Wizi unaofanywa na Fast Jet na kukwepa kodi

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
866
1,108
Kampuni ya ndege ya FastJet kwa kutumia utaratibu wa malipo online wamekuwa wakiwaibia wateja wake kwa kupokea fedha bila kutoa tiketi ya kusafiri.

Mathalani abiria amefanya booking akiwa songea kwa njia ya online booking fedha yake inakatwa toka kwenye akaunti yake ya tigo au voda lakini Fast Jet hawatoi tiketi.

Wateja wanapofuatilia wanaambiwa watarejeshewa fedha zao na kama wapo mikoani wanahitajika kufika hapa dar.

Uchunguzi mdogo uliofanyika unaonesha kuwa pamoja na kutumia details za fastjet wakati wa kufanya booking na malipo lakini fedha hizo zinapotoka kwenye akaunti ya mteja yaani tigopesa au mpesa inkuwa deposited kwenye akaunti ya kampuni inayoitwa 3G direct payment na sio fastjet moja kwa moja.Kampuni hii imesajiliwa nchini kenya.

Kwa kuangalia kiwango cha malalamiko katika ofisi za fastjet upo uwezekano wa fedha nyingi kuchukuliwa na hii kampuni ya kenya ambayo inajitambulisha kama collection agent wa fast jet.

Maswali ya kujiuliza

1.Inakuwa vipi wateja tutumie particulars za fast jet halafu fedha iingie kwenye kampuni nyingine?watu wa tigio na voda wanasemaje?

2.Je, haya mauzo online yanayopita kwenye kampuni nyingine tena ya kigeni yanawezaje kuonekana na TRA wakati wa kulipa kodi?

3.Je, mamlaka ya udhibiti wa safari za anga haioni uwizi huu unaosababisha usumbufu kwa wasafiri?
 
BOT,TCRA yapaswa kuwa na kitengo maalumu cha kudhibiti transactions za mitandaoni,pesa nyingi sana zinapotea huko.Kuna hizi kamari Betting za mitandaoni pia
 
Back
Top Bottom