MZK
JF-Expert Member
- Sep 13, 2012
- 236
- 306
Leo Wizara ya Nishati na Madini imetoa tamko rasmi ikipiga marufuku usafirishaji wa mchanga wenye madini kwenda nje ya Tanzania. Tamko hili ni pigo kubwa sana kwa wawekezaji wa Madini na Sekta nzima ya madini Nchini Tanzania. Hii inatokana na kuwa Smelting Furnance za Mchanga huo zinapatikana ktk Mashariki YA Mbali (China na Japan) maana ni gharama kubwa na pia zinahitaji malighafi nyingi sana kuziendesha ndo maana hizo Furnance zinapatikana nchi chache sana Duniani. Kwa Tanzania furnance hii ikijengwa inaweza kupata malighafi ya kuiendesha kwa muda wa mwezi mmoja tu kwa mwaka. Ndo mana ht Nchi km South Africa na Ghana ambazo ni wazalishaji wakubwa wa madini na wameanza zamani sana kabla ya karne ya 20 hawajenga hizo Smelting Furnance.