Fisherscom
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 1,913
- 1,035
asante sana kwa taarifa mkuu lakini huoni kama na wewe unaendeleza hili tatizo kwa kuogopa kutaja jina la basi/kampuni ambalo tukio hili limetokea? ukitaja jina la basi utawasaidia wasafiri wengine wakae nalo mbali au tuwe makini kwani aliyebaki ni konda peke yake kulinda mizigo ya watu.
Ahh, mie hata nikiwa Schiphol, laptop yangu hachukui mtu..ebo!Hata mimi nilitaka kuuliza....wewe utaachaje laptop kwenye basi? Hata majuu kwenyewe watu hawaachi laptop hovyohovyo namna hiyo.
Hilo ni kosa lilifanyika na mjadala mkali ulifanyika ndani ya basi na polisi Ilula walizungumza hivyo ila ni kiburi cha dereva kuangalia zaidi anakoelekea wakati upekuzi huo ungeweza kufanyika Ruaha.......ilikuwaje mwende ILULA wakati pale Mbuyuni kuna Kituo? Huoni hapa ndipo ulipoiicha Laptop yako Ruaha Mbuyuni?
Abiria mwenyewe ndio mzembe..unaezaje kuacha laptop ndani ya gari??
Ahh, mie hata nikiwa Schiphol, laptop yangu hachukui mtu..ebo!
Point ni kwamba pamoja na ulinzi na umakini uliopo pale, siezi kumuachia mtu laptop yangu ambayo ni kama my best friend kwene sayari hii. I would n't trust anyone with that.mkuu,hata ukiacha hachukui mtu sanasana wataitwa ANTI-TERROR SQUAD au BOMB DISPOSAL UNIT......
Jana nilikuwa safarini toka Dar kuelekea Mbeya kwa kutumia usafiri wa mojawapo ya basi la kampuni kubwa hapa nchini. Safari yetu ilikuwa nzuri toka Dar asubuhi hadi mida ya mchana saa saba tulishuka Ruaha Mbuyuni eneo la Al Jazeera kununua vyakula pamoja na kuchimba dawa. Abiria wote walishuka ndani ya gari kondakta anadai alibaki garini mlangoni kuangalia usalama wa basi lile. Tuliporejea ndani ya basi abiria wawili walidai kutoziona laptop zao pamoja na simu zao mbili. Taarifa zilifikishwa kwa dereva nae akashauri tuendelee na safari hadi Ilula ambako kuna kituo cha polisi. Tulifika Ilula na ukaguzi kufanyika ndani ya gari na nje kwenye eneo la mizigo. Hadi mwisho wa zoezi hilo hakuna kilichopatikana na kuthibitisha vitu hivyo kuibiwa. Muda uliopotea safarini kutokana na wizi huo ni zaidi ya masaa mawili na kupelekea kufika Mbeya saa 3.30 usiku.
Swali langu ni kwa wamiliki wa vyombo hivi vya usafiri pamoja na wahudumu + madereva wamejiandaa vipi/wanalichukuliaje tatizo kama hilo?
Pia wasafiri wanajiandaa vipi kukabiliana na matukio kama hayo ikiwa dhamana ya usalama wa mali zao ipo kwa wahudumu na wamiliki wa vyombo hivi vya usafiri?

Thanks mkuu... you cant just leave laptop like that... watu wengine sijui wanawaza niniAhh, mie hata nikiwa Schiphol, laptop yangu hachukui mtu..ebo!