Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,842
- 10,765
Kuna vitendo ambavyo ni wizi w wazi wazi kabisa, mbaya zaido vingine hutekelezwa na serikali dhidi ya wananchi wake. Nataja baadhi hapa:
1. Huduma za maegesho ya magari
Mfano UCHUMI building maeneo ya Mtava, mwenye jengo katengeneza parking nzuri kwa ajili ya wateja. Serikali imeweka watu wake watoze kodi ya maegesho tena kwa saa. Mambo haya hufanyika kwenye maeneo mengi tu ya jiji ni kero kubwa na ni wizi. Wamiliki wa magari hulipa kodi mbalimbali mpaka kuliweka gari barabarani lakini ukifunga break tu mtaani, unalipa kodi.
2. Kuingia Ubungo na Msamvu
Yaani ni lazima msindikizaji kulipa ushuru wa kumsindikiza abiria. Halafu ukiindiza gati mfano abiria ana mizigo ama ni mgonjwa basi utalipa ushuru. Huu ni wizi, wenye mabasi wanalipa kodi ya maegesho (stendi) na pia kwenye tiketi kuna kodi ya ongezeko la thamani.
3. Huduma ya vyoo
Huduma ya vyoo vya jumuiya (public toilet) imegeuka biashara kitu ambacho manispaa walipaswa kutoa kwa sababu ni jukumu lao kuhakikisha afya bora za raia wake.
4. Kukusanya taka majumbani
Huduma hii imegeuka kituko tu, huku msisitizo ukiwa ni pesa. Uswazi sanaa ni nyingi zaidi kuliko vitendo na pia kodi hii imekuwa kero kubwa. Serikali badala ya kutoa huduma bureimegeukia biashara.
5. Matengenezo ya barabara mbovu
Kuna tabia ya vijana kujikusanya na kufunga barabara wakidai pesa kwa wenye magari kwa kisingizio cha kufukia mashimo barabarani hata kama hakukuwa na shimo la maana. Vijana hawa hugeuza maeneo yenye kasoro kama chanzo cha mapato na wanaweza kudumu hapo hata wiki nzima.
6. Mizani za madukani na sokoni
Yaani mizani inabeba jiwe la kupimia masaa yote (24/7). Ukitaka ubadili jiwe, mfano ameweka la kilo moja nawe unataka bidhaa ya kilo tano, atahakikisha anaweka jiwe la kg5 kwanza ndipo atoe hilo jingine. Ni heri basi kuweka bei juu kiasi na kutenga haki kuliko wizi huu unaoendelea ni kama hakuna serikali.
5. Kuomba msaada
Mfano umefika kariakoo nawe unataka kujua ni wapi wanauza redio. Ukimuuliza yeyote hawezi kukuonyesha bali atalazimisha akupeleke. Atakufikisha kwenye duka husika lakini jua utapandishiwa bei ili naye aje apate kamisheni. Huu ni wizi.
6. Chenji
Ukitoa pesa kubwa kwenye daladala halafu ukasahau chenji kondakta hawezi kukukumbusha. Badala yake atainua mikono juu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kipato cha ziada. Huu ni wizi. Hata kwenye baa ukilewa basi ujue utazidishiwa bill
7. Tuition
Ingaw yaweza kuonekana ni vyema, lakini kuanzishwa tuition kumepelekea walimu kutofundisha vema mashuleni. Hii imejenga tabaka la kati ya walionacho na wasionacho, imeleta ubaguzi wa kielimu. Sasa basi, mzazi anapolipa ada anatarajia mtoto wake apate elimu bora, lakini hilo halitokei kwa mara nyingi. Huu ni wizi. Masomo ya ziada (tuition) yalikuwepo tangu awali na walimu wa shule husika waliomba wanafunzi warudi shuleni kupata masomo ya ziada hasa kama topic haijaeleweka. Lakini sasa tumehalalisha wizi na kuua elimu.
8. Ada ya usaili
Mfano zinatangazwa nafasi za masomo. Unatakiwa utoe pesa 20,000/= kupata fomu ambayo imechapwa kwa shilingi 60. Tena mfano zinatangazwa nafasi za kuigiza, unatoa pesa ya fomu na bado hupati nafasi, pesa hairudishwi. Huu ni wizi.
Haya ni baadhi tu ya yale ambayo yamepandikizwa vichwani mwa jamii nayo ikayapokea bila kuchuja. Ni mambo yanayoumiza jamii na hivyo kugeuka kero kubwa.