WIZI KATIKA KAMPUNI ZA SIMU! MPesa

WIZI KATIKA KAMPUNI ZA SIMU! MPesa

Ze burner

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
514
Reaction score
83
Habari zenu wadau!

Kama tunavyofahamu, kumekuwa na wimbi kubwa sana la vibanda vya MPesa na vyenginevyo. nazungumzia Mpesa kwa sababu huko ndiko kaidha ninayotaka kueleza ilipotokea.

Nimekutana na wizi wa kimacho macho wa laini yangu ya Mpesa!. Awali niliitumia laini hiyo kufanya kazi eneo XXXX, baadaye nikaamua kuihamishia eneo YYY. niliacha kufanya kazi kama wiki mbili tu wakati nikifanya utaratibu wa kuihamisha laini hiyo kwenda YYY.

Mara tu baada ya kuwasili laini hiyo tuanza kuweka pesa kiasi cha (xxxx.....) hivi. Tukafanya transaction za majaribio zikakubali fresh tunaanza kazi. Siku iliyofuata baada ya kuanza kazi kama transactions mbili tatu hivi laini inakata network. kufuatilia jamaa wanasema eti laini inafanya kazi. siku ya pili hivo hivo wakati laini yenyewe ilikua haina hata network.
Baada ya kufuatilia zaidi wananambia laini eti haijatumika kwa muda mrefu. hivi inawezekanaje wakati tuliacha kufanya kazi wiki mbili na tulianza kazi ikiwa iko vyema sasa inakuaje imeuzwa. Hiyo laini wanayoisema wao imeendelea kutumika kwa zaidi ya mwezi kabla ya mimi kupeleka malalamiko yangu.

Najua nimeibiwa ila kwa misaada yenu naamini hiki hawezi potea bure!

Mawazo tafadhali
 
Mimi pia nimekuta laini yangu ya airtel imeuzwa baada ya kusafiri na kutoitumia less than six months, nilichofanya ni kuachana kabisa na laini hiyo ya airtel na kuwajulisha ndugu zangu kuwa sina laini yoyoe ya airtel kwa sasa. Wachache wanaonitafuta kwenye airtel wananijulisha kuwa kuna jibaba linapokea namba hiyo.
 
Sasa naomna ushauri wenu, nilitaka kujiunga na mabenki kupitia m-pesa hapo imekaa kaaje ili niwe nachukua hala benki kupitia m-pesa au kuweka kupitia m-pesa
 
Kwanza kabisa naomba nikuulize maswali kadhaa ukijibu na majibu ya maswali yako yatapatikina kutokana na majibu yako
1. Unamfahamu agreegator/wakala mkuu wako?
2. Hiyo till/line ya mpesa uliipataje kwa kununua au? Na ninani alikuuzia( si maanishi utaje jina)?
3. Je! Ina soma jina lako/kampuni/duka lako?
4. Ulipeleka lesen ya biashara,Tin no na copy ya id yako??
Jibu hapa kwanza af ntarud
lkn note kuwa wingi wa vibanda
vya mpesa mitaani havihusiki na tatzo lako!
 
yawezekana anatumia tilly ya kuuziwa na mtu na huyo mtu keshaiswap coz vibali vyote anavyo yeye!!kununua tilly kwa watu binafsi bila kupitia kwa agregeter ni hatari sn!!na hata ukifatilia hawakusaidii coz ID ilotumika na TIN vyote sio vyako!majanga matupu!
 
Tanzania sheria ambazo zinaweza kutulinda kwenye E-Banking.Hivyo inakuwa vigumu sana hata pakuanzia.Nakumbuka kuna rai wa kigeni kutoka Bulgaria aliiba fedha za wateja kuto Benki fulani kupitia ATM lakini jamaa akapotezewa na sijui ile kesi iliishia wapi.Kwa hiyo ni muda wa mamlaka husika kuangalia kuhusu hili suala la uwekaji sheria kazi za kuwalinda watumiaji.
 
yawezekana anatumia tilly ya kuuziwa na mtu na huyo mtu keshaiswap coz vibali vyote anavyo yeye!!kununua tilly kwa watu binafsi bila kupitia kwa agregeter ni hatari sn!!na hata ukifatilia hawakusaidii coz ID ilotumika na TIN vyote sio vyako!majanga matupu!

well said mkuu!
Ajibu kwanza hayo maswali ndo tuje na majibu na nita msaidia wapi aanzie otherwise akae atulie sio kuja na title ka gazet la
udaku kwa kupaka matope kampun wakati kosa lako mwenyewe!!
 
wakala wangu mkuu namfahamu vizuri
kuhusu till nilipeleka tin, leseni na kila walichotaka wakanipa ya mtu mwengine baada ya kulumbana nao wakabadili ikawa inasoma kwa jina langu
Niienda kwa wakala kabisa ndani ya ofisi yake ndiyo nikaipata.

msaada plz
 
Back
Top Bottom