Wizara ya mawasiliano itusaidie wananchi

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,292
Wakati serikali inahama kutoka analog kwenda dijitali iliwaahidi wananchi kuwa zile Channels local zitaendelea kupatikana katika kila king'amuzi na zitakuwa free.

Ni kweli mwanzoni wakati huu mfumo unaanza, Wamiliki wa ving'amuzi walitii hili jambo.

Hata hivyo kadri siku zilivyoanza kwenda, wakaanza polepole kuzibana hata hizi chaneli.

Tunaiomba serikali, iingilie kati suala hili ili kuhakikisha Wananchi wanaweza kupata TV mbalimbali za humu ndani ya nchi katika ving'amuzi wanavyomiliki.

Kiukweli ni Lazima serikali ifahamu kuwa, Taarifa ni muhimu sana kwa wananchi, Na tunategemea kuwa Serikali italisimamia jambo hili.

Kwa mfano Kampuni ya Startimes kwa muda mrefu walikuwa wanaonyesha Local Channels free, ambalo ilikuwa ni katika muongozo wa serikali, lakini hata hivyo sasa na wenyewe wameondoa Chaneli kama ITV na Kubakisha TBC1 na nyingine chache tu ili kukwepa kukwaruzwa na serikali, Lakini hata hii ni janja ya nyani tu, wananchi wanashindwa kufuatilia TV nyingine za local kwa sababu ya mzigo wa gharama.

Au chukulia mfano kampuni ya Azam, wao wanakupa wiki tatu tu ya kuaccess Local Chaneli, then baada ya hapo wanazifungia hizo local channel mpaka ulipie.

Ni dhahiri, Wizara ya Mawasiliano haina Budi kuwasaidia wananchi, kwa kutambua hali halisi ya uchumi wa wananchi.

Je Serikali inataka Wananchi turudi enzi zile za Kumiliki Video lakini kazi yake ni kuangalia sinema za Kihindi tu?

Je TV nazo si ni muhimu kwa ajili ya Ustawi wa Jamii bora, yenye ufahamu?

Je Serikali haioni kuwa Mafanikio tuliokuwa tumefikia ya wananchi kuwa na access ya huduma za television nchini, sasa tumerudi miaka mingi sana nyuma kwa kulimit hata TV za ndani ambazo wananchi walikuwa wanaaccess?
 
Serikali haiwezi kukusaidia Mangi,Sera ya Magu ni kufanya kazi,Hawataki pultebo wala tv,sasaa we nenda bar kaangalie tv
 
Free of charge au dezo, daladala walimu free of charge au dezo, na tv nazo mnataka free of charge au dezo?, Fanya kazi ulipie gharama za tv
 
Free of charge au dezo, daladala walimu free of charge au dezo, na tv nazo mnataka free of charge au dezo?, Fanya kazi ulipie gharama za tv
Acha ujinga ww...!? Huko duniani hakuna mambo ya namna hii, iweje kwa nchi kama Tanzania yenye watu maskini walionyonywa hata tone la mwisho waendelee kubebeshwa mzigo hata usiostahili?
 
Free of charge au dezo, daladala walimu free of charge au dezo, na tv nazo mnataka free of charge au dezo?, Fanya kazi ulipie gharama za tv
Sijui kwa nini nimekosa imani kabisa na hii serikali yangu? Eti siamini hats kidogo kama itaweza kuweka gesi ktk mitung yetu ya kupikia ili being ishuke,pia siamin kama hilo LA vingamuz wanalichukulia kwa uzito mkubwa,na pia siamini kama inajua bei ya umeme ni janga kwetu,au hali hii ndo upinzani? Nikipata kadi ya chama cha serikali sintayaona haya? Nisaidieni wadau
 
Back
Top Bottom