WIZARA YAFUNGUKA DAWA MPYA YA UKIMWI

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Kigwangalla-1.jpg


Waziri wa Afya, Dkt. Kigwangallah



BAADA ya hivi karibuni dawa mpya ya kupambana na Virusi Vya UKimwi kugundulika na kuanza kutumika nchini Kenya, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini imefunguka, Uwazi lina habari kamili.

Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita, Msemaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Nsachris Mwamwaja alisema wao kama wizara wanafurahi kusikia dawa imepatikana lakini akafafanua kwamba bado haijaingiaTanzania.



Aliongeza kuwa kama dawa hiyo itapitia taratibu zote za usajili, wizara haina tatizo wala kipingamizi.

“Kwa sasa bado haijaingia Tanzania ila ikiingia tu tutawajuza wananchi ila lazima ipitie taratibu zetu za usajili baada ya hapo ndipo ianze kutumika,” alisema Mwamwaja.

Baadhi ya wananchi nchini walionesha kufurahishwa na ujio wa dawa hiyo nchini Kenya wakiwa na imani kwamba zitaingia nchini na kusaidia waathirika wa Ukimwi.

DOLUTEGRAVIR.jpg

Dolutegravir.

Dawa hiyo imeifanya Kenya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuanza kutumia vidonge vya ugonjwa wa Ukimwi ambavyo vinaweza kuboresha afya na kurefusha maisha ya maelfu ya watu wanaosumbuliwa na magonjwa nyemelezi ambayo hayakubali tiba nyingine.Jina la dawa hiyo kitaalamu ni Dolutegravir (DTG), lakini itajulikana kama Tivicay.

Imeelezwa kwamba, dawa hiyo imekuwa chaguo la kwanza la watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa miaka miwili iliyopita katika nchi za watu wenye kipato kikubwa kwa kuwa ina athari chache, ni rahisi kutumia kuliko dawa za ARV zinazotumika sasa (yaani kidonge kimoja kidogo kila siku).

Mwaka 2015, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilipendekeza DTG iwe chaguo la kwanza kwa watu wazima na vijana, lakini hadi siku za karibuni watu wanaoishi na VVU katika nchi kama Kenya walikuwa hawawezi kupata dawa hizo.

Vidonge hivyo, ambavyo vilipitishwa kutumika nchini Marekani mwaka 2013, sasa vinagawiwa kwa wagonjwa 20,000 nchini Kenya kabla ya kupelekwa Nigeria na baadaye Uganda, kwa kusaidiwa na UNITAID, ambao ni wakala wa afya duniani.


DTG ni dawa inayotumiwa na watu wenye VVU ambao hawakuwahi kutumia dawa za kufubaza makali ya Ukimwi ARV.

Dk. Peter Kimuu, mkuu wa idara ya sera za afya na mipango katika Wizara ya Afya Kenya, aliwahi kusema dawa hiyo haina madhara mengi kwa wagonjwa wanaoaishi na HIV na haina hatari ya dawa kuwa sugu.


Alisema DTG ni nzuri kwa vile ina madhara madogo sana kulinganisha na dawa nyinginezo.

UNITAID, mshirika wa mpango huo, imetoa karibu chupa 148,000 za DTG kwa Wizara ya Afya ya Kenya ambayo itaweza kuwafikia asilimia moja tu ya watu wanaoishi na HIV nchini humo.

STORI: GLADNESS MALLYA, DAR

chanzo.Wizara Yafunguka Dawa Mpya ya Ukimwi

Kumbe Dawa yenyewe haitbu huo Ukimwi inakusogeza siku za kuishi mpaka ufike wakati wako wa kuondoka duniani? Bado hapo Wizara ya Afya hamjafanya kitu kabisa.
 
Bashite mwingine in action.

Kumbe essence ya hii habari ni kufurahishwa na kinachoendelea kenya kuhusu hiyo dawa "inayotibu" ukimwi

Swali la kizushi, kwanini hii habari imetolewa na gazeti la "udaku" at first instance? (I stand corrected)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi huyu tangu aseme hajui ajira tz kama n tatizo nimekosa kabisa imani naye... kama tu kitu ambacho ata kwa macho kinaonekana alidiliki kusema vile je ayo mengine ya kitaalam?
 
Nyuzi km izi huwa na washiriki wachache . ila watazamaji wengi .

Matumaini yasokuwepo .

Achen kuuza gemu kizembe.
 
habari za ukimwi hazijawahi kuyaacha magazeti ya udaku salama!
 
Mkuu kama unaweza kusogeza siku kwa dawa isiyokuwa na madhara mengi (minimal side effects) si kitu kidogo. Side effects ya dawa huweza kusababisha mgonjwa kushindwa kutumia hiyo dawa.
 
Hakuna Dawa za kuweza kutibu ukimwi kwa dawa za Mahospitali Wamarekani ni Wasanii. Wanataka kuuza Dawa zao na kuzifanyia majaribio kwa nchi za ulimwengu wa Tatu nchi za Bara la Africa. Dawa ya kuweza kutibu ukimwi ni Dawa za Asili sio dawa za Hospitali hakuna kidonge kitakacho weza kutibu Ukimwi, ni Biashara tu hapo.

''THE PHARMACEUTICAL INDUSTRY DOES NOT CREATE CURES THEY CREATE CUSTOMERS''

(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')
 
Hakuna Dawa za kuweza kutibu ukimwi kwa dawa za Mahospitali Wamarekani ni Wasanii. Wanataka kuuza Dawa zao na kuzifanyia majaribio kwa nchi za ulimwengu wa Tatu nchi za Bara la Africa. Dawa ya kuweza kutibu ukimwi ni Dawa za Asili sio dawa za Hospitali hakuna kidonge kitakacho weza kutibu Ukimwi, ni Biashara tu hapo.

''THE PHARMACEUTICAL INDUSTRY DOES NOT CREATE CURES THEY CREATE CUSTOMERS''

(''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD'')
Crystal clear

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom