Wizara ya Maji: Maji ya visima Dar sio salama

sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,318
4,399
Ndugu wana Jf,

Nimeona Habari kwenye gazeti nipashe likimnukuu waziri wa Maji Mh Eng Lwenje akiwaasa wakazi wa Dar es Salaam kutotumia Maji hayo na badala yake watumie yale ya DAWASCO

Swali langu Na jakamoyo yangu ni kuwa hivi kweli Mheshimiwa anajua kuwa maji ya DAWASCO wanapata asilimia ndogo sana?

=================================

image.jpeg
 
kwani hayo ya dawasco yanapatikana wapi nje ya darsalama? halafu wana mpango gani sasa? maji yenyewe ya dawasco siyaelewagi kabisa nimecha kutumia kitambo tu
 
Visima vipo aiba nyingi! Visima virefu mita 60 na kuendelea, na vingine vifupi mita 10 hadi 20....sasa waseme wanalenga Visima vipi? Maana watu wanachimba Visima virefu wanaendelea na maisha dawasco hawana habari nayo!
 
Hapo ni visima vifupi ndo vimelengwa..(mita 20-60)...Kama kisima kisima chako kipo mita 60 ni bora ukawa unapima sample ya maji yako kila mwaka, Maabara zipo ,hata pale Ubungo maji zipo au ofis za Dawasco. Visima vingi vyenye urefu wa zaidi ya mita 100 ni safi na salama kwani mkondo wake wa maji sio rahisi kuathiriwa na mauchafu ya nje....Wana Daslam, ngoja niwaambie kitu, wale wanaojenga vyoo vya gorofa, utakuta nyumba ya kawaida lakini choo kina ngazi 6 kama unaenda gorofani vile, ile yote ni shida!! Kile kinyesi kinaenda kuungana na maji yanatembea kule chini, ndo mana mnaambiwa visima vingi Dar si salama. Mfano visima 90% vilivyochimbwa temeke ni Tatizo!! Vina mavi.:rolleyes::rolleyes::rolleyes:o_O
 
wasambaze maji kwa haraka maana naona tangu yafunguliwe, huku kinondoni yamebomoabomoa ardhi mpaka barabara
 
Angeongea hayo baada ya kuhakikisha kuwa wanakidhi mahitaji ya maji kwa jiji la DSM.
Ivi anajua serikali nayo iko na visima vyake uko uko DSM navyo tuvipige chini.
 
Waziri bado mgeni sana katika kazi yake. Muhimu kwanza kusoma mazingira kabla ya kuzungumza lolote Mheshimiwa Waziri. Hivi anajua kuwa katika mkoa wa Dar es Salaam kuna sehemu hata hawajui maji ya DAWASCO yana ladha gani. Uliza uongozi wa DAWASCO kama Kigamboni wanapata huduma ya maji ambayo yeye anaamini ni safi na salama. Ni miaka zaidi ya 50 baada ya Uhuru wa Tanganyika na Kigamboni hawana huduma ya maji ya DAWASCO. Waziri anategemea wapate wapi maji? Ilitakiwa awashukuru sector binafsi kwa kuweza kuwapatia maji wananchi japo kwa gharama kubwa ambayo mwananchi mwenye kipato cha angalau kati anachimbisha kisima na anawapata huduma majirani.

Mh Waziri anatakiwa asikurupuke ila asome mazingira ndiyo azungumze.
 
Ivi nashindwa kuelewa, kama hela za wafadhili (REA) zilitolewa kwa miradi mitatu ambayo ni UMEME, MAJI na BARABARA, Je? mbona mradi wa maji hauzungumzwi na una suasua sana na tangu uanze wa bomba la maji kutoka Ruvu chini hadi leo sidhani kama maji yashafika Dar, chini ya waziri Maghembe kipindi hicho na kwa style hii sijui kama dhana ya maji safi na salama itatimia!
 
Wakati mwingine naitaga AKILI-MATOPE. Ana hakika hayo ya maji ya DAWASA yako salama? mbona mitaani tunakutana na mabomba yaliyopasuka na kuchanganyika na maji machafu? hayo yanaweza kuwa maji salama kwa watumiaji? Hebu tuangalie Dar peke yake: DAWASA ina uwezo wa kuwapatia maji watu wangapi mpaka sasa?? Hakuna haja ya kujadili matatizo kama hatuna uwezo wa kutoa suluhisho.
 
Waziri,

Hapa Yombo (mwisho wa lami,) hakuna maji ya dawasco na tunahitaji kununua dumu kwa 500

Tukiacha maji ya visima,tutumie yapi?
 
waziri mzigo katika serikali ya CCM....obvious serikali sijui itakuwaje
 
Hata sisi tunajua haya maji si salama ukizingatia nyumba za dar zilivyokaa..na pia maji ya kisimi hayapitii purification processes

Hatuna option..Ngoja tufe na saratani za ajabu ajabu
 
Heri mimi nakunywa maji ya dukani kisima, shauri yenu nyie mnaokunywa ya dawasco au ya visima
 
Back
Top Bottom