zenu nyie voda
 
Back
Top Bottom